RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BUNDUKI ZARUHUSIWA MAKANISANI


Katika hali isiyokuwa ya kawaida kwenye nyumba za ibada, Kanisa nchini Marekani jimbo la Arkansas, limeruhusu ubebaji wa silaha ibadani.


©Goodrock

Hatua hiyo imekuja baada ya muswada kupekekwa kwenye mamlaka za kutunga sheria jimboni hapo, na kwa kupitishwa kwake, inamaanisha kanisa limepewa uhuru wa kuchagua na kuamua nani anaweza kuingia na silaha yake ibadani.

Seneta wa jimbo la Arkansas, Bryan King, amesema kuwa kanisa litakuwa huru kufanya wapendavyo kuhusiana na hali ya usalama, kwa njia wanayoona kuwa ni sahihi.

kwa upande wake Seneta kutoka Democrats, bi Linda Chesterfield, amesema kuwa alikuwa anatafakari namna gani ya kutomuhusisha Yesu Kristo na fujo ama mashambulizi.

"Kama kuna mtu ambaye hakuwa mgomvi, basi ni Bwana na Mwokozi wangu, Yesu Kristo" alisema Chestefield ambaye anapingana na uamuzi huo.
Marekani iko katika hali tete kufuatia mashambulizi ya mara kwa mara yanahohusisha silaha za moto, jambo ambalo linawapa wananchi hofu ya kushabuliwa muda wowote. Na tukio hili limekuja wakati kuna shambulizi lingine ambalo limeripotiwa kutoka Phoenix, Arizona, ambapo mtu mmoja ameripotiwa kufanya shambulizi kwa silaha ya moto kwenye ofisi mmojawapo, ambapo watu kadhaa wamejeruhiwa. Na huku siku chache zilizopita, jambazi mmoja akishindwa kupora mali na fedha baada ya kuitiwa jina laYesu.

Inatoka: Gospel Kitaa

Comments