RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MCHUNGAJI ANTHONY LUSEKELO “MZEE WA UPAKO” KIBANGU AFUNGUKA KATIKA LUNINGA YA CHANNEL TEN


Kuna mambo ambayo Mchungaji Anthony Lusekelo wa kanisa la Kibangu Ubungo aliyazungmza katika luninga na yalinigusa sana. Blogger wenu Rulea Sanga nilibarikiwa sana na shuhuda zake na vile alivyosimulia huduma yake. Na haya ni baadhi ya yale aliyoyaoongea katika kipindi chake cha TUTASHINDA kinachorushwa na Channel Ten hapa Tanzania


"Baba yangu ni Mnyakyusa wa Mbeya, ila alihama Mbeya muda mrefu sana na kuhamia Iringa. Mimi nimezaliwa Iringa na nimekulia Iringa, nimesoma Iringa. Mchungaji Mboya ndiye anayejua historia yangu, tangia alipoaanza huduma yake pale Iringa  miaka ya 60, na watotio wake nimekuwa nao.

Nimebahatika kuwa na watoto wane mpaka sasa ambao ni Nishael, Salome, Elishaddai (Blogger wenu sikumsikia wa nne mnisamehe)

Ubungo Kibangu ambapo huduma yangu ipo, nimefika 1992, nina miaka 20 hapa katika kazi ya Mungu. Mwaka 2000-2001 kanisa lilikuwa na watu 30 mpaka 40. Baada ya Mungu kunitumia katika kufanya miujiza na ishara kubwa na kutumia vyombo vya habari ndipo  huduma ikaanza kukuwa.

Katika wahubiri wanaoishi maisha ya kawaida na sio ya kitajiri, mimi ni miongoni mwao. Ninajuwa kuna matajiri wana magorofa, mapesa katika mabenki na magari ya kifahari.

Ninaamini nguzo kubwa ya uchumi katika kanisa ni sadaka ukiacha miradi mingine. Waumini wananunua viti na magari kutokana na sadaka. Uchumi wa mchungaji ni sadaka. Miongon mwa kazi ya sadaka ni kumtunza mchungaji. Ukiona mchungaji ananona ujue ana waumini walionona. Mchungaji anawaombea mambo yao yanakuwa safi ndio maana wanatoa sadaka nzuri kanisani, na mimi mchungaji ninanona, na inafikia watu wanasema ni tajiri.

Hakuna kanisa linalogawa fedha kwa waumini wake, ila watu wanaenda kanisani kupeleka pesa na maombezi. Ila kanisa linaweza kufungua miradi kama Bank, SACCOS, Shule, Mahospitali na watu kupata ajira.

Sura ya nchi ni rais a sura ya kanisa ni mchungaji, ndio maana bajeti ya Raisi ni kubwa, ndvyo kwa mchungaji, bajeti yake ni kubwa. Sio vizuri kumuona rais anapanda daladala, ndivyo ilivyo kwa Mchungaji hapendezi kumuona anapanda daladala. Mchungaji TD Jakes wa Marekani mwaka 1998 aliingia na ndege nane na akajenga visima vingi kwa fedha yake, hii inatoka na miradi na sadaka za waumni wake.

Kuna watu wanaesema mimi nilitabiri kuhusiana na mvua kutonyesha, mimi sikutabiri ila mamlaka ya hewa ndiyo iliyotabiri. Mamlaka ya hali ya Hewa walitabiri kuwa  kutakuwa mvua kubwa na kusababisha mafuriko kati ya mwezi wa 3 na  itakuwa kubwa kuliko ya mwezi wa 12.  Lakini mimi nilipiga kutokea hali hiyo kwa kuona nchi yangu itaangamia katika majanga makubwa kama barabara na makzi ya watu kuangamia na majanga mengine mengi, kwa kutumia mamlaka ya Mungu nikasimamisha ile mvua waliyotabiri na kutonyesha tena.

Tumepewa mamlaka na Mungu kama vile Yesu alivyokuwa na mamlaka alipokuwa duniani. Kanisa kwa sasa ndio linalotawala nchi. Mungu hufanya kazi nje ya nguvu za mwanadamu wala nguvu za sheria. Mungu sio cheo ila ni sifa. Kuna mamala ambayo Mungu ameweka ndani yangu ndio maana naombea watu wanapona na mapepo yanakimbia."

MUNGU AWABARIKI
-------------------------------------------------------

SHUHUDA ZA WAUMINI KANISA KWAKE KIBANGU UBUNGO.

MGONGO
Nimeumwa na mgongo kwa muda mrefu sana , baada ya maombezi nimepona kabisa.

FIGO
Nimeumwa figo kwa muda wa miaka sita. Leo Mungu ameniona kwa njia ya uimbaji, walipokuwa wanaimba nimejishika baridi sana, na baadae kupokea uponyaji

KUPIGA MIAYO
Nilikuwa nikipiga miayo mpaka taya zinauma sana. Lakini leo Mungu ameniponya baada ya kuambiwa nishike kichwa

KIUNO
nilikuwa naumwa kiuno ambapo nilikuwanahisi kiuno kinawaka moto. Nimetumia maji ya upako na kupata uponyaji.

KIUNO NA MGUU NA KUFA GANZI MIKONO
Muda wa miaka kumi nimeteseka na mikono yangu kupata ganzi, miguu na kiuno kuuma, wakati wa maombi nimesikia kama ubaridi, nikapata uponyaji

MAJINI
Nimeteseka na majini kwa muda wa miaka kumi. Namshukuru Mungu sasa niko safi. naitwa Evalist Chavala kutoka Makongo juu Dar es Salaam.

SIKIO
Nilipokuwa nasikia vyombo vya muziki kanisani vikipigwa masikio yangu yalikuwa yanauma sana. Lakini sasa niko mzima baada ya maombezi.

KICHWA
Uliposema tuweke mikono kichwani nimepokea uponyaji

TUMBO LENYE GESI
Uliposema tuweke mikono tumboni nikapokea uponyaji

UBAVU
Uliposema tuweke mikono kichwani nikaona kivuli kikipita na nimepona.

NYONGO
Nilikuwa siwezi hata kupandiza ngazi, lakini sasa napandisha ngazi bila maumivu baada ya maombezi.

KARIBUNI KANISANI KWETU
Kanisa letu liko Ubungo Kibangu, Ukifika Liverside utaona bango kubwa la Mzee wa Upako Mchungaji Anthon Lusekelo








Comments

Anonymous said…
Nyie bado mnaamini upuuzi huu..
meriiitooh said…
Imani ndio kila kitu katika maisha ya binadam songa mbele baba