RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

JAMBAZI LAKIMBIZWA NA JINA LA YESU, LASHINDWA KUPORA


Ni katika nyumba ya mwanamama Jacquie Hagler, Lake City, Florida, akiwa na wakinamama wenzake takriban kumi na tatu. Wakati wakiwa katikati ya kilichowakusany nyumbani hapo (hafla ndogo). Ghafla akaingia jambazi mwenye silaha ya moto huku akiwa amejifunika uso ili kutotambulika.
Jacqui Hagler akiwa nyumbani kwake. ©First Coast News
Wakinamama hao wakiwa nyumbani kwa Bi Hagler, walikua wakijiandaa kucheza mchezo mmojawapo kati ya mingi waliyopanga. Na walikuwa wameketi kila mmoja akiwa amepakata pochi yake, ndipo ghafla mvamizi akajitosa ndani ya nyumba na kumuwekea bastola mmojawapo wa wakinamama waliokuwepo, akiamrisha pochi, na vito vyao vya thamani kukusanywa.
Pamoja na kwamba hiyo ni bastola ya ukweli, bado wakinamama hao hawakujua kinachoendelea, huku baadhi yao wakidhani kuwa ni sehemu ya mchezo, kama ambavyo imeandaliwa na mwenyeji wao.
"Mi nilijua kuwa ni shemu ya mchezo, hivyo sikuwa na wasiwasi, lakini nilipomtazama mwenyeji wangu, ndipo nikagundua kuwa uso wake umejawa na wasiwasi, basi nikaju kuwa hali ni tete" anasema mwanamke mmojawapo.
Lakini ghafla, wakati kila mtu akwa ameduwa na asijue la kufanya, Bi Hagler alijawa na ujasiri na kumuamuru mvamizi huyo kuondoka kwa jina la Yesu. Jambo ambalo lilimfanya mvamizi huyo kwa muda huo kuchukia na kurejea kauli ya kuwataka kinamama hao kutoa kila walichonacho.
Baada ya kuduwaa kwa ukimya kidogo hivi, ndipo wakinamama wote wakaungana na mwenyeji wao kumkemea Jambazi huyo kwa jina la Yesu, wakimuamuru atoke ndani ya nyumba.
Nguvu ya jina la Yesu ilipomzidia jambazi huyo, akaamua kutimka akiliacha jeshi la kinamama 14 wakiendelea kumkemea kwa jina lipitalo majina yote, jina la Yesu.
Kama mwanamke wa imani, ninajua jina la Yesu lina nguvu kubwa, na huwa ninalitumia kwenye matatizo, lakini sijawahi kuitumia kama siku ya leo, leo ni ajabu sana. Lakini sishangai sana kwa kuwa ninajua kuwa Biblia imetuambia tuliitie jina lake wakati wa shida. Amesema bi Hagler wakati wa mahojiano na vyombo vya habari.
Kwa upande wake afisa habari wa Lake City, ambaye pia ni mpakwa mafuta mtumishi wa Mungu, Craig Strickland amesema kuwa, kitendo alichofanya bi Hagler, ni mfano tosha wa nguvu ya jina la Yesu, lakini sio cha kuigwa na kila mtu.
Hata hivyo jambazi huyo alikamtwa lisaa limoja baadae alipoamua kwenda kufanya jaribio la kumuibia mtu aliyekuwa amekwenda kuchukua pesa kwenye mashine ya ATM. Na hii pia ilitokana na utambuzi wa wanawake hao, ambao katika kurupushani za kumkemea, jambazi huyo alihangaika kiasi cha nguo aliyofichia uso wake kudondoka.
Pamoja na hayo, bi Hagler anamshukuru Mungu, kwa kuwa siku hiyo mambo yangekuwa tofauti, ni mengine yangekuwa yanazungumzwa leo hii, kama sio muujiza kutokea, hasahasa ikizingatiwa kuwa binti yake mwenye umri wa miaka 14 alikuwa miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo.

Comments