RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHAKACHAKA ASEMA HATORUHUSU MUMEWE KUOA MKE WA PILI



Mwanamama Yvonne Chakachaka.

Gwiji la muziki barani Afrika mwanamama Yvonne Chakachaka kutoka nchini Afrika ya kusini ameweka wazi kwamba ni heri aachane na mumewe kuliko kuona mumewe huyo akioa mke wa pili. Chakachaka ameyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na vyombo vya habari makao makuu ya umoja wa mataifa(UN) nchini Marekani.

Chakachaka ambaye alitangaza kuokoka miaka mitatu iliyopita amesema anatambua fika kwamba mumewe bwana Mandlalele Mhinga ni mtoto wa familia ya kifalme kabila la Shangaan nchini kwao hivyo kuruhusiwa kuoa wake watatu hadi wanne lakini hatoruhusu hilo na hata mumewe anajua hilo ndio maana akaamua kumuoa yeye. Chakachaka aliachia album yake ya 22 mpya mwishoni mwa mwaka jana ikifahamika kwa jina la ''Amazing Man'' ndani yake kukiwa na wimbo maalumu kwa mama yake ambaye anaishi maisha ya ukiwa baada ya baba yake Chakachaka kufariki dunia.


Chakachaka alipotembelea nchini miaka ya karibuni akiwa sambamba na Upendo Kilahiro

a
Chakachaka na mumewe katika pozi.

"Thanx Gospel Kitaa for ur news"...says Rumafrica

Comments