RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NABII FLORA AKIHUBIRI KATIKA IBADA YA JUMAPILI 03.03.2013

KIPINDI CHA SALAMU KUTOKA KWA NABII FLORA
Nawasalimu kwa jina la Yesu Kristo aliye hai…Nawasalimu wazee wa kanisa na watu waliofika leo. Ninawakaribisha siku ya leo ya tarehe 3.3.2013, huu ni mwaka wa mapambazuko, mwaka wa BWANA kutenda.

Ndugu wapendwa leo Katibu wetu hakufika mahali hapa, amesafiri kidogo, ameenda Monduli kuna emergency imetokea.

Ninaomba uinue mikono yako juu. Usiku huu wakati naongea na Mungu kuhusu ibada, niliona mafuta yakiwa yamepanda juu angani, Bwana akanambia fuata yale mafuta. Nilipoyachukua yale mafuta niliona upako ukitembea kwa watu, sikuona mtu aliyesimama, sikuona mtu aliyekaa kwenye kiti, niliona watu wakinitokea, niliona wagonjwa wakipata Baraka, niliona kama Jumatano watu wamendokewa pesa ambazo sijwahi kuona, niliona watu wakipokea Baraka.



Nabii Flora akiomba kabla ya kukanyaga madhabahu.

Mungu akanambia , wambie watu wangu, hakuna atakayekuja hapa akakosa kufanikiwa, hakuna atakayefika mahali hapa akakosa kuingia mbinguni. Ninataka nikwambie asubuhi ya leo, uko utukufu wa Mungu umetanda hapa, wako watu 470 wameandaliwa na wakiangalia akaunti zao, uta-check simu yako.

Bwana nilitee watu wako ambao umewaandaa asubuhi ya leo. Ninaona utukufu wako Baba umetandaa, maana ninahitaji watu 470. Natazama ninaona kuna watu wamefungua mioyo yao. Baba ninaomba uniletee watu hao sasa katika asubuhi ya leo, maana wanakwenda kufanikiwa, wanakwenda kufunguliwa. Bwana nahitaji watu hao sasa, nataka sasa utukufu kutembea kwa kila mmoja..nasema Tembeeeeeeeaaaaaaaaa!!!!b kwa jina la Yesu.
Nabii Flora Peter

Leta watu hao sasa, watu wanachomoka pande zote, watu 470 baada ya sauti hii angalia simu yako, angali Tigo Pesa yako, angalia akaunti yako…Ninapotazama ninaona kuna watu wamekusudiwa siku ya leo, kutendewa na Bwana asubuhi ya leo. Sikia Mtanzania, mwanamke, mwana wa Mungu, mwanaume, ninakutamkia Baraka. Ninaona watu wanakuja kama mvua, wewe ni BABA tembelea watu wako, tembelea mkutano kwa jina la Yesu Kristo.

Ninasema utukufu..utukufu..utukufu..Ninakamata pande zote za giza, ninasitiisha juu yangu, ninasema hazina nafasi. Yesu watembelee watu wako sasa, naachilia neema, ninaachilia utukufu siku ya leo,

Ninaona watu wanapokea Baraka, ninaona watu wanavutwa mbele . Yesu tembelea watu hawa (Nabii alianza kunena kwa lugha). Ninaona kuna watu wanavikwa Baraka. Ninasema ninaupanga wenye moto, ninaenda kukata, ninakata matatizo yako. Ninaupanga wenye moto, ninazo silaha za maangamizi, ninaenda kuangamiza kazi za shetani, ninazo silaha za kukutwanga ibilisi. Ninakupinga ibilisi, achia watu wafanikiwe. Umekamata maisha yao, umekamata kipato chao, watu wamepoteza misingi, watu wamepoteza riziki, biashara, watoto.

NInakuambia wewe shetani unapigwa kwa damu ya Yesu. Ninayo mamlaka ya kukuangamiza wewe shetani.uuuuuuunguuuuaaaaa!!! kwa jina la Yesu. Natamka neema kwa damu ya Yesu Kristo. Tembelea watu wako BABA, tembelea kanisa lako leo.

