RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWIMBAJI MACHACHARI JIJINI DAR ES SALAAM NA ALIYEBAHATIKA KUZAWADIWA GARI AKIWA MTOTO MDOGO KUTOKA NA KUIMBA, JESSICA HONORE KUTOKA KANISA LA WORLDALIVE AFUNGUKA NA KUELEZEA ALIKOTOKA ALIPO NA ANAKOENDA…..





Rumafrica ikiwa katika harakati zake za kutafuta maisha ilibahatika kukutana na Jessica Honore maeneo ya Sinza Afrikasana akiwa katika harakati za maisha. Rumafrica ilimuomba Jessica kufika katika ofisi za Rumafrica ili waweze kuongea machache kuhusiana na huduma yake ya uimbaji. Na haya ndiyo mazungumzo yalivyokuwa:

 Mwalimu na mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania, Jessica Honore

RUMAFRICA: Hello Jessica, Bwana Yesu asifiwe

JESSICA HONORE: Ameni Rumafrica…mzima wewe???!!!

RUMAFRICA: Rumaafica iko safi Mungu anaiwezesha. Jessica umekuwa kimia sana ila leo tuelezee ujio wa albamu yako mpya ambayo tumesikia baadhi ya nyimbo zikipigwa maredioni.

JESSICA HONORE: Kwa muda mrefu nilikuwa kwenye mchakato wa kumalizia kufanya albamu yangu ya kwanza, tangu Jessica mmemfahamu. Kiukweli nimechukua muda mrefu ambapo albamu yangu ingekuwa tayari iko sokoni. Kwa sasa albamu yangu iko mwishoni kumalizika na imebakia sehemu ndogo sana kui-release. Albamu yangu ina nyimbo nane (8) imebeba jina la SITANYAMAZA. Mwezi wa Februari 2013 nategemea kufanya tamasha la ku-Preview albamu yangu.

RUMAFRICA: Kwanini albamu yako umeiita SITANYAMAZA?

JESSICA HONORE: Nimeamua kutumia jina hilo kwasababu nyimbo yangu ni ya kumsifu Mungu nikimaanisaha muda wote mimi nitakuwa mtu wa kumsifu Mungu iwe asubuhi, mchana, usiku mimi sitanyamaza kumsifu Mungu wangu. I just praise God all the time. Kwa upande mwingine nimekuja Fully, kwahiyo sitanyamaza tena

RUMAFRICA: Maana ni muda mrefu sana umekuwa kimia sana, na watu wengi walikuwa wakijiuliza Jessica Honore yuko wapi?..Tuambie baada ya kutoka hii albamu yako ya kwanza, una mategemeo yoyote yakutoa albamu nyingine?

JESSICA HONORE: Baada ya albamu yangu hii ya SITANYAMAZA kuitoa, nategemea mwezi wa nane (8) 2013 nategemea kufanya LIVE concert.

RUMAFRICA: Albamu yako ina nyimbo ngapi:

JESSICA HONORE: Ina nyimbo nane (8)

RUMAFRICA: Kwanini albamu nyingi za injili hapa kwetu Tanzania, mara nyingi zinakuwa na nyimbo kuanzia tisa (9) kushuka chini na kwanini isiwe zaidi ya tisa (9)?

JESSICA HONORE: Mimi nadhani ni mfumo Fulani ambao wamimbaji wengi wanafuata, kwasababu wanaona waimbaji wengi wanakuwa na nyimbo tisa kushuka chini. Lakini wenzetu wa nje ya Tanzania utakuwa wana nyimbo ishirini (20) na kuendelea mbele katika albamu moja. Sisi tunakuwa na nyimbo kiasi hicho kutoka na mfumo wetu jinsi ulivyo, mwingine utaona kuweka nyimbo nyingi ni kama anapunjika katika soko la kibiashara, kwani anaweza kutunga nyimbo nyingi na akaweka zote katika albamu, mwisho wa siku gharama za uuzaji zinakuwa kama yule mwenye nyimbo tisa katika albamu yake. Utunzi na wenyewe ni kazi, unatumia muda mwingi sana na unaumiza kichwa kuuteneneza wimbo. Pia gharama za studio zinakuwa kubwa.

