RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NABII FLORA: UJUMBE WA TAREHE 20.12.2012 NI WA KUTUBU NA KUFUNGA NA KUJINYENYEKEZA MBELE ZA MUNGU KWAAJILI YETU SISI, WAOTOTO NA MALI ZETU.

Ninakukaribisha katika kipindi cha Neno la Mungu chenye miujiza na maajabu. Nina kila sababu ya kusema asnte kwa Baba kwaajili yako, na kwaajili yangu pia. Kuna watu wanashindwa kusimama kwa muda mrefu, ni kwa neema ya Mungu tu, kuna wengine wanachoka kuamka alfajiri kufamya huduma, wengi hawaweze ila ni neema tu, sifa na utukufu  apewe Mungu kwani Yeye ndiye anatuwezesha sisi kusimama muda mrefu kufanya huduma yake.

Nina kila sababu ya kusema asante kwa Mungu, kwani toka mwanzo wa wiki nimeona watu wakipona kisukari, wasiotembea wanatembea, nimeona watu wakipata kazi, watu wakipokea baraka za Bwana. Mungu aendelee kutenda juu yako, Mungu aendelee kusema juu yako, Mungu aendelee kukujalia neema.



Umekuja hapa ili kuona baraka za Mungu.

USHUHUDA 0: Katika wiki hii kuna mtoto alipotea na sasa amepatikana kwa yule mama Muha alikuja Jumatatu, siku hiyo ya Jumatatu alimpata mtoto. Alienda kwa mama nitilie wanaochoma maandazi, akakuta mwanae amejigeuza kuwa chokolaa. Alienda mahali pale akamkuta mtoto wake kijana wa miaka 19.

Nina kila sababu ya kukusalimia maana anasema ni njema kila iitwapo leo, mkono wa Bwana ni asubuhi kila iitwapo leo.

SALAMU ZA NABII FLORA KWAKO WEWE.

Tutasoma katika kitabu cha Maombolezo 3:22, kabla ya kusoma,  ninakusalimia mkazi wa Tanzania, mkazi wa dare s Salaam, watu wote wanaonisikiliza kwenye internet au Tv au radio.

Tunasoma katika Biblia zetu, “Ni huruma ya Bwana kwamba hatuangamii kwa kuwa rehema zake hazikomi, ni mpya kila siku asubuhi waminifu wake ni mkuu sana. Bwana ni fungu langukwahiyo nitamtumikia Yeye. Bwana atanitangilia asubuh, Bwana atanilinda mchana, jioni atakupa riziki yako
 Nabii Flora aliyekaa chini akiwa na msomaji wake wa Biblia
Unapaswa hata wewe mwezi huu wa kuelekea Krismasi, nataka uwe mpya ndani ya moyo wako. Fadhili za Bwana ni mpya kila asubuhi. Nataka wewe mkazi wa Dare s Salaam, mkazi wa Tanzania, wewe unayenisikiliza sehemu mbalimbali, Bwana anasema “Fadhili za Bwana ni mpya kila asubuhi tena fadhili za bwana hazikomi”   Nataka fadhili za Bwana zisikome kwako, baraka za Bwana zisipungue kwako, wema wa Mungu usikome kwako, kubarikiwa kusikome kwako, ukabarikiwe, nataka baraka zimiminike juu yako. Kwani Bwana amesema fadhili zake ni mpya kila iitwapo leo.
 
nataka Mungu atende muujiza kwako, nataka bwana akubariki, nataka Mungu akuinue, nataka Mungu akutendee.

USHUHUDA 1: Leo asubuhi nilikuwa naongea na Mheshimiwa Nyanja, akawa ananambia, “nabii Flora nimesikia huduma yako, nakuomba nije, nikamwambia njoo ninakupa appointment ya saa tano na nusu. Akasema nataka na mimi nikae kwenye foleni nitajipanga, nataka kukutana na Yesu kwa anahadithiwa kote mjini, nikamwambia,  Njoo utakutana naye.

Nataka asubuhi ya leo umtumaini Bwana, ukapate kumtumia Mungu asubuhi ya leo, kwa maana Bwana ndiye fungu langu na lako. Hebu muweke Yesu mbele hakuna jambo litakaloshindikana.

USHUHUDA 2: Tumeona jana watu wakishuhudia. Kuna baba alikuja anasema amepona. Alikuwa na tatizo la moyo, kisukari na figo, lakini juzi amepima katika hospitali ya Muhimbili na kuona majibu yote safi. Akaniomba kuwa Krismasi angependa kula na mimi Nabii Flora. Nikamwambia mwanangu njoo hapa kanisani tule Krismasi pamoja.

USHUHUDA 3: Nimemuona Mungu wa ajabu. Kuna binti moyo ulitanuka na ili bidi kwenda hospitalini kutolewa, lakini alipokuja hapa alipona kutokana na maombezi yangu na yako.

Fadhili za Bwana ni mpya kila asubuhi tena hazitakoma juu yako, ukimwamini Yesu fadhili zako hazitakoma. Baraka asubuhi, jioni, mchana zitakuja, mtondo go zitakuja. Utapata baraka za pesa.

