RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HESHIMU KAZI YAKO UTAONA MAFANIKIO


Mungu anapokupa kiupenyo fulani cha kupatia riziki, yakupasa uheshimu na umshukuru Mungu kwa huo mpenyo aliokupa. Kuna wengine wanatamani sana kazi unayofanya lakini wanashindwa kufanya. Na hii ni kwa neema ya Mungu. Kuna wengine wanafanya kazi ya kufagia choo na Mungu anawabariki wanafanikiwa katika mipango yao. Kuna wengine wanatamani kufanya kazi ya kufagia choo lakini wanashindwa kutokana na aibu zao. Ninachosema ni kwamba, ni kwa neema ya Mungu kupata kazi. Binafsi ninamshukuru sana Mungu kwa kunipa elimu hii ambayo imekuwa msaada kwa walio wengi. Unaweza usitambue msaada huu lakini unafanya kazi katika maisa yako ya kila siku. Utajiuliza ni msaada gani?  Muombe Mungu akupe mwanga wa kujua....

Naomba nikupige picha..Asante KJunior kwa kunipiga picha.
Rafiki yangu iombee kazi yako kwani inapigwa vita a walio wengi. Kuna wengine hawatamani kukuona wewe unafanikiwa. Muweke Yesu mbele katika kazi yako. Kuwa mwaminifu na fanya kazi yako kwa bidii zako zote.

Ipende kazi yako hata kama inakuingizia kiasi kidogo, ifurahie kazi yako, jiamini kuwa wewe nio bora kuliko wengine, rizika na kile unachobarikiwa ila chukia kuona mapungufu katika maendeleo yako, tafuta njia bora za kutatua matatizo yako, unapoamuka tambua ni nini unaenda kufanya kwa siku yako, yachuje mawazo ya watu yanayokujia kwa lengo la kutaka kukushauri, usikubali kila wazo, angalia marafiki walio wema katika kuwashirikisha mambo yako, kuwa na maneno machache vitendo vingi, jiheshimu na ujishushe.

Mimi nikutakie mafanikio mema katika jina la Yesu Kristo.

Wako katika Bwana
Rulea Sanga

Comments