RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RULEA AMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA KOO NA TUMBO

MUNGU AMENIPONYA MAUMIVU YA KOO NA TUMBO.
Namshukuru Mungu kwa rehema zake na huruma zake kwangu. Nilikuwa naumwa malaria, koo na tumbo. Nilikuwa napata taabu sana wakati wa kumeza chakula na maji. Maumivu yalikuwa makali sana, nilikuwa nahisi kama mtu anapitisha kisu kuanzia kooni hadi mwisho wa mapavu wakati wa kumeza chakula au mate.
 Mungu ni kila kitu katika maisha..ishi katika imani na mtegemee Yesu Kristo wa kati wa shida na raha


Ndugu yangu nilikuwa natamani kulia na mara zingine nilikuwa nalia sana kutokana na maumivu makali. Nilienda dispensary ya Amani iliyoko Sinza Dar es Salaam na niliambiwa na daktari kuwa naumwa malaria. Nilipewa dawa za kumeza ikiwemo Diklopa na Metakaflin, na nilipomaliza ile dozi sikupata uponyaji wowote.

Nikajaribu kuulizia kuhusu maumivu ninayopata ya koo na tumbo,  wakasema hawajui ni nini. Wakanipa dawa za kutuliza maumivu pamoja na vidonge vya vitamini. Niliziangalia zile madawa na kujiambia mwenyewe kuwa sitazitumia kwani yuko Mungu ambaye ni mponyaji

Nilipofika nyumbani nikapiga magoti na kumuomba Mungu aniepushe na haya magonjwa na anirudishie hali yangu ya zamani.

Baada ya muda nikakumbuka kuwa nina Anointing Water niliyopewa na  Nabii TB Joshua, nilichukua yale maji na kuyanywa na mengine nikajipulizia mwilini, huku nikiamini kuwa naenda kupona.   


Nilijawa na mawazo mengi sana kuhusu tumbo, nikahisi labda nina vidonda vya tumbo!!

Nilipoangalia vile vidonge vya maumivu na vitamins nikasema siendi kunywa hata kidonge kimoja ila ninaamini Mungu anaenda kuniponya. Nikazidi kuwa na imani kubwa. Sikupenda watu wengi kujua kuwa ninaumwa ila niliwajulisha watu wachache kama Boniface Magupa, Imma solo, Yuniki Sanga, Scina, Macha, Stella Joel, Master Prophate Machibya, na wengine wachache.

Niliamua kwenda kanisani kwangu EFATHA kwa Nabii na mtume  Josephate Mwingira na nilipofika pale sikutaka kumjulisha Nabii kuwa naumwa, nilimwambia Mungu, “Niko katika nyumba yako nahitaji uponyaji kutoka kwako” Nilimuomba sana Mungu huku nikishika tumbo langu ili Mungu ashushe neema yake kwangu. Baada ya ibada kuisha nilielekea nyumbani huku maumivu yakiwa bado makali sana, niliamini Mungu kuwa yeye anaendelea na operation ya uponyaji.

Nilipofika nyumbani nilimshukuru Mungu kunifikisha nyumbani kwangu, niliamua kwenda kulala, na baada ya kuamuka niliendelea na kazi zangu za kawaida.
Madawa ambayo nilikataa kutumia nikiamini Mungu ndiye mponyaji

Siku ziliendelea kusonga huku nikitaabika sana. Siku ya mkesha niliakwa na Nabii Flora kanisani kwake na nilipofika pale nilisalimiana naye, na sikutaka kumueleza chochote kuhusu afya yangu. Nilichoamini ni kwamba Mungu alishasikia maombi yangu. Wakati Nabii Flora akiendelea na maombezi nilisikia kama kuna vitu vinaachilia ndani ya tumbo langu. Nilimshukuru Mungu.

Mkesha ulipoisha nilifunga safari kuelekea nyumbani. Ilipofika siku ya pili nikimaaniha KRISMASI maumivu yalipungua kabisa. Siku ya kwanza baada ya KRISMASI nilipokea uponyaji wangu na sasa ni mzima wa afya njema na sina maumivu yoyote.

Ninamshukuru Mungu kwa kuniponya kwa kutumia njia zake za ajabu, ninamshukuru Nabii TB Joshua Maji yake ya Upako, Ninamshukuru Nabii na mtume wangu Josephate Mwingira kwa maombezi yake aliyokuwa anaomba katika ibada kwaajili ya wagonjwa.

USHAURI: Ninakuomba usikatae kutumia dawa kama huna uhusiano na Mungu vizuri. Imani yangu ilikuwa imani ya kuji-risk sana. kama umepewa dawa naomba uzitumie na Muombe Mungu akusaidie.

Mimi niliongozwa na Roho Mtaktifu kutotumia dawa ili ushuhuda wangu wa uponyaji ukujenge.

AMININI WATUMISHI WA MUNGU YALE WANAYOTAMKA MTAPONA NA JISIMAMIE KIMAOMBI KATIKA MAPITO YAKO.

Rulea Sanga..
+255 715 851523

Comments