Ninakuomba utazame mbele mtu wa Mungu, na inua mikono yako juu isjhara ya kupokea kitu. Utaona mikono hiyo inadondokewa kitu. Kuna watu wanaenda kudondokewa Baraka. Bwana amesema watu wakiinua mikono yao, kuna kitu Bwana atafanya asubuhi ya leo. Ninaona Malaika wamekwisha kutua, wameshuka na wingu jeupe, wametanda mahali hapa.
Wewe ambaye unahitaji Bwana akuguse, usiondoke na mateso yako, lazima tutoke kwa kishindo. Iko miezi 18 utukufu umetanda hapa, watu wanajiokotea Baraka. Lazima Bwana atende siku ya leo.
Nabii Flora na Mchungaji Ansila

Ninazungumza na watu wanasikiliza radioni, wanaosoma katika facebook, ninakwenda kutamka Baraka. Kuna vijana wamesoma katika Facebook wamepata ajira na wengine wamepata VISA. Ninahitaji Bwana wangu akutembelee, inua mikono yako vizuri kama unapokea kitu na uinue juu sana.na sura yako tazama juu mbinguni.

Ninaamuru hiyo mikono iweze kutikisika. Ninaamuru upepo utoke pande zote nne na uingie upepo wa Baraka. Malaika wa utajiri, Baraka, ninakuamuru sasa utembee, uingie katika kanisa hili. Watebelee watu wako wameinua mikono ya kupokea. Wachungaji, wazee wa kanisani wamenyoosha mikono na wako tayari kupokea. Ninasema na kanisa lote, mikono tikisika na pokea. Sipendi kukuona umesimama kama mti, nataka mikono yako uliyoinua ikitikisika,.
Ninaona vifungo vinakatika, ninaona vilivyoshikilia mafanikio yako iko kamba inakatika, ninaona mbingu zinaanguka sasa, Yule adui yako anaaaaaanguuuushwaaaa!! Ameanguka sasa, ngome, wachawi, majini, mambo ya mizimu, mipango ya shetani, mapepo, vinavyozuia ajira, vinavyozuia watoto, vinavyozuia  upako vimeanguka. Pokea Baba, mama Baraka zako kutoka kwa Mungu. Ninaona Baraka zinadondoshwa, ninaona Baraka unapokea sasa.
Pokea mtaji, pokea msingi, pokea kazi, pokea safari za kwenda Ulaya, kwa damu ya Yesu Kristo. Ninakuita Baba,mitume na Manabii, Yesu Kristo anashuka, ninaona nguvu za ajabu, pokea mwanangu Baraka. Ninaona neema kwa Pastor Jury-pokea Baraka. Mahitaji yako yote peleka kwa Mungu sasa.
Ninaona kitabu chako kimegfunguka, mambo yako yamefunguka sasa, pokea kufanikiwa, pokea Baraka, pokea uponyaji kwako wewe mwenye UKIMWI, watoto na nduh=gu zako walikufa kwa kutatanisha ninaona wanarudi, kwa damu ya Yesu Kristo.

Ninaachilia neema sasa, ninasema pokea. Wewe ni Baba, wewe ni Mungu, wewe ni Jehova, umetuka Baba. Ninaona upako unatembea, Yesu umeshuka uwanjani.

Bwana anasema mikono yote tikisika, kwa wale wanaotaka kupata pesa, wale wanaotaka kupata ajira. Ninasema kanisa zima mikono cheza kwa jina la Yesu


Nabii Flora Peter

UJUMBE WA JUMAPILI KUTOKA KWA NABII FLORA
Tutasoma Mathayo 14:22-36.
USIZUIE UPANGA WA BWANA KUFANYA KAZI YAKE UTALAANIWA.

Maana ya Mlisho ni mbele, Biblia inasema kulikuwa na upepo ukitokea mbele. Yamkini na wewe umetenda matendo Mkuu ya Mungu na watu wakaona ni kivuli, iala nataka kuwaambia hapa kwetu ni LIVE na sio chengachenga wala kivuli. Hapa inatembea injili LIVE na sio kama mhele wenye michanga.

