RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

"RAIS OBAMA ANATENGENEZA NJIA KWA UTAWALA WA MPINGA KRISTO."


Robert Jeffress, pastor of First Baptist Church of Dallas.
Mchungaji Robert Jeffress wa First Baptist Church Dalla, Texas.        
Moja ya habari iliyoongoza katika mtandao wa Christian Post mwaka huu ni suala la mchungaji Robert Jeffress wa kanisa la First Baptist lililopo Dallas nchini Marekani ambaye katika moja ya mahubiri yake siku moja kabla ya uchaguzi mkuu nchini humo alikaririwa akihubiri kanisani kwake kwamba Rais wa sasa wa nchi hiyo Barack Obama anasafisha njia ya utawala wa mpinga Kristo.
Mchungaji huyo ambaye huwa anatoa kauli zenye utata (kwa watu wengine wasiofuatilia maandiko) alisema hayo akinukuu kitabu cha nabii Daniel kuhusu siku za mwisho na kuwataka waumini wake kutomkariri vibaya kwamba anasema Rais Obama ni mpinga Kristo la hasha ila rais ajaye atapata kura nyingi sana ndiye huyo atakayekuwa mpinga Kristo na kuwataka waumini wa dini ya Kikristo hususani wa nchi hiyo kumuomba sana Mungu kuwaepushia janga hilo kwa kuchukua hatua ya kumpigia kura mtu sahihi.
Ukiacha jambo hilo pia Mchungaji huyo kiongozi aliwahi kukaririwa akisema aliyekuwa mpinzani wa rais Obama bwana Mitt Romney kwamba licha ya kutaja Yesu ni Bwana na Mwokozi si mkristo bali ni Momorn kwakuwa ibada yao si ya Kikristo kwahiyo amesema Romney si Mkristo ni Momorn kwahiyo wasidanganyike na misemo yake.

First Baptist Church Dallas, Texas.  


x

Comments