RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RULEA SANGA ALISHWA CHAKULA KANISA LA EFATHA JUMAPILI KUHUSIANA NA ROHO WA BWANA AKIWA JUU YAKO

Namshukuru sana Mungu wangu kwa kunipa chakula cha kiroho kupitia kwa Mtume na Nabii Josephate Mwingia wa kanisa la Efatha Mwenge lililoko wilaya ya Kinondoni mkoa wa Dar es Salaam katika nchi ya amani Tanzania.

Nimewahi kulishwa vyakula na watumishi wa Mungu katika makanisa mbalimbali lakini siku ya jana kwangu ilikuwa ya pekee. Nilifurahishwa na kubarikiwa sana na huduma inayotolewa katika kanisa lile. Chakula kilikuwa kitamu sana mpendwa na ningependa na wewe upate angalau kidogo ya kile nilichokula.

Namuomba Mungu akusaidie kuelewa kile ambacho nimekiandika kutoka madhabahu ya Nabii Josephate Mwingira. Pale ambapo hutaelewa naomba unisamehe na omba Roho Mtakatifu akufungue ili uelewe.

Chakula cha Jumapili hii ilikuwa ni mwendelezo wa chakula cha wiki iliyopita, Somo lilikuwa:


ROHO WA BWANA YU JUU YANGU.
Roho wa Bwana yu juu yangu kwa kuwa amenitia mafuta. Soma Zaburi 45:7.
Tusome pia Wakoritho 1:12:4  Basi pana tofauti za karama, bali Roho ni yeye yule, Tena pana tofauti ya huduma, na Bwana ni yeye yule, Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendae kazi zote katika wote.

Katika kitabu hicho cha Wakoritho tunaona kuna makundi matatu

  1. Karama
  2. Huduma
  3. Kazi

Na makundi haya yote matatu, Bwana ni yeye yule. Katika dunia kuna watalaam wa hali ya hewa ambao wanajua mambo ya mwezi, sayari, nyota n.k. Kuna watalamu wengine wa udongo wanaojua undani wa maji, ardhi n.k na wengine ni watalaamu wa nguvu mbalimbali kama vile nguvu za umeme, mabomu, kompyuta n.k na wote hawa tunawaita wanasayansi.

KAZI
Tunatakiwa kutambua kuwa Roho wa Bwana yu juu yetu kwasababu ametutia mafuta kwaajili ya kazi yake. Mafuta tuliyopakwa na Bwana ni kwaajili ya kufanya kazi yake na sio kwaajili ya kuyahifadhi. Mungu anapenda kuona watoto wake wanafanya kazi na sio kuwa watu wa kupokea tu baraka kutoka kwa watumishi wao bila ya kufanya kazi.

HUDUMA
Tusome Waefeso 4:12- Kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe. Kubaini utendaji wa vitu Fulani. Ili uweze kuumba huduma kunahitaji watu ambao ni watenda kazi. Kuna watu Mungu amewapaka mafuta duniani na amewapa mafuta ya kufanya kazi ili huduma itokee na baadae karama itokee. Watu walio wengi wameishia kwenye karama na wachache kwenye huduma na wachache zaidi kwenye kazi. Tunatakiwa kuwa watu wa kufanya kazi ili baadae tuwe watu wa huduma na hatmaye kutumia karama zetu katika kazi ya Mungu. Walio wengi wanapenda kufanya huduma na wanakimbia kufanya kazi ya Mungu. Eliya aliambiwa na Mungu awapake mafuta watu ili wakafanye kazi. Kuna baadhi ya watu Mungu amewapaka mafuta ili wakafanye huduma.

Tusome Luka 4:18-Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa.