RUMAFRICA:  Rumafrica ingependa kujua baadhi ya nyimbo zilizoko katika albamu yako ya SITANYAMZA

JESSICA HONORE: Yah..kuna nyimbo moja ambayo nime-release sasa hivi na inaendelea kupigwa katika vyombo vya habari, inaitwa NAPOKEA, nah ii nyimbo nimeifanyia Video na Audio. Nyimbo zingine ni:
  1. juu yako nitaimba
  2. Sitanyamaza
  3. Mfariji
  4. Uwepo wako na nyingine nyingi
RUMAFRICA: Wasomaji wangu wangetamani kujua style ya uimbaji umefanya katika albamu yako na kwanini umefanya hivyo?
Jessica Honore

JESSICA HONORE: Mhhh…nimechanganya kidogo, kwani kuna Southern beat, Kwaito, Chakacha na slow. Mimi ni Mwafrika na Africa kuna vitu vingi, na hizo style hizo ziko Africa, kwahiyo nimeamua kuchanganya ili kila mtu Africa aweze kuipenda kazi yangu na pia ujumbe uweze kumfikia barabara

RUMAFRICA: Ni studio gani umefanya hii kazi yako?

JESSICA HONORE: Nimefanya katika studio za SHEKINAH STUDIO Sinza Afrikasana hapa jijini Dar es Salaam. Ila nategemea kufanyia mixing Kenya kwasababu nataka kuweka utofauti kidogo na kuongeza radha kutoka nchi nyingine.

RUMAFRICA: Ni matatizo gani umekumbana nayo katika zoezi zima la kutegeneza albamu yako?

JESSICA HONORE: Matatizo ni mengi, lakini kuna hili na nenda rudi nenda rudi za studio kutokana na umeme kukatika, kubadilisha ratiba, programa zangu nyingi zimeharibika kutoka na  ruti za kwenda studio, na inafika wakati unachoka kabisa. Hali hii imeharibu sana mipangilio yangu niliyoipanga,

Ukiangalia albamu yanugu imekuwa katika maandalizi ya miaka miwili sana na ndio maana nilikuwa kimia sana. Na kukaa muda mrefu kama huu nikutokana na mimi mwenyewe kutaka kuja na kitu bora. Kwahiyo utaona leo naenda studio naingiza sauti na ninarudi nyumbani, na nikirudi nyumani ninaanza kufanya mazoezi na kuiboresha nyimbo yangu, nah ii inanisaidia mimi ku-improve. Sasa nikirudi studio naona ile sauti niliyoingiza haiko katika kiwango kile nataka na kinachofanyika ni kufuta na kurudia tena. Mimi nilikuwa sijisikii vibaya kufuata nyimbo zangu ninapoona kuna udhaifu Fulani kwasbabu nilikuwa nataka ku-improve katika uimbaji wangu.

Lakini sasa wakati umefika, na nimeona huu mchezo wa kufutafuta nyimbo niuache na nitazame kazi.

Na upande wa fedha, halijanisumbua sana na sio kama nina pesa sana na sina mtu aliyeweza kuni-sponsor ili niingie studio. Mimi ninasema ni Mungu tu aliyenisaidia kupata fedha na kuingia studio, ni kama vile Mungu alivyonisaidia kuishi ndivyo alivyonisaidia kupata pesa za studio.

RUMAFRICA Kwani wanamuziki wengi wanapokuwa wamealikwa kufanya huduma katika kanisani Fulani na wanapokuwa wamefanya huduma yao ya uimbaji wanaamua kutoka na kwenda kufanya mambo yao mengine wakati ibada bado inaendelea?

