RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

TAMASHA LA KWANZA JUNI HII ARUSHA

Kati ya vitu ambavyo unatakiwa kuanza kufanya Juni hii, ni pamoja na kumsifu Bwana. Na kwa nafasi yako, tamasha la uponyaji na kukuweka huru upate kumuabudu Mungu katika Roho na kweli kwenye kanisa la Rehoboth Victory Mianzini jijini Arusha Juni 2 2013.

Tamasha hili litakuwepo kuanzia saa tisa alasiri, ambapo baadhi ya waimbaji watakaohudumu ni pamoja na Jackson Benty, Neema, Joshua Ngoi, Victory Choir, Grace Kimati, Grace Mwanjombe, na TAG Galilaya Ngaramtoni.

Tamasha hilo litatanguliwa na ibada asubuhi ambapo kutakuwa na ibada maalum ya uponyaji na maombezi kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa sita mchana, ambapo mnenaji atakuwa Mtume Naston Ngoingoi.

Kanisa lipo kituo cha pili kabla ya kituo cha daladala cha Technical ama Tripple A. Nyote mnakaribishwa bila kukosa.

Comments