RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI ANAYEPENDA MICHEZO: ORIDA NJOLE

Kuna waimbaji lakini sio kama dada Orida Njole, ambaye ametokea kuipenda michezo kama anavyopenda kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Tunaambiwa na walimu wetu wa muziki kuwa ukitaka kuwa na sauti nzuri yenye kuwavuta watu kwa Yesu wasikiapo nyimbo zako, la msingi ni kuzingatia mazoezi ya kukimbia na pia michezo mbalimbali. Orida aliliona hilo na likamfanya kuwa makini sana katika michezo.

Michezo imemsaidia sana Orida Njole kukutana na watu mbalimbali na kujenga urafiki na wengine wamemsaidia katika huduma yake kwa kupata mawazo kutoka kwao. Michezo ina faida nyingi katika miili yetu kwani inasaidia kuepukana na magonjwa mbalimbali.

Orida Njole ni mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania, kwa sasa ametoa albamu yake inayoitwa  "Duniani Tuwapitaji" yenye nyimbo tano. Albamu hii inapatikana sokoni na pia unaweza kuwasiliana naye kwa simu +255 718939396 na pia unaweza kumpata katika facebook yake Orida Njole.

Mungu amemuwezesha na sasa yuko katika maandalizi ya VIDEO.

Kama unamhitaji katika tamasha au huduma yoyote ya Mungu, unaweza kuwasiliana naye. Na yuko kihuduma zaidi na sio kibiashara kama watu wa dunia wanafyofanya...

Unaweza kujiuliza huyu dada anatokea mkoa gani..? Nakuachia mwenyewe hilo swali...

 Kutoka kulia ni Sada Salim, Joyce Richard, Victoria Godfrey, Amina Wavu, Insia Mafue, Maua Magome, Orid


 Orida wa kwanza kutoka kushoto

Ukaguzi wa kucha ukiendelea...
 Orida (kulia) akijaribu kumpa pasi rafiki yake
 Orida wa pili kutoka kushoto akifuata mpira.
 Kazi ikieendelea kusaka ubingwa

AUDIO CD COVER
 Upande wa Mbele

Upande wa nyuma
 
Nyimbo

Kazi ya kutengeneza CD Cover imefanywa na RUMAFRICA Tanzania
Wasiliana nasi kwa simu +255 715 851523
au rumatz2012@gmail.com





Comments