RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA INAOMBA USHAURI WAKO KUHUSIANA NA TSHIRTS HIZI MPYA

RumAfrica inaomba ushauri wako kuhusiana na hizi Tshirts anbazo inategemea kuziweka sokono hivi karibuni. Kama mdau wangu na unayependa maendeleo ya RumAfrica, Unazionaje..? Kuna Tshirts zingine tutawaletea hivi karibuni, nazo tunahitaji maoni yako...

MADHUMUNI: Wakristo tunatakiwa kushindana na watu wa mataifa katika kumuinua Kristo. Kama watu wanafanya kazi ya kuwatangaza mastaa wa duniani katika nguo mbalimbali, kwanini sisi tunayempenda Yesu tusitumie elimu hii ndogo tuliyonayo kumtangaza Kristo kwa njia ya mavazi?

Huwa nauminia sana napoona watu wakinunua nguo zilizoandikwa ujumbe ambao hauna hata mafundisho katika jamii na wanauza kwa bei ghali sana. Umefika wakati wa kufanya mapinduzi. Huu ni wakati wa Yesu na sio wakati wa Mataifa.

Tunachohitaji ni kuwa wabunifu na tusiweke mashindano katika kazi ya Mungu. Kama wewe ni designer mzuri na unaweza kushindana na watu wa mataifa nitafurahi sana kuona kazi zako, na Rumafrica iko tayari kutangza nguo zako zenye ujumbe wa Yesu.

Pia kama wewe ni mbunifu na huna uwezo wa kutumia komptyuta kutengeneza artwork mbalimbali, tunaomba ubunifu wako ili kuujenga mwili wa Kristo. Watu wa mataifa wanatumia kila njia kuhakikisha sisi Wakristo tunapenda vitu vyao  kuanzia mavazi, vinywaji, vyakula, n.k. Ifike sasa na sisi tuwe na products ambazo zina label ya Yesu. Kwa mfano chupa ya maji iandikwe MAJI SALAMA YA YESU, Nyama za Kopo ziandikwe. SHIBA CHAKULA CHA YESU n.k huu ni mfano tu.

Mungu akubariki



Comments