RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BENNY HINN ACHANGISHA ZAIDI YA BILIONI 3 KUMALIZA MADENI

Mchingaji maarufu wa kimataifa, Benny Hinn, ameripotiwa hivi karibuni kuwaomba waumini wake kuchangia dola milioni mbili na nusu, sawa na zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa hela za Kitanzania, ili kuinusuru huduma yake dhidi ya madeni.


Mchungaji Benny Hinn. ©Bennyhinn.org

Kwa mujibu wa taarifa ambayo pia imewekwa kwenye tovuti yake, Mchungaji Hinn amewataka waamini wa mafundisho yake kuchangia huduma hiyo ili Bwana awarudishie maradufu kwa kadri ya utayari wao kwenye kuchangia, kwani tayari wana ahadi ya fungu kama hilo, iwapo tu waumini watachanga ndani ya siku 90

"Mungu anataka huduma yenu isiwe na madeni kabisa, na nataka nipande mbegu iliyobarikiwa ili kukuwezesha kupiga hatua kubwa kutoka katika madeni kabisa", inaeleza sehemu ya ujumbe wa mtu huyo ambaye anasemekana kuwa rafiki wa karibu wa Benny.

Tayari Benny Hinn ameshawafikishia waumini wake ujumbe wa rafiki yake huyo ambaye ameelea kumuamini sana, na sasa kinachosuburiwa ni ndani ya siku 90 kwa ajilii ya kukamilisha michango hiyo, vinginevyo mbegu hiyo kutoka kwa mtumishi huyo ambaye hajatambulishwa bado, haitotolewa.

Iwapo wananchi watachanga kiwango hicho cha pesa, basi mpoanda mbegu huyo naye atatoa kiasi hicho hicho cha pesa, ila kama wakizidisha kiwango, basi na mpanda mbegu huyo atapanda dau zaidi. GK imebaini.

Comments