RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PALESTINA WASHANGILIA DUNIA KUWATAMBUA, ISRAEL NA MAREKANI WAPINGA


Furaha, nderemo na vifijo vimeibuka katika mitaa ya taifa la Palestina, baada ya nchi wanachama wa umoja wa mataifa kupiga kura na kuipitisha nchi hiyo hiyo kama taifa. Nchi mia moja thelathini na nane ziliunga mkono hatua ya kuitambua Palestina kuwa nchi ambayo si mwanachama wa Umoja wa mataifa lakini itaruhusiwa kushiriki katika shughuli za umoja wa mataifa, kama mwangalizi, bila ya kuwa na uwezo wa kupiga kupigia kura maamuzi.
Sherehe kila mtaa.  ©The Independent
Mataifa tisa yakijumuisha Isarael na Marekani yalipiga kura ya kupinga mpango huo huku mataifa arobaini na moja yakikosesakana kwenye kura

Baraza la umoja wa mataifa limepitisha kwa kauli moja kwa wingi wa kura kupandisha hadhi ya eneo la Palestina.
Kura hiyo yenye umuhimu mkubwa sasa inaiwezesha Palestina kuwa na ushirika na umoja wa mataifa na mashirika mengine kama vile mahakama ya ICC.
© AP Photo/Majdi Mohammed
Mwandishi wa BBC amesema kuwa wapelestina wanaweza kutumia nafasi hayo kuishataki Israel kwa kusababisha visa vya dhulma dhidi ya ubinadamu katika ngome yake.
Kutambuliwa kwa Palestina kama taifa, bado hakutabadili mambo haraja, kwani eneo ambalo umoja wa mataifa unatambua kama sehemu ya Palestina, 'West Bank', Ukanda wa Gaza, na Jerusalem Mashariki vikingali katika utawala wa Israel. Lakini hilo, halikuwazuia Wapalestina kusheherekea maamuzi hayo ya umojwa wa mataifa, wakiuita wa manufaa sana kwao, kwa kuwa wameulilia kwa muda mrefu sasa.
Shangwe hizo zimeambatana a kumsifu kiongozi wa Mamlaka ya Wapalestina, Mahmoud Abbas, kwa kuongoza vizuri mamlaka hiyo mpaka kutambuliwa kama taifa. Lakini kwa upande wao.
Israel kwa upande wao wamepokea taarifa hizi kwa masikitiko, wakiamini kwamba itarudisha nyuma mpango wa mazungumzo ya amani, ulio na faida kwa wananchi wa pande zote mbili - wale wa mamlaka ya Palestina, na wale wa taifa la Israel. Je, nini kitatokea baada ya hapa? Maana mpoaka hivi sasa inatabiriwa kuwa Palestina inaweza kutumia fursa hii kuishitaki Israel kwa kusababisha visa vya dhulma ya ubinadamu katika ngome yake.
BBC/13wmaz na mashirika mengine ya habari.

Comments