JESSICA HONORE: Mimi naweza kusema kwamba, kuna matatu, yupo after money au hajui kujisimamia (hajui kusema ndio au hapana) au mchanga kiroho. Pesa imekuwa ikim-control. Kwahiyo haoni umuhimu wa kukaa chini na kusikia au kula Neno la Mungu. Kwangu mimi nafanya hivi, Jumapili huwa najua siku ya ibada kwahiyo huwa na kuwa nasehemu maalum ya kwenda kuabudu na ninaabudu, na kama nimealikwa katika hilo kanisa nitaimba na nitabaki maka ibada iishe. Na niwe nimeamua kuwa na hudumu pale na ninakula neno pale na nikashamaliza ninaenda sehemu nyingine na kama ratiba zinaingiliana, itabidi niamue kuchukua kimoja na sio vyote viwili kwa wakati mmoja.
RUMAFRICA: Kuna baadhi ya waimbaji wanaalikwa katika kanisa Fulani na wanapewa hata pesa ya nauli ila cha kushangazaa yule mwimbaji hafiki na anazima simu yake, wewe unazungumziaje hili?

JESSICA HONORE: Huyo ni mwizi kwasababu wewe utafanyaje kitu kama hicho kama mtumishi na kioo katika jamii. Unaweza kufanya kwa mtu mmoja, ila habari zako zinasambaa, na hatma yake wewe kuchafua jina lako, na unafungia watu mioyo yao kupokea ile huduma yako. Kwahiyo the end of the time unakuwa hauna soko, huna faida katika ufalme wa Mungu kwasababu huduma yako inakuwa ishanfungiwa. Itafika mwishowa siku huduma yako itakuwa inasikika na familia yako tu na utakuwa unajiimbia nyumbani kwako.

RUMAFRICA: Hii albamu yako ya SITANYAMAZA ni albamu ya ngapi

JESSICA HONORE: Ni albamu yangu ya kwanza.

RUMAFRICA: Well !! ….Umeanza kuimba lini?

JESSICA HONORE: Nimeanza kuimba muda mrefu sana, ila rasmi nilianza kuimba mwaka 2005. Kukaa kwangu muda mrefu kuanzia 2005 mpaka 2012 nilikuwa nataka kwanza kukua katika muziki, na kusema ukweli siku hadi siku nilikuwa naendelea kukua. Na nimekuwa chini ya watu kama RUGE wa Clouds FM, na ukizingatia 2005 nilikuwa bado mdogo na ninasoma, na nillikuwa chini ya mwongozo wa kiroho kutoka na umri wangu. Nafikiri Mungu alikuwa ananiandaa ili kufikia hatua kwamba the time nikija kutoa kitu kiwe kimeshiba. Ningeamua kuingia katika muziki kama nilivyoamua sasa kwa kipindi kile, najua kungekuwa na hitilafu.

RUMAFRICA: Kuna tetesi kuwa umeshawahi kuzawadiwa gari katika mashindano Fulani ya ya uimbaji, naomba utuhakikishie?

JESSICA HONORE: Habari hizo ni za ukweli kabisa. Yalikuwa ni mashindano ya Gospel star search, na kipindi hicho nilikuwa nasoma nikiwa darasa la saba. Yalipotokea mashindano hayo nikaenda kushiriki na mwisho wa mchakato nikashinda. Mashindano haya yalikuwa yanahusisha watu wa mablimbali nimikimanisha watoto, vijana na hata wazee, kulikuwa hakuna makundi ya umri. Kipindi hicho nilikuwa na umri wa miaka kumi na tano (15). Namshukuru Mungu nilishinda lile gari na baada ya kulipata lile gari likanisaidia katika harakati zamgu za kimasomo

RUMAFRICA: Mbali na muziki ni kazi gani zingine unafanya?

JESSICA HONORE: Ninafanya Jingles, na nishafanya matangazo mengi Radio ya watu Clouds FM, Kampuni ya simu Vodacom. Pia mimi ni mwalimu muziki na nimejikita sana katika upande wa sauti (vocal) . Kanisani kwangu WorldAlive huwa ninafundisha Praise Team na kuna kanisa la Huduma ya Akuzam lililoko Posta hapa Dar es Salaam. Na pia ninafundisha watu wengine binafsi.