Wanafunziwa Yesu walidhani ni kivuli walipomuona Yesu akitembea juu ya maji, yamkini na wewe katika maisha yako wameona kama kivuli kinachotembea na kutenda miujiza, ninakumabia hapa ni Yesu Kristo Mnazareth anayetembea hapa. Yamkini wewe ulidhani ni kivuli kinachotembea hapa kanisani, nakuambia hiki ni kitu halisi. Ninakuambia hapa anatembea mwanaume wa wanaume Yesu Kristo.


Wanafunzi wa Yesu wakaogopa  wakapiga yowe kwa hofu maana waliona na kujiuliza,  hiki kivuli kinachotembea kimetoka wapi? Umekuwa ukiona watu kupandishwa cheo, wakipona UKIMWI, na umekuwa ukiona kama ni kivuli na sio Yesu anafanya na umekuwa na hofu, leo nakuondoa hofu, ninakutamkia kumuona Yesu halisi, utaenda kuona Yesu akisimamupande wako na kumuona Yesu halisi,

Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa jipeni moyo wala mimi msiniogope. Yamkini umekuja hapa na umemuona Yesu LIVE lakini unakadhani ni kivuli. Ninasema hiyo hali lazima niichinje na kuinangamiza kwa damu ya Yesu Kristo.

Petro alipoona hayo hakuamini kuwa ni Yesu. Hata waumini wa sasa wanamashaka wanapoona vilema wanatembea, wanapoona Nabii Flora anafufua akina Mariamu Yule wa  Morogoro, wanapoona watu wanafanikiwa bado wana mashaka. Napenda nikwambie leo, ondoa mashaka yako, ondoa wasiwasi. Yuko Yesu Mnzareth anayetenda haya. Mnaona ni mwanadamu wa kawaida, hata mkichukua darubini na kugalia mnaona ni kivuli.

Nabii Flora Peter

Kuna mama alikuja hapa amepotelewa na mwanawe, nikawambia, nenda Gongo la Mboto katika soko la kati utakuta. Mwingi alikuja amepotelewa na ndugu yake nikamwambia nenda Kibamaba utamkuta mwanao, sio kitu rahisi, kama unaweza tabiri. Karama hii inatoka kwa Mungu wala sio kwa nguvu za wanadamu.

Na mimi Nabii Flora ninaita watu kutembea, nnaita njooo upokee upako na Baraka. Kuna leo watu wataitwa na Bwana njoo, wataketishwa na Bwana wetu Yesu Kristo, wataenda kufanikiwa mambo yao. Ninaona kuna watu 7 tayari, Bwana anawaita njoo. Kuna watu hapa mbele, haponyuma , huko kati na huko pembeni mwa kanisa, wanaanza kurushwa.
Ninakuambia njoo mama yangu, tembea juu ya maji, yamkini Yesu anakuita sasa, maana Yesu alimwita Petro njoo njoo njoo. Ninyo ambayo Yesu anaiita akisema njoo kwangu.


Hebu tembea juu ya wacahawi, hebu tembea juu ya mateso yako, hebu tembea juu ya shida uliyonayo, hebu tawala mateso yako, hebu tawala kesi uliyonayo.

Kipindi ulikuwa na pesa ulikuwa unaheshimika, lakini sasa umebakiza historia, watu wanakudharau. Ninakuambia leo utatembea juu ya maji kama Yesu. Ninaona kuna watu zaidi ya 40 wamezama kiroho, ninakwenda kukutoa katika hali ya kuzama. Leo ninataka kuona watu wakipiga yowe kama Petro wakisema Bwana niokoe. Fungua mdomo wako sasa, piga kelele sema Bwana niokoe kwa maana ziko nguvu zitashuka. Upo upepo wa mlisho utakufunika , ipo nguvu ya uponyaji inaenda kushuka sasa, ninaona watu wanaenda kuinuliwa, kipato kilichozama kinainuliwa, cheo chako kimezama kinainuliwa sasa, watu wamekalia barua yako, biashara zako zimekaliwa, leo ninaenda kuzichoma hizo roho chafu
SOMO LINAENDELEA




