RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SEMINA JIJINI ARUSHA, MARANATHA CHRISTIAN CENTRE

Kwa uliyekosa leo hii, bado una nafasi ya kufika pale Maranatha Christian Centre kesho na kumalizia Jumapili. Ni kuanzia saa kumi hadi saa kumi na mbili jioni, ambapo kwa Jumapili tarehe 2 Juni itafanyika kuanzia saa saa moja na robo hadi saa tatu na nusu, na kisha kwenye ibada ya pili, saa nne kamili hadi saa sita mchana

Kwaya ya Maranatha Shalom, Maranatha Glory pamoja na waimbaji mbalimbali watahudumu kwenye semina hii ya Uamsho Revival Meeting ambayo itahubiriwa na watumishi kutoka nchini Marekani, ambapo imeandaliwa na Askofu Eric Mukwenda wa Maranatsha Christian Centre lililoko Mianzini, Arusha Mjini.

Mchukue mwenzako kwa pamoja mje mpokee miujiza yenu, kwa kuwa atakayelitafakari neno atapata mema.

Comments