USHUHUDA: Kuna mchaga mmoja alikuwa na milioni moja ndani mwake, baada ya kuondoka Jumapili hapa, pesa zimeongezeka laki moja.



Nilisema watu watadondokewa pesa hapa kanisani. Utaenda kufanikiwa biashara yak oleo, utaenda kufunguliwa uliyekuja mahali hapa, maana Bwana anasema, atabariki kazi ya mikono yako. Anasema jioni atakupa riziki yako—utakapo kuja nyumbani kwako jioni na kupiga mahesabu utaona ongezeko la matunda yako ya mchana.

Kabla ya mwaka haujaisha Mungu akufanikishe. Yesu arudishe ya baraka kwako. Mwaka 2013 uingie kwa kishindo, maana anasema mbinguni tutaingia kwa nguvu nyingi. Wenye nguvu ndio wanaouteka ufalme wa Mungu

NABII FLORA: UJUMBE WA TAREHE 20.12.2012 NI WA KUTUBU NA KUFUNGA NA KUJINYENYEKEZA MBELE ZA MUNGU KWAAJILI YETU SISI, WAOTOTO NA MALI ZETU.
Esra 8:21, Ndipo mimi nikaamuru kufunga pale kwenye mto Ahaba, ili kupata kujinyeyekeza mbele za Mungu, na kutafuta njia iliyonyooka kwaajili yetu sisi na watoto wetu na kwaajili ya mali yake. Basi aliomba haya  kumuomba mfalme kikosi cha askari. Tulifunga ili kukata minyoro ya adui. Basi baada ya haya yote Esra alipokuwa akiomba na kuungama, akijiangusha chini kifudifudi, akawakusanya na ndugu zake wote, wanaume kwa wanawake, pamoja na watoto. Kilio chao kilisikika mbele za Mung. Walikusanyika wanaume, wanawake na watoto wote wakiwa wanalia sana, baada ya hapo Bwana alisikia kilio chao. Wale walioamriwa kufunga na kuomba, Bwna anasikia kilio chao caha kuokoa taifa lote. Ndipo aliamuru kufunga pale kwenye mtu Ahaba ili tupate sisi sote kujinyenyekeza mbele za Mungu na kutafuta njia iliyonyooka kwaajili yako mwenyewe. Kwaajili ya watoto wako, na kwaajili ya mali zako na chohote unachokimiliki.

Mkono wa Mungu u juu ya kila mtu anayemtafuta na wale wanaotenda mema kwa maana uweza wake uko juu ya wale wanaotenda maovu.

Basi Ezra alipokuwa akiomba na kulia sana, alijiamgusha kifudifudi mbele ya nyumba ya Yakobokatika kusanyaiko la Israel yote. Wanaume, wanawake pamoja na watoto wadogo walikusanyika na wote wakamlilia sana Bwana.


Watumishi wa Mungu tunaenda kufunga, ila wewe unayeumwa usifunge kwa maana hairuhusiwi. Kabla ya mwaka tunaenda kufunga na kujitakasa. Tunapoenda kula Krismasi lazima tusafishe mioyo yetu. Mtu anapofunga ni kwaajili yake yeye mwenyewe kwanza. Funga maadui ndani ya moyo wako, funga maneno maneno, funga mapepo, funga umbea, funga kila kitu kisipenye ndani yako, wafunge makahaba, yafunge magonjwa, funga machuma ulete katika mwezi ili tuingie kula Krismasi kwa amani na furaha.

Wewe unayeteswa na UKIMWI, amua sasa kuwa unakwenda kwa Bwana Yesu, unakwenda kuonana na nabii Flora
 Amini mama yangu kuwa kilio chako leo kinasikika mbele za Mungu. Kutoka mbinguni Bwana anasikia kilio chako, machungu uliyonayo anasikia, magumu uliyonayo binti anasikia,  una madeni benki na wataka kufilisi nyumba yako ila Bwna anasikia kilio chako.

Dua yako ni nini mwanaume na mwanamke? Bwana atasikia maombi yako, dua yako Bwana ataenda kusikia.

Kumbuka tunapofunga tunatafuta njia iliyonyooka. Nataka asubuhi ya leo kila mmoja atafute njia iliyonyooka kwaajili ya Krismasi ili Yesu azaliwe ndani yako. Lazima wageni walioko ndani yako waondoke, wageni ni usengenyaji, wivu, kumsema mumeo vibaya-kipibndi ana hela ulikuwa unamwita Baba, ila anapoishiwa fedha unaanza kumnena vibaya. Lazima asun=buhi ya leo tuondoe hao wageni waliko ndani mwako.

Tunatakiwa kutafuta njia iliyonyooka na kumwita Bwana ili atende ndani ya maisha yetu na nyumba zetu. Ataenda kutenda na kuonekana kwako asubuhi ya leo.

Siku hizi watu hawatoi machozi kwaajili ya kumlilia Mungu wakati wa maombezi

KUOMBEA WATU
Yesu naomba uwatembelee wanaotenda mema siku ya leo. Huu ni wakati wa Bwana kuwatendea mema. Ninakuita Mungu siku ya leo, shuza wingu
SOMO LINAENDELEA

Comments