Kwaya Kuu iliyofika kanisani kwaajili ya kuimbia Mungu katika kanisa la nabii Flora

Baada ya Nabii kuhesabu mara tatu, watu wa Mungu waliangushwa na nguvu za Mungu chini na kulaliana
Mungu pekee ndiye anayefuta machozi ya wenye haki

Kutoka kushoto ni daniel Basila, Anna, Albert, Mama Lugano na Jury-wahudumu kanisani

Kutoka kulia ni Faith, Mrs. Lugano na Albert
xxxxxxxxxxxxxxxxx



Maombezi ywakiendelea katika kanisa la nabii Flora
wanakwaya wa nabii Flora



Kwaya Kuu wakimwimbia Mungu. Hawa wanaimba Acapela, hawatumii vyombo vya muziki ila sauti yao tu.
Maji yakiombewa
Mama akimlilia Mungu wake
Matroni akiwahudumia watu katika kipindi cha maombezi yanayoendeshwa na nabii Flora
Taabu ni mbaya katika maisha ya mwanadamu
Imani ni kila kitu
Mungu ndiye njia ya uzima na kweli. Ukimkimbilia utaona baraka zake.
KIPINDI CHA SUKRANI

KAKA ALIKUWA OMBAOMBA NA HANA KITU SASA AJENGA NYUMBA MBILI ZA KISASA NA ANATEGEMEA KUNUNUA GARI
Bwana Yesu..Kwa jina ninaitwa Daniel. Namshukuru Mungu wa Nabii Flora. Nilikuwa nauguliwa na mtoto wangu mwenye miaka 13. Miaka 10 alikuwa anaumwa, nilitembea kote hakuna nilichofanikiwa na bimaliza milioni 20, lakini baada ya kufika kwa Nabii Flora nimebadilika. Nilipokuja hapa kwa Nabii Flora na binti yangu sikuwa hivi nilikuwa nimechoka kabisa sina hata pesa ya kula. Mama Mzungu aliweza kunisaidia sana wakati hali yangu ni ngumu, alikuwa akinipa mchele na mboga. Pia namshukuru Bwana Albert ambaye alikuwa akinitia moyo kila wakati na bila kumsahau Mchungaji Ansilla.
Na sasa Mungu ameniinua ninajenga nyumba mbili za kisasa, na nimeweka mafundi 20 wanaendelea na ujensi. Na pia nategemea kununua gari.
(Baada ya shukrani zawadi ilikabidhiwa kwa Nabii Flora, na Nabii Flora alimuombea na kumuachia Baraka kwake na kwatu wengine. Nabii Flora alimshukuru Mama Mzungu kwa msaada wake.)


