RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NABII FLORA ATABIRI YAKUWA “WIKI HII NI YA MUNGU KUJITOKEZA NA KUPUKUTISHA MAADUI ZAKO” IBADA IMEAFANYIKA 29.01.2013 ASUBUHI


Bwana Yesu asifiwe..nawasalimu kwa jina lishindalo majina yote la Yesu Kristo….Ameni

Ninakukaribisha wewe uliyefika mahali hapa kwa jina la Yesu na Mungu atimize haja ya Moyo wako.

Ni kila sababu ya kusema asante kwa BWANA kwa kunipa siku nyingine hii. Ninasema siku ya leo Mungu ataenda kukutokea wewe, kama inavyosema Ufunuo 3:20 kwamba “Tazama BWANA amesimama mlangoni anabisha hodi".
Yupo Kristo asubuhi ya leo amesimama mlangoni akibisha hodi, amesimama juu ya moyo wako anabisha hodi. Asubhi ya leo anasema Bwana, ukifungua mlango wako tu, Bwana ataingia na kufanya makao ndani mwako, Bwana ataingia katika nyumba zenu mama na uaskini unaenda kuondoka, mikosi inaenda kutoka maana Bwana anasema tazama mimi nasimama mlangoni nabisha hodi na mtu akisikia sauti Yangu na kufungua mlango mimi nitaingia na kukaa ndani mwake..Haleluya…
Bwana anasema ukimruhusu kuingia ndani mwako atakula pamoja na wewe, atabadilisha maisha yako, atabadilisha ndoa yako, atabadilisha uchumi wako, atabadilisha kiroho chako, atabadilisha watoto wako,
Hakika Bwana akiingia ugonjwa unatoka, kansa inatoka, UKIMWI unatoka,  umaskini utatoweka mama, kukoswakoswa kutatoweka,  kukosa ajira kutatoweka, hebu fungua mlango sasa.
Maana ya mlango ni fahamu zako. Yesu ni wa thamani, amezidi kukupa uzima, afya, amekupa uponyaji, hebu fungua mlango wako asubuhi ya leo.
Nabii Flora Peter akiwa madhabahuni.

Bwana anaenda kugeuza majego ya adui zako, atawapindua maadui zako kama yalikuwa yanatazama mbele yatatazama nyuma, yaani kama ulikuwa hupati watoto sasa unaenda kupata. Ninachotaka kusema ni kwamba hapa maadui watapigwa kwa jina la Yesu Kristo.
Hata kama maadui zako wameandaa adui kama samba au nyati, Mungu atawageuza hao maadui, na kama waliandaa mipango yako kuyumba ninasema mipango yako itanyooka na kuwa na mafanikio makubwa, hata kama walikusudia mwaka huu wakuondoe hapa duniani watashangaa unamaliza mwaka na kuona mwaka mwingine kama ulivyouona mwaka huu 2013, mwambie jirani yako sifi tena, Bwana amekusudia jambo kwangu mwaka huu kwani yeye ndiye aliyenitunza, aliyenipa ajira.
Ninaona mema na Baraka, ninasema..pokeaaaaa Baraka zako kwa jina la Yesu,
 Nabii Flora akihubiri Neno la Mungu

UJUMBE WA LEO WA MUNGU KUTOKA KWA 
NABII FLORA
Yoeli  2:13-14 Rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu, kwa maana yeye ndiye mwenye rehema, amejaa huruma,  si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughahiri mabaya. N’nani ajuaye kwamba hata rudi, na kugeuka na kutuachia Baraka nyuma yake, naam sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji kwa Bwana, Mungu wenu?.  Yoeli 2:18 Hapo ndipo Bwana alipoona wivu kwaajili ya nchi yake, akawahurumia watu wake.

Bwana anasema inua mioyo yenu na maana ya kuinua miyo yenu ni kujiachilia kwa BWANA, unakubali moyo wako kuvunjwa vunjwa, unakubali moyo wako kupondeka. Sio kuangalia haya mavazi uliyovaa, na mimi siko mahali hapa kumwambia mtu umevaa vibaya ila nipo kwaajili ya kumtangaza Yesu, nipo kwaajili ya kusema watu waokolewe, wewe njoo kama ulivyo kwani damu ya Yesu itakutakasa, noo kama ulivyo Yesu atakubadilisha, na usije kwa kujiona unaumbo zuri, una nywele nzuri, ninachofanya ni kuzungumzia Kristo ainuliwe juu, watu waokolewe.
Tusipoteze wasomi kwaajili ya kansa, tusipoteze wasomi kwaajili ya kansa, tusipoteze watu kwa magonjwa. Nipo hapa kwaajili ya kumwita Yesu aliponye taifa langu.

