RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KILA JAMBO LINA MWISHO WAKE..WAKATI WA LULU KUKAA LUMANDE UMEFIKA MWISHO


Jamani tukumbuke kuwa kila jambo chini ya jua lina mwisho wake. Unaweza ukawa una kula raha za dunia na kumsahau Mungu na ukajisahau kuwa ipo siku utatoweka hapa duniani. Unaweza ukawaumiza wenzako ukijisahau hayo unayofanya yatakujia na wewe.

Kumbukeni kumtumikia Mungu maisha yenu yote. Leo hii Lulu baada ya kuteseka na maisha ya gerezani, umefika wakati wa kuliacha gereza na kuungana na wenzake uraiani. Lulu analia kutoka na yale yaliyomsibu maishani mwake. Hakutegemea kuwa ipo siku atakutwa na haya yaliyomkuta.
Ndugu yangu unajifunza nini kutoka kwa Lulu kuhusu Mungu? Tuache kwa na kiburi na kujiona sisi tunayaweza yote...Mali zako zisikupe kiburi cha kutomtumikia Mungu. Na wewe unayemtumikia Mungu, fanya kazi ya Mungu kwa moyo wako wote na kwa kumaanisha, usifanye kazi ya Mungu ili uonekane na watu kuwa wewe ndio kijeba.

Mtumikieni Mungu naye atawatumikia...Ni mimi Rulea Sanga

 
Machozi ya furaha. Picha zote zimepigwa na habarimpya.com

Lulu na mama yake mzazi wakilia baada ya kukutana nje ya Mahakama, Lulu amechiwa huru na Mahakama leo january 29 2013 mchana, pembeni ni mwigizaji Dr. Cheni ambae amekua karibu na familia ya Lulu kwa muda mrefu sana.


Lulu akiingia kwenye gari.

Comments