KIPINDI CHA SHUHUDA
DADA ALIYESAHAU BIDHAA AZIPATA
 Bwana Yesu asifiwe. Mimi nilikuwa nimesahau bidhaa ambazo sio zangu. Baada ya hapo ikabidi niende stand, na sikuweza kuona. Nikaja hapa kanisani na kumwambia Nabii kuwa mimi sijaibiwa, ila nimesahau bidhaa za watu. Nabii akanambia, wala usijali Mungu anaweza, akasema nenda pale kituoni ulipokuwa na utaona bidhaa zako. Nilipofika niliona bidhaa nilizosahau.
MAMA ALIYEKUWA HAONI KWA MUDA TANGIA 2004 APATA UPONYAJI WA KUONA
 Bwana asifiwe. Ninamshukuru Mungu kwa kumponya mama yangu alikuwa ameadhirika na macho tangia mwaka 2004. Tulipopigiwa simu kuwa mama anaumwa, tukamwambia nabii Flora, na nabii aliombea maji na ilipofika siku 7, mama aliweza kutembea peke yake na gongo akaliacha.
DADA ALIYEKOSA KAZI KWA MUDA MREFU ALETA CV KWA NABII FLORA NAYE APATA KAZI
Ninasimama kwa niaba ya dada yangu aliyekuwa akitafuta kazi kwa muda mrefu sana. Alipokanyaga hapa na CV zake aliombewa na siku ya Ijumaa alienda kufanya interview na kuweza kupita. Amepata mkataba wa maana siku ya Jumatatu.
MTOTO ALIPOTEA KWA NJIA ZA AJABU APATIKANA
Bwana asifiwe..Mimi natakoka Yombo Viyuka jijini Dar es Salaam. Ni mara yangu ya kwanza kuingi hapa katika ibada ya Jumapili. Siku ya Jumatatu binti yetu alitoweka nyumbani Jumapili katika hali ya kutatanisha. Huyu binti aliuugua karibu miaka mitano, na hajawahi kutoka na kwenda mahali popote. Lakini siku ya Jumatatu asubuhi akatoka, na hatukujua ameelekea wapi. Tulianza kupigia simu na kuwauliza kuwa yuko wapi. Kuna shemeji yangu anayekaa Tegeta.tulipomupa habari kuwa binti yetu amepotea> Shemeji yetu akachukua picha ya kijana wetu aliyepotea na kuja nayo hapa kanisani. Nabii Flora alipotazama akasema mtoto huyo amechukuliwa na wachawi, na wamemuweka masokoni, akasema nenda Tandika  soko la Kati na mtampata. Tukaenda na kumuona akiwa hana fahamu yoyote, hata jumatanio tulipomuleta hapa, sura yake ilikuwa ngumu kwetu kumtambua, nay eye mwenyewe alikuwa hana mawasiliano na sisi, tulikuwa tukimshika kwa nguvu kamam vile tumeshika kichaa Fulani

Nabii alipomuwekea mkono tu, ndipo sura iliporudim na kuanza kuchangamka

DANIEL ASHINDA KESI BAADA YA KUOMBEWA FAIL LAKE


Bwana asifiwe. Nilikuwa na kesi ya kudhurumiwa gari kwa muda wa mwaka na zaidi, ilikuwa mwaka 2012 Feb, nikashinda kesi, na niliposhinda kesi alikata rufaa. Mwezi wa Dec. 2012 mke wangu akaja na faili hili kanisani, akampa nabii na kumueleza kuwa tuna kesi na tumeshinda ile mtu mwenyewe amekata rufaa. Nabii akaombea na akasema, hakika utashinda kesi. Wiki iliyopita tarehe 28.02.2013 ilikuwa siku ya hukumu. Nilisafiri kwenda Morogoro na nikampigia simu Nabii kuwa ninaenda Morogoro kwaajili ya kesi. Na nilipofika pale nikashinda kesi

Ushuda wa pili ni usiku wa kuamkia usiku wa leo. Nilikuwa na mke wangu, ambaye ni mjauzito wa wiki kama thelathini na kitu. Siku ya jana alisikia mtoto akicheza ambayo sio kitu cha kawaida. Alipofika saa saba usiku akawa anasikia maumivu yasiyo ya kawaida (uchungu). Tukaenda sebuleni nay eye akawa amepiga magoto sebuleni akiomba lakini haikusaidia. Nikakumbuka kumpigia dakatari wake saa tisa usiku, akaomba kuongea na mke wangu na kumwambia hilo suala ni la kawaida, na akanambia na mimi kuwa nimpeleke hospitali. Likaja wazo na kujiuliza kwanini nimpeleke hospitali wakati nabii Flora yupo. Mke wangu akawa mgumu kuruhusu kumpigia nabii Flora (nadhani ni pepo lilikuwa linazuia). Nimampigia nabii mida ya saa 12 alfajiri. Nabii akamuombea mke wangu na baada ya kumuombea nikaongea naye nabii na kusema anamuona mtoto ni mzima na anacheza. Baada ya hapo mtoto alicheza na kupiga mateke zaidi ya mara 10.