ninakumbia usijaribu kumkosa mtu kwani Mungu atankarabati, unachotakiwa kufanya ni kuomba na kumuombea mtu huyo anayefanya makosa. Unaona mtu kava suruali unaanza kumsema, kwahiyo ulitaka mtu huyo asisali, ninakuomba umuache na suruali yake amuombe Mungu wake.
Mungu wetu amejaa neema na si mwepesi wa hasira, Bwana wetu hana ubaguzi anahitaji kuwabadilisha watu wote. Mungu wetu anawatazama matajiri, anawatazama maskini, anatazama watu wanaojiweza na wasiojiweza ili apate kuwainua..Haleluya!!... Mungu hahesabu makosa ya watu wanaomkosea.
Bwana anasema amewahurumia watu wake na kanisa lake. Mwaka huu Bwana anenda kutuletea nafaka yaani tutakula tutashiba. Ataruhusu wingi wa Baraka, Ataruhusu wingi wa mazao, Ataruhusu wingi wa utajiri, Ataruhusu wingi wa pesa. Mungu anasema nanyi mtashiba mwaka huu, na Bwana ameahidi wiki hii kuleta Baraka kwako, kuleta vyakula, kuleta watoto, kuleta maji, kuleta soda. Na mimi Nabii Flora ninasema pokea motto wako sasa.
 Nabii Flora akiwa madhabahuni kwa kazi ya Mungu

KIPINDI CHA MAOMBEZI MAOMBEZI
Ninasema magonjwa, UKIMWI, Kansa, TB, kuonewa teketea kwa jina la Yesu. Ninasema leo ninakukurupusha umezoea kutesa watoto wa Mungu, ninasema siku ya leo toooooka….moto ukulambe…moto wa Yesu ukuunguze… Ninatangaza jina liletalo uzima..pokea jina hilo wewe unayehitaji likuokoe siku ya leo. Ninasema wewe mama ulikaa hapo tikisa kichwa chako, Bwana anakuja kukutembelea na kuondoa shida zako, ninasema tikisa na endelea kutikisa kichwa chako, kwwa kutikisa kichwa chako unenda kupona ugonjwa wako na taabu zako zinatoweka amini hivyo watu wa Mungu. Ninafichua mizimu inayokutesa siku ya leo. Mizimu mnayesikia sauti hii nasema tokeani mlikojificha na muacheni huyu mama awe huru .


Bwana anasema leo hatawafanya nyinyi kuwa watu wa aibu tena, hata wakiwafanya ninyi kuwa kama  watu wa mataifa, kwani watasema Yule mama hana kitu chochote. Lakini nataka kuwaambia kuwa Yesu hatawafanya kuwa watu wa shida, Yesu anaenda kuwabariki. Walio wadharau wataona BWANA akiwahudumia, waliowabeza wataona unaendesha magari mazuri, waliowabeza wataona unaishi katika nyumba nzuri, waliowabeza wataona mna makampuni, waliowabeza wataona masoma shule za International na nzuri kielimu. Mungu analeta Baraka, ninyi mtakula na kushiba, lazima Mungu ainue uchumi wako sasa.
 Watu wa Mungu wakimsikiliza Mungu.

Ninasema tumechoka sasa kuchekwa na kudharauliwa na kutokufanikiwa. Ninasema Yesu lazima aguse mtu, kwa maana watu wamekaa muda mrefu wakitarajia kufanikiwa. Na mimi kama Nabii Flora ninasema mwezi huu na wiki hii mpaka kufikia Ijumaa  Yesu anaenda kutubariki na anenda kujifunua.
Jeshi la adui zenu wanaowaloga, wanaoingilia mipaka yenu  Mungu anenda kuwafukuza. Na mimi nataka kuona watu wanaotaka Mungu afukuze adui zao wakimtumikia Mungu wa kweli. Ninasema maadui wanafukuzwa leo katika jina la Yesu. Ninasema inuka sasa njoo kwa Yesu ndugu yangu.
Pokea Baraka zako kwa jina la Yesu Kristo. Nataka watu wafurike wamrudie Mungu wao, na Mungu ataenda kupambana na wale walikokuwa wanaiua ndoa yako, biashara yako, mipango yao. Na mimi Nabii Flora nakataa kwa jina la Yesu..
Mungu akishughulika na watu walioamua maisha yao kuwa kwake
Watu wakishuhudia kwa macho yao matendo makuu ya Mingu yanayotokea katika Kanisa la Yesu Kristo la Maombezi
Kwa Yesu kuna raha..kama unavyoona watu wa Mungu wakipokea baraka za Mungu na kutabiliwa na Nabii Flora
Nabii Flora akifafanua somo linalosomwa na msomaji katika kitabu kitakatifu
 Nabii Flora akiwatabiria watu
 Watu wakipokea baraka za Mungu kwa kupitia Nabii Flora

...dada akitafakari ..
 UKITAKA KUJUA MENGI KUHUSU HUDUMA YA NABII FLORA PETER TEMBELEA
www.nabiiflora.blogspot.com

Mwandishi
Rulea Sanga
Rumafrica
creative Director and Graphic Designer
Mob: +255 715851523
Email: rumatz2012@gmail.com
Blog: www.rumaafrica.blogspot.com
MUNGU AWABARIKI.
SOMO LINAENDELEA...

Comments