RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWALIMU MWAKASEGE KUANZA ARUSHA JUMAPILI HII, DAR WAKIJIANDAA


Mwalimu Christopher Mwakasege.


Wakazi wa jiji la Arusha na viunga vyake wanatarajia kuwa na wakati mzuri kuanzia jumapili hii wakati ambao Mwalimu Christopher na Diana Mwakasege watakapoanza semina ya neno la Mungu kupitia huduma yake ya Mana katika viwanja vya Reli vilivyopo mjini humo kuanzia majira ya saa tisa alasiri hadi saa 12 jioni huku semina hiyo ikirushwa moja kwa moja na kituo cha radio Safina cha jijini humo pia matangazo ya moja kwa moja kupitia tovuti ya Mwalimu Mwakasege pamoja na kicheko.Semina hiyo inafanyika wakati ambao pia wakazi wa jiji la Dar es salaam walipata wasaa wa kufundishwa na Mwalimu Mwakasege kwa semina ya siku moja ya kupanda iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jumapili iliyopita na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jiji hilo hata kufanya ukumbi huo kusiwepo nafasi. Ambapo wanatarajia kupata semina ya wiki nzima katika viwanja vya Jangwani kuanzia tarehe 24 February hadi tarehe 3 mwezi Machi mwaka huu

Comments