RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UTAFITI UMOJA WA MATAIFA: CHAGUA VIPAUMBELE MAISHANI



Picha iliyonakiliwa na Gospel Kitaa kutoka tovuti ya my world © My World 2015

Umoja wa Mataifa kupitia taasisi yake ya utafiti ya My World, inaendesha utafiti wa kujua vipaumbele, na namna ambavyo ungependa ulimwengu uwe. Kwa maana ya vitu gani muhijmu kwako na kwa familia yako maishani.

Zaidi ya watu milioni mia tatu duniani wameshachagua vipaumbele vyao, nawe bila kupoteza nafasi hii, unaweza kuingia kwenye tovuti ya my world na kuchagua vipaumbele, kwani hadi leo hii Tanzania ina takriban watu mia tatu waliochagua, huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikiwa na takriban watu 4,000 wakati Kenya ikiwa na watu zaidi ya 1,000, na Rwanda ikiongoza kwa ukanda wa Afrika Mashariki ikiwa na watu zaidi ya 15,000 waliochagua vipaumbele vyao tayari.

Miongoni mwa chaguzi ni pamoja na Elimu bora, Serikali nzuri inayowajibika, huduma bora za afya, usafiri na barabara nzuri, usawa wa kijinsia na kadha wa kadha. tembelea www.myworld2015.org ili kukamilisha chaguzi zako, na kuwezesha Umoja wa Mataifa kujua vipaumbele vya watu maishani.


Baadhi ya vipaumbele ambavyo walimwengu wamechagua, chaguzi za Watanzania zikiwa pembeni ya chaguzi za dunia nzima kwa ujumla hadi hivi sasa. Jedwali zinazofuatia zinaonesha namna watu walivyochagua kutokana na umri, jinsi, nk. © My world 2015

Comments