RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MAZISHI YA SHAROMILIONEA SIKU YA JANA


Jana Tarehe 28 November ndo mwili wa marehemu Sharomilionea ulizikwa,ni ngumu kuamini inauma lakini ndo hivyo ameshatangulia mbele ya haki.Ndugu zake walikuwa na uchungu sana ukizingatia alikuwa mtoto wa kiume pekee na wa mwisho.Kwa mujibu wa Mama Mdogo wa Marehemu Bi Mahija Mkiety,Sharomilionea alizaliwa Muhimbili Dar es salaam lakini kulelewa Tanga na kusoma alisoma Tanga shule ya Msingi Lusanga mpaka darasa la 7 baada ya hapo hakuendelea na masomo tena.Alisema Alizaliwa tarehe 15 mwezi wa 3 mwaka 1987.

Hapo ni mtaani kwakina Sharomilionea Kijijini kwao Lusanga,huko Muheza Tanga
Msanii Roma akiwa kwenye mtaani hapo ambapo ni hatua chache kutoka nyumbani kwao
Kinamama wakiwa msibani
Wazee wa kijijini kwa kina Sharomilionea wakiwa kwenye mazishi
Wasanii wa maigizo
Mama Mdogo wa Sharomilionea na Dada mkubwa wa Sharomilionea Salma Ally
Muhogo Mchungu
Msanii wa maigizo Bi Mwenda

Anayeonekana katikati ni Dada yake marehemu Sharomilionea wa kwanza.Kutoka kushoto ni mtoto wa mama mdogo wake na anayefuatia ni mama mdogo wake
 Ndugu zake wengine
Huyu kaka alikuwa akilia sana, ni kati ya ndugu wa marehemu wa karibu hata kuongea alikuwa hawezi
Baadhi ya wasanii wa BongoMovies Irene na Rose Ndauka
Yusuph Mlela,Dj Mackay wa East Africa Radio na Sajuki
Wa kwanza ndo rafiki wa karibu wa marehemu ambaye alimuazima gari lake anajulikana kwa jina la Moud

ANGALIA MATUKIO MENGINE KWA KUBOFYA "Read More"
HAPO CHINI



Mwenye shati jeupe ni Waziri wa Njenje,nyuma Mzee Majuto na msanii wa maigizo Mzee Chilo
Tiny Dad
Nape na Viongozi wengine wa CCM walikuwepo
Baadhi ya wasanii na watu wengine wakiwa kwenye eneo ambalo amezikwa Sharomilionea
Roma
Kaburi ambalo liko nyuma ya nyumbani  kwa kina Sharomilionea Tanga,Muheza na hapo ndipo ambapo mwili wa Sharomilionea ulipopumzika milele
Watu wengi wa hapo Kijijini walikuwa wanataka kupiga picha na wasanii baada ya mazishi,hapo ni Kitaani kwa kina marehemu Sharomilionea,ni Rose Ndauka akiwa na wasanii wa kundi la TNG kutoka Tanga.
Mimi,TNG ndani ya Kitaa cha kina Sharomilionea
 Mzee majuto 
 Hii ndio nyumba ya milele ambapo mwili wa Hussein (Sharo) utapumzishwa hapa
 Mama yake mzazi Marehemu Hussien (Sharo)
 Mama mzazi na Dada yake Marehemu
Jeneza likiinuliwa

Comments