RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

GOSPEL LIVE SHOW KUANZA KUUNGURUMA KATIKA HOTEL YA FIVE STAR SERENA NA JESSICA HONORE

Jessica Honore anategemea kuanza kufanya GOSPEL LIVE SHOW kwaajili ya kumtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji, na hii itakuwa inafanyika kila wiki katika hoteli ya Five Star Serena iliyoko Posta jijini Dar es Salaam. Endelea kufuatilia blog hii kwa kujua mengi kuhusu ujio huu mpya na wa viwango vya Kimataifa ambao mwana dada huyu anataka kuonyesha Watanzania wanaopenda kazi ya Mungu.


Jessica Honore

Tumekuwa tukiona watu wa mataifa wakifanya Show zao katika majumba na mahoteli ya kifahari, lakini sasa huyu dada anataka kuonyesha ya kuwa watu wa Mungu wanayaweza yote katika yeye atutiaye nguvu.

Ukimwangali huyu dada kimwili huweza dhania na kile ambacho Mungu amempa kwa njia ya uimbaji. akiwa anasoma sekondari aliweza kuzawadia gari kutokana na sauti yake kuwa ni ya kipekee kwa uimbaji.


Jessica Mwana wa Honore

Jessica Honore amewahi kuimba na band maarufu sana hapa jijini Dar es Salaam inayofanya kazi moja tu ya kumwimbia Mungu, inayoitwa Glorious Celebration.

Jeesica Honore mbali na kubarikiwa huko pia mwaka huu anaolewa na mtangazaji wa Television ya Channel Ten, Boniface Magupa. Mungu amuwezeshe mwimbaji huyu. Unaweza kumuwezesha kwa lolote na yeye yuko tayari kwa mawazo yako, mchango wako wowote ule.

Mbali na hayo yote pia RUMAFRICA iko katika zoezi la kutngeneza blog yake inayoenda kwa jina hili. www.thejessicamusic.blogspot.com


Hi pipo..I love you all..!!!

Jessica Honore

Comments