RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

APOSTLE GIDEONI T MUTALEMWA AFANYA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA DVD YAKE MPYA YA SAMBAMBA NA YESU

Baada ya kuona hajatendea haki video yake ya kwanza ya "Sambamba na Yesu", Apostle Gideon Mutalemwa ameamua kufanya shooting upya kwa kiwango cha juu sana ukilinganisha na shooting ya mara ya kwanza. Shootingi hii imefanyika Bagamoyo, kanisani Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi kwa Nabii Flora Peter ambako Apostle Gideon Mutalemwa anaabudu, Bahari ya Hindi, Makumbusho Dar es Salaam, TAZARA Dar es Salaam, Msitu wa Kisarawe Dar es Salaam na mazingira mbalimbali.

Baadhi ya watu walihoshiriki katika video hii ni upande kucheza (dancing) ni Linah. Veronica, Sakinah, Elizabeth, Keny, Winfrida, Marry, Rich.na Traditiona Dancers
Kutokana na maelezo ya ITC wanaedai video itakuwa sokoni baada ya mwezi mmoja kutoka sasa, (Mwezi wa sita mwaka huu 2013)

Apostle Gideon anamshukuru sana Mungu kwa kwa maarifa na ufahamu wa kuboresha kazi yake katika kiwango cha juu sana. Pia anawashukuru jamaa na marafiki kwa ushauri wao na ushirikiano wao katika kazi nzima ya kufanya shooting.
Wasiliana na Gideon Mutalemwa kwa
simu +255719697252
Blogu: www.apostlegideon.blogspot.com

Angalia Picha
 Apostle Gideon Mutalemwa-


 Apostle Gideon Mutalemwa

 Kutoka kulia ni Sakinah, Veronica, Winfrida, Eliza, Linah na Apostle Gideon wakiwa bahari ya Hindi Dar es Salaam








Wakiwa Bagamoyo






Wakiwa katika Hoteli ya Kiromo Bagamoyo

 Marry

 Keny

Wakiwa Tangi Bovu dar es Salaam katika shamba la babu yake na Apostle Gideon, mzee Lutimba









Comments