RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

GLORIOUS CELEBRATION KUANDIKA HISTORIA YAO BUREE IJUMAA




Kundi makini katika muziki wa gospel nchini la Glorious Celebration (G.C) linaloundwa na vijana wenye vipaji vya hali ya juu katika kumsifu Mungu chini ya meneja wao Emanuel Mabisa, Ijumaa hii linatarajiwa kuandika historia ya aina yake pale litakapokuwa linarekodi DVD yake ya kwanza Live katika ukumbi wa kanisa la City Christian Centre Upanga jijini Dar es salaam.

Kundi hilo ambalo limeweza kujitambulisha vyema kupitia album yake ya kwanza ''NIGUSE'' linatarajia kurekodi nyimbo mpya ambazo hazijawahi kusikika na kurekodiwa kabla ambapo waimbaji wote wapo katika hali nzuri kabisa kimazoezi na sauti zao tayari kwa recording yao siku ya ijumaa ambayo imepewa jina la ''Night of Worship'' ikiwashirikisha waimbaji wengine nyota akiwemo John Lisu na kundi lake,Christina Shusho, Pastor Safari na waimbaji wengine.

Emmanuel Mabisa amesema Ijumaa itakuwa maalumu kwa ajili ya recording yao ya DVD na baada ya kumalizika kwa tukio la recording hiyo ndipo wataungana na waimbaji wengine kuendelea na mkesha kwa kuimba pamoja hadi majira ya asubuhi watakapomaliza mkesha huo, na kuongeza kuwa kambi yao ya mazoezi imefanyika vizuri sana na kuwataka watu wote kufika bila kukosa siku ya ijumaa na kujionea kazi nzuri itakayofanywa na watumishi hao katika kumsifu Mungu, hakutakuwa na kiingilio ni bure kabisa.

   CHEKI BAADHI YA PICHA KUNDI LA GLORIOUS CELEBRATION LIKIWA KAMBINI






                      ANGALIA WIMBO ''NIGUSE'' ULIOWATAMBULISHA GLORIOUS

Comments