RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UPENDO HUTHIBITIKA KWA VITENDO NA SIO KWA MANENO





Ninngependa leo nielezee kidogo kuhusiana na upendo. Upendo hauonekani katika raha, bali huthibitika katika shida. Upendo mara nyingi umekuwa ukionekana sana kipindi cha raha, kwa mfano mimi ninavyokuwa nimebarikiwa na Mungu na kuwa na vitu vingi, utakuta marafiki wengi wanakufuata ili watake urafiki na wewe na hatimaye kufaidika nay ale matunda uliyobarikiwa na Mungu, huu ni upendo feki kabisa!! Ukijitahidi kuwakwepa watu wa namna hii wataanza kusema maneno mengi na kusema unaringa na mali ulizonazo. Unapopatwa na matatizo marafiki zako na ndugu zako watakukimbia na kuwa mbali sana na wewe, na unapojitahidi kuwa karibu nao, watajitenga na wengine kupuuzia lile tatizo unalowaeleza. Watu hawa husahau yale mema ambayo uliwafanyia kipindi wao walivyokuwa na uhitaji. Tabia hii huumiza sana hasa kwa yule aliyekuwa anawasaidia kipindi wanauhitaji.

Upendo una sura mbili wakati wa raha watu walio wengi wanarithika na upendo huo. Upendo unakipimo chake, na kipimo hicho huonekana wakati wa shida. Unapopatwa na shida na ukaona rafiki yako yuko bega kwa began a shida yako, hapo utaamini kuwa kuna upendo wa dhati ndani yake. Yule anayeweza kusimama na wewe wakati wengine wanakukumbia huyo ndiye ndugu yako na unapaswa kumheshimu katika maisha yako ya hapa duniani, kwa maana nakuokoa katika magumu unayopitia, yule amabaye hapendi kuona unaharibikiwa hata mkikosa hapendi kuona unateseka huyo ndiye mwenye upendo wa ukweli.

Watu duniani wanahangaika hupenda vinavyopendeza na kutopenda visiovopendeza. Wapendeni wanaowaudhi na Baba yenu atawapa dhwabu na Mungu atasema hawa wafanya vizuri. Wapendeni wanawakosea na acha kuwasengenya, na kuwaombea wanapopatwa na makubwa. Upendo hauthibitiki wa kwa maneno bali kwa vitendo na hauonekani kwenye raha.

Songa mbele ndugu yangu usijiali maneno ya watu yanasemaje bali wewe muangalie Mungu tu ndiye atakayekuokoa. Rafiki yako hata asipofika kukufariji katika magumu, wewe simama na Mungu na kuwa na amani ndani ya moyo wako. Mbali na hayo unayofanyiwa na rafiki zako, zidi kuwaombea na kuwapenda, sahau yote uliyofanyiwa bali songa mbele na macho yako yamtazamae aliyejuu.

Usipende kuwa mtu wa kisasa, ukifanya hivyo utakuwa unamuudhi Mungu. Wanapokuchukia wewe zidisha upendo kwao. Najua ni ngumu sana kuona unampenda yule aliyekuudhi, lakini wewe mwambie Mungu na kuonyesha utofauti kwa kuwapenda.

Kuna watu wengine wanaishi kwa ndugu zao na hao wamewafanya ndiyo kila kitu. Wanasujudu kama miungu yao, hata wanaposemwa maneno mabaya wamekuwa wavumilivu, wakiogopa kuwa wakijibu vibaya wanaweza kufukuzwa nadani ya nyumba. Jambo hilo unalofanya wafanya vizuri kwa kujifanya mpole. Onyesha upendo wa thati na Mungu antakuonyesha kuwa yeye anaweza kuwasaidia wanyonge katika magumu yao.

Comments