Askofu Mkuu wa KKKT, Dr. Alex Malasusa |
HALI imezidi kuwa tete katika Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati baada
ya Mchungaji Philemon Mollel kufukuzwa kazi na kusimamishwa kutoa Huduma
katika Kanisa hilo Nchini.
Wiki iliyopita bodi ya Dayosisi hiyo
chini ya Uenyekiti wa Israel Ole Karyongi ambaye pia ni katibu mkuu wa
KKKT, ilimtimua kazi Meneja wa Hotel ya Corridor Springs Bw. John
Njoroge kwa Tuhuma za Ubadhilifu wa fedha.
Vyanzo vya Habari vinasema kuwa, Chanzo
cha Mchungaji Philemon Mollel kufukuzwa kazi, ni kushindwa kutekeleza
mambo matatu ambayo Tume maalum ilimtaka Mch. Mollel ayafanye, na
alipewa Siku 3 za kuomba radhi na hakufanya hivyo.
Habari zaidi zinasema kuwa, mambo matatu
ambayo Mch. Mollel alitakiwa kuyafanya ni; 1. Kumuandikia Barua Askofu
wa Jimbo la Kaskazini Kati Dr. Thomas Lazer kueleza ni kwanini
alimkashfu na kumdharau. 2. Kutoa tamko katika Mtaa wa Azimio Ibadani
Desemba 23, kuomba radhi kwa yale aliyotamka.
3. Amwarifu Katibu Mkuu kwa Barua baada ya kuyatekeleza hayo na awe amefanya hivyo kabla ya Desemba 24 Mwaka huu.
Habari zinaeleza kuwa, walioteuliwa
Desemba 14 Mwaka huu na kwenda kumuona Mch. Mollel ili kutekeleza hayo
ni Pamoja na Msaidizi wa Askofu, Mch. Solomon Massangwa, Katibu Mkuu wa
Jimbo la Arusha Magharibi Mch. Godwini Lekashu na Katibu Mkuu Israel Ole
Karyongi.
Hata hivyo Mch. Mollel alipopigiwa simu,
alikiri kupokea nakala ya barua hiyo ya kufukuzwa kazi na kuvuliwa
Uchungaji lakini alisema hakuwa kwenye nafasi nzuri ya kulizungumzia
hilo. Mch. Mollel aliongeza kwa kusema kuwa Uamuzi huo umechukuliwa kwa
Chuki na Fitina, na haukuangalia madhara ya Deni la Sh. Billioni 11
endapo Kanisa litashindwa kulipa fedha hiyo.
Comments