MAMA ALIYEACHWA NA MUME WAKE KWA MUDA WA MIAKA 33 NA WATOTO WAKE KUSAMBARATIKA, SASA MUME ARUDI NA WATOTO WAJA NA VIJUKUU.

Mungu amenitendea makuu katika madhabahu hii. Kwanza nilikuwa nimetengwa na watoto wangu kwasababu ya kutengana na mume wangu kwa muda wa miaka 33 na watoto wakasambaratika na wakawa hawanipigii hata simu. Nilipokuja kwa mtumishi wa Mungu kwa nabii Flora, aliweza kuniombea na watoto wakawa wanakuja nyumbani, wakawaleta na wajukuu ambao nilikuwa siwajui. Na la mwisho tumeweza kurudiana na mume wangu

BABA ALIYEKUWA ANAOTA NDOTO NA WATU WALIOKUFA AOMBEWA NA SASA HAOTI TENA


Mimi Nimeokoka Mwaka 1991 na kipindi hicho chote nilikuwa naota ninashi na watu waliokufa na wakati mwimngine nafukuzwa na nyoka. Nilipofika hapa kanisani kwa Nabii Flora, muda wiki nikakuta wanauza picha za Nabii Flora, nikanunua moja na nilipofika nyumbani nikailalia. Nilikuwa naamini kuwa nabii ni hatari. Nilipoilalia nikaota niko katika nchi ya samba wala watu na kila sehemu nikipita wako. Nikamweleza Nabii akaniombea na kuanzia hapo sijaota tena. Tunatakiwa kuwatii manabii. Nabii Flora ni nabii halisi

MAMA ALIKUWA AMEJAA MAJI KATIKA UZAZI  AKIWA MAJAUZITO APONA

Mimi ni mke wa daktari katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili,  nilienda hospitali na kupimwa baada ya kujisikia naumwa. Nilipopigwa Utra Sound nikaambiwa mfuko wa uzazi ukejaa maji, na nilikuwa sisikii mtoto akicheza tumboni mwangu. Nilikuja kwa nabii Flora, nabii akanambia na mimi ninaona hayo maji, nitakusaidia kwani ni nguvu za giza. Baada ya kuniombea nakasikia mtoto hachezi tena na tumbo langu lilikuwa kubwa na sasa limepungua.

MTOTO ALIYECHANGANYIKIWA APONA BAADA YA MAOMBEZI
Mtoto wangu ameugua miaka 20. Mwanangu alipelekwa Muhimbili akawa analala kwa kamba, amefungwa mikono na miguu. Nikawa najiuliza nitampeleka wapi huyu mtoto?. Baada ya muda Fulani nikasikia sauti ikinitokea mara tatu ikiniiambia nimpeleke kwa nabii Flora. Nabii Flora alikuwa hanijui na mimi simjui. Nilipofika hapa kanisani Nabii Flora akabariki maji. Nikatoka hapa kanisani na kuelekea hospitalini Mwimbili, na baada ya kufika nikampa mgonjwa wangu maji, kitenge na chakula. Mgonjwa aliweza kula chakula wakati siku za nyuma alikuwa hali chakua, akanambia chakula cha leo ni kitamu sana mama yangu.

MTOTO ALIYEKUWA ANAKAMATA NAMBA ZA MWISHO KATIKA MASOMO SASA ANAKAMATA NAMBA BILI DARASANI.
Mimi ninatokea Gongo la Mboto. Mwanangu wa pili wa kitado cha pili ambaye alikuwa akifanya mitihani ya kuingia kidato cha tatu. Mwanangu alikuwa akikamata namba za chini katika mitihani aliyokuwa akifanya. Nikatoka nyumbani nikaja kulala hapa kanisani kwa Nabii Flora, na ilipofika asubuhi nikaonana naye Nabii Flora. Nabii Flora akaniombea na kunitabiria ya uwa mwanao atakuwa anakamata namba mbili. Na sasa mwanangu anakamata namba mbili






Comments