Makusudi ya kuwa na Roho wa Bwana  ndani yetu ni ili:-
  1. Maskini wasikie habari njema
  2. Wafungwa wapate kufunguliwa
  3. Vipofu wapate kuona tena

VIPOFU WAPATE KUONA TENA
Tunapozungumzia upofu tunamaanisha dhambi. Dhambi inapofusha watu wanashindwa kuona yaliyo mema na wanabakia kutenda maovu na machukizo mbele za Mungu. Unapokuwa na Roho wa Munguanakuondoa ule upofu wa kutenda dhambi na kutamani kufanya kazi ya Mungu

Tusome Wakoritho 1:2:9- Lakini kama ilivyoandikwa. Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu), mambo ambayp Mungu aliwaandikia wampendao.

Tunaposema vipofu wapate kuona tena tuna maanisha kuwa ni ile hali ya kumjua Mungu na kuwa katika hali ya utakatifu.

Kuna mamabo ya kuzingatia katika kufunguliwa upofu:-
  1. Mtu anapata kuona maovu.
Ili mtu aweze kuona maovu ni lazima
    • Kulijua Neno
    • Kujua ni wapi Neno lilipo
    • Ni nani analo hilo Neno


KUJUA NENO
Tusome Yeremia 23:28- Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na Neno langu, na aseme Neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema BWANA.

Hapa tunaona ya kuwa kuna wengine wana ndoto na wengine wana Neno. Sio kila mhubiri ana Neno bali wana ndoto. Mhubiri alipooka alioteshwa ndoto ya kuwa mhubiri lakini hakupewa Neno la Mungu kuwa mhubiri. Na hii inatoka na mtu kutamani kuhubiri wakati hana Neno la Mungu na hajaitwa na Mungu kufanya kazi hiyo ila ametamani kuwa mhubiri kwa kuona watu wengine wanahubiri. Wale wenye ndoto ni wale wanakurupushwa na Mungu kufanya huduma kama vile Eliya

KUJUA NI WAPI NENO LILIKO.
Tunapataje Neno la Mungu?  Neno la Mungu tunalijua kwa kufanya yafuatayo:
  • Kusikia. Soma Warumi 10:14
  • Kusoma. Soma Luka 1:3

Neno la Mungu linapoingia ndani yetu linaumba pumzi ndani yetu ili kuleta uhai
Tusome Mwanzo 2:  Mungu alipomuumba mwanadamu alichukua udongo na kuupa pumzi na mwanadamu akawa hai. Pumzi inapoingia kwetu, siri ya Mungu inafichuka. Uhai unasababisha kujua kuelewa siri.

Tusome Wakoritho 1:2:10- lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Mungu hutufungulia mafumbo yaliyofichika na ya sirini ambayo ni ya Mungu wetu. Kuna mambo mengine kwa akili au uwezo wa binadamu ni ngumu kuyajua ila ukiwa na Roho wa Mungu utayajua hata yaliyofichika na Mungu.

Tusome Ufunuo 10:10: Mungu pamoja na kuwa ameficha yaliyo yake bali hufungulia kwa Roho wake. Kuna watu Mungu amewakirimia ya siri ili wapate kuona, kwahiyo wanapaswa kusikiliza yule aliye na Neno lake kwa kuwa na macho ya kuona na baada ya hapo unapata yafuatayo:

  1. Pumzi
  2. Ya sirini
  3. Kuingizwa ufalme
  4. Unapokea ahadi zake
  5. Unaweza kutumia nguvu zake

Mungu anaruhusu ahadi zake kutimiliza ahadi zako unapofikia hatua ya kujua siri. Tusome Wafilipi 4:13- Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. Unayaweza mambo yote baada ya kuona siri za Mungu zimekuwa wazi kwako  na hakuna kuning’inizwa tena na shetani. Ili kujua siri za Mungu unatakiwa kujikana na kujinyima na usikosekane katika ibada za kanisani kwako. Unapotaka kuzitumia zile nguvu za Mungu ili ziweze kufanya maajabu.

NANI ANALO HILO NENO AU NANI KABEBA NENO LA ROHO
Unapata kujua kuwa Roho wa Mungu ni zawadi na kazi yake ni:-
  1. Kukufanya uwe wa tofauti na wengine


MUNGU AWABARIKI
TUTAENDELEA WIKI IJAO

Comments