RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NABII FLORA PETER SIKU YA JANA ASUBUHI AHUBIRI JUU YA MAONGEZEKO KATIKA MADHABAHU YA MUNGU

Ibada hii ilifanyika katika kanisa lake kwa lengo la kuwakumbusha waumini kuwa Mungu anahitaji kuona ongezeko katika madhabahu yake. Na haya ndiyo aliyohubiri Nabii Flora Peter

 
Nabii Flora Peter akihubiri juu ya Ongezeko la Shekeli nyumbani mwa Bwana

Leo ni siku pekee ya kurejesha fedha na shekeli katika madhabahu ya Bwana. Ni siku ya maongezeko, yakuongezeka kila maeneo. Unaenda kuongezeka katika biashara zako, katika uchumi wako,  uzao wa tumbo lako, unakwenda kuongezeka kila maeneo.

Mbarikiwe watumishi wote akiwemo Anna Makinda, mtumishi Kenesi na mtumishi Joshua. Wote mliosimama hapa kusikia neno la Mungu, Mungu awabariki

Salama za Nabii zinatoka katika kitabu cha Kutoka: 3:6, Mimi ni Mungu wa baba zako, Mungu wa Ibrahimu , Mungu wa Yakobo, Mungu wa Isaka, . Musa akaficha uso wake, aliogopa kumuangalia Mungu. Bwana akasema hakika nimeyaona mateso ya watoto wangu, nami nimesikia kilio chao, kwahiyo kwasbabu hiyo nimeshuka nije niwasaidie yale mateso wanayopata na kwa wasimamizi wao. Kwa maana nayajua maumivu yao, mimi nimeshuka ili niwaokoe, niwapandishe katika nchi njema. Nitakupeleka katika nchi ijao maziwa na asali. Nitamhamisha, Mkanani, Mhiji, na Muamori…Tazama kilio cha watu wangu Israel, kimenifikia na nimeona mateso walioteswa Wamisri, haya basi ninakutuma sasa kwa Farao ukawatoe watu wangu wa Israel katika. Nitakutoa katikati ya maadui, nitakuficha katika mbawa zangu, ili hayo mateso ya Wamisri yasikupate tena katika nchi hakuna kuzaa mapooza, hakuna atakaeitwa tasa, kwasbabu Bwana ndiye mchungaji wangu na sitapungukiwa na kitu, kwasababu katika majani mabichi hunilaza na kando ya maji matulivu huniongoza, huniwisha nafsi yangu na kuniongoza na hkatika haki huniongoza kwa jina lake. Naam nijapopita katika bonde la mauti, hakika mimi sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami, hakika Bwana ni gongo langu na fimbo ya kunifariji. Wanabeza mbele yangu na machoni pa watesi wangu, ulinipaka mafuta kichwani pangu, na kikombe changu kinafurika, hakika wema na fadhili zitanifuata
 
Nabii Flora Peter akiwa na mtafsiri wake wakati wa ibada
Bwana anasema, “Ukimjua Bwana utajengwa na ukiondoa udhalimu mbali na hema yake…Bwana anasema asubuhi ya leo, mjue sana Mungu ili upate kuwa na amani” Kumbe mtu anayemjua sana Mungu ana amani ndani yake na hana la kumkwaza na ndivyo mema yatakavyokujia. Na mimi nakuambia ya kuwa wale waliokudharau kuhusu fedha, Mungu atakubariki mno, watu watakuogopa waliokudharau, wataona aibu, watatafuta wafiche nyuso zao, wataogopa kukutazama kama Musa alivyoogopa kutazama uso wa Mungu. Nakuambia utatisha kama nini, maisha yako yatabadilika, utainuliwa asubuhi ya leo, utarudishiwa kibali kile ulichonyang’anywa, kibali cha Yusufu, utajiri, utapewa baraka ya Bwana. Bwana atakufanikisha wewe uliefika hapa kanisani, ataenda kukubariki, Yesu anaenda kukusimamisha wewe upya, ataenda kukuinua Bwana.

Bwana anasema nitaibariki Yerusalem na tena nitawabariki hata wateule wangu walisikilizao neno langu. Bwana anasema asubuhi hii kuwa ameyaona mateso ya watu wangu. Naye Bwana amesikia kilio chako mtu wa Mungu. Hata kama unaomba huko unamadonda, Ukimwi, kansa na mateso mengi lakini Bwana anasema kwa kutumia watesi wenu, nimeyaona mateso yenu. Ameshuka asubuhi ya leo ili atuponye, atuokoe, watoto waliopotea wapate kupatikana. Mungu atakupeleaka katika nchi njema upate kufurahi, kufanikiwa. Bwana anasema anakutoa katika UKIMWI, katika magonjwa, nakutoa katika hali ya kansa, na katika hali ya ukame katika jina la Yesu. Nakutoa katika mkono wa Kimungu katika mkono wa Farao. Ufukara ni Farao amekalia maisha yako. Farao ni adui, magonjwa, umaskini, kukosa kazi. Farao amekufanga, ninatuma Neno la Mungu likutoe katika kifungo hicho. Wat wnasema hautanyonyesha, lakini utanyo.

Ndugu yangu ukimwamini Yesu hautapungukiwa na kitu, utakapopita katika misukosuko mingi ya ndoa, kazini, watu wanakutenga na kukukataa. Amini jina la yesu hutapungukiwa na kitu, jina la Yesu ni jina pekee, ukiamini jina hili utabadilishwa na kugeuzwa, mimi nimeamini nimebadilika, kuokoka ni kubadilika wapendwa

MUNGU AWABARIKI

Mwandishi
Rulea Sanga
RumAfrica

KAMA UNGEPENDA KUJUA MENGI KUHUSU MATENDO MAKUU YA MUNGU KWA KUPITIA NABII FLORA PETER INGIA KATIKA BLOGU YAKE ILIYOTENGENEZWA NA RumaAfrica...


www.nabiiflora.blogspot.com










Comments