RUMAFRICA: Ni kweli katika familia yenu ni waimbaji wote?

JESSICA HONORE: Ndiyo sisi sote ni waimbaji wa nyimbo za injili. Katika sisi kuna kaka zangu watatu wanapiga gitaa wa kwanza ni James Honore ambaye anafanya hizi tamasha za Holy Base Giter na anafanya vizuri sana kwangu mimi ni the best in Tanzania na niko so proud na yeye, wa pili ni anaitwa Jacksoni anapiga solo na Rhythm na pia ni mwimbaji, watatu ni John ambaye niko naye pale kanisani kwetu na yuko katika Praise Team, huwa tunapenda kumuita kilaka kwasababu  anaweza drums, keyboard, Base gitaa, mwimbaji, ni music composer anaweza akamtengenezea mtu muziki.

Na wao wattau, James, John na Jackson wameshatoa albamu inayoitwa WACHA MUNGU BAND, lakini brother wangu wa mwisho John ameshamaliza albamu yake..soon atai-release sokoni.

RUMAFRICA: Umeshafikiria kuimba wote wane kama familia na mkatoka na albamu yenu as family?

JESSICA HONORE: Inwezekan na ni wazo zuri, lakini ni vizuri kwenda kwa Roho Mtakatifu na sio kwa kuiga eti kwasababu mtu Fulani kafanya hivi au familia Fulani imefanya hivi halafu na sisi tufanye. Wat mnaweza mkawa familia moja na mnafanya kitu kimioja lakini mmeitiwa tofauti tofauti. Mimi ninavyotakiwa kuimba inaweza kuwa tofauti na John alivyoitiwa na Mungu. Labda ifanyike kwasababu tunataka kutengeneza ule umoja kama wait wa familia, ila kiukweli sijawahi kuambiwa na Roho Mtakatifu kuwa tufanye kitu kama hicho. Kwahiyo sitaki kukurupuka na kuunda vitu ambavyo sijaambiwa

RUMAFRICA: Unaweza kufanya huduma yako ya uimbaji bila ya malipo?

JESSICA HONORE: Kiukweli ninaweza, na nimeshafanya hizo nyingi sana, na sio kwasababu sasa hivi ndio naingia kimuziki zaidi ndio sitafanya bure..hapana…Kuna wakati mwingine unafanya huduma na unakarisikia ila hudumainasonga mbele. Ninamshukuru Mungu kwa yale yanayotokea, wakati mwingine unaona hizi ni dharau, lakini unaamua kufanya kwasababu nimefanya kwa Bwana.

Laniki tunakuwa jamani, tunatoka utukufu mmoja na kwenda utukufu wingine. Na siku hizi huduma yangu imekuwa sio kama zamani, Mungu amenipa neema ya kuwa na Kikundi changu, ambapo binapoenda kuhudumu naenda nao.

Sasa hivi nafanya LIVE Music, niko mimi na wapigaji wangu. Kwahiyo utakuwa unanionea, ukinnita na kunifanyiza kazi bure. Na ujue ninapokuja kufanya kazi na wewe ninakuwa nimebeba watu na siko mwenyewe…Kwa kiufupi haipendezi.
 
 Dada Jessica Honore
RUMAFRICA: Tupo jina la Band yako

JESSICA HONORE:: sina jina, na sijaipa jina, kwasababu mimi ni solo artist, kwahiyo nina watu permanent ambao ninafanya nao kazi, na wtu hawa wanatoka makanisa tofauti na kanisa langu la WorldAlive. Na mahali amabpo tunakutana katika mazoezi ni katika kanisa la WorldAlive Sinza Mori kwa Mchungaji Deo Lubala. Tunafanya mazoezi kila Jumatatu, Ijumaa na Jumamosi


\RUMAFRICA inakushukuru kwa kupoteza muda wako na kuwajuza wadau wa Rumafrica kili ulichonacho.

Comments