RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PAPA ATEUA MAKARDINALI SITA - ROMA WATOKA KAPA, NIGERIA NDANI


Kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani, Papa Benedict wa 16, ameteua makardinali wapya 6, kutoka nchi za Lebanon, Nigeria, Marekani, Ufilipino, Colombia na India, huku makao makuu, Roma wakikosa mtu.
Uteuzi huu wa viongozi hawa wa ngazi ya juu ambao ndio wenye mamlaka ya kuchagua mrithi wa papa, umefanyika leo Jumatano 24 Oktoba, ambapo Papa alikuwa na hutubu katika mikutano yake ya kila wiki, ambapo alilitoa tangazo hili kwa kustukiza bila watu kutarajia.
Tazama viongozi hawa ambao watapandishwa rasmi tarehe 24 Novemba 2012, kuwa makardinali.

Archbishop John Olorunfemi Onaiyekan wa Abuja, Nigeria

Archbishop Luis Antonio Tagle wa Manilla, Ufilipino
Archbishop Ruben Salazar Gomez wa Bogota, Colombia

Archbishop James Harvey (kushoto) wa Mareani akiwa na Papa Benedict XVI

Archbishop Bechara Boutros Rai, wa Lebanon

Archbishop Baselios Cleemis Thottunkal, wa India
Kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani, Papa Benedict XVI


 Uteuzi huu umefanya Ulaya kuwa na jumla ya makardinali 62, Latin America 21, North America 14, Asia 11, na Afrika 11.

Comments