RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WAKRISTO HATARINI KUTOWEKA MISRI


Mohammed Morsi, Rais ambaye anaonekana tishio kwa uwepo wa Wakristo nchini humo kwa kuwataka aidha kusilimu, kuuenzi uislamu ama kuondoka nchini humo wale wote wasioutaka, akimaanisha Wakatoliki wa Kicoptik. ©Mohamed Abd El-Ghany/Reuters

Wakati serikali ya Misri ilipopinduliwa madarakani, ilikuwa ni dhidi y autawala dhalimu na wa kidikteta wa Rais Hosni Mubarak, kila mtu alishangilia, wananchi wakijua kwamba ni mwanzo mzuri wa kuongozwa na mtu atakayefuata utawala wa demokrasia, lakini kwa sasa hali ndivyo sivyo, kwani sasa Wakristo nchini humo wako hatarini kuangamamizwa kabisa wasiwepo.

Haya ni mawazo ya mgombea wa zamani wa urais nchini Misri, Bwana Hamdeen Sabbahi alipokuwa akizungumza kwenye kongamano ambalo lilikuwa linazungumzia kuhusu uhuishwaji wa umoja wa kitaifa na menejimenti ya dini nyingi.

Bwana Sabbahi amesema kuwa serikali haifanyi chochote wala kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo husika wale wote wanaohusika ama kuhusishwa kwa namna moja ama nyingine na kushambulia makanisa.

Aidha Bwana Sabahhi ameongeza kuwa hadi hivi sasa wameshaanza kukusanya sahihi za kutokuwa na imani na Rais Morsi ambaye yuko sanjari na Islamic Brotherhhod, ili waweze kumuondoa kwa njia ambayo haitamwaga damu.


Imenakiliwa Christian Post

Asante: GK

Comments