RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RULEA SANGA AFIWA NA MTOTO WA SHEMEJI YAKE EDNARA SANGA MAKONGO JUU DAR ES SALAAM


Rulea Sanga wa Rumafrica
Siku ya jana ilikuwa ni siku yake ya mwisho ya kuishi na sisi Marehemu Vailet Kipangula. Mungu alimpenda zaidi na kuamua kumchukua mida ya saa nane mchana akiwa anaelekea Muhimbili. Vailet Kipangula alikuwa akisumbuliwa na uvimbe tumbo kwa muda mrefu. Marehemu alikuwa akilalamika sana na ikafikiwa wakati akawa anatamani kuchukua kisu kujiua kutokana na maumivu aliyokuwa nayo.


Marehemu mara ya kwanza alilazwa Muhimbili na baadae kuruhusiwa kurudi nyumbani kwa matibabu. Alipofika nyumbani hakuweza kumaliza hata mwezi bali Mungu alimuwezesha kutimiza wiki mbili na siku ya jana ya tarehe 28/06/2013 ikawa ndio siku yake ya mwisho.

TARATIBU ZA MAZISHI
Marehemu Vailet Kipangula  atazikwa siku ya Jumapili katika makaburi ya Sinza. Kutakuwa na misa na kumuaga nyumbani kwake Makongo Juu karibu na minara ya ITV kuanzia saa 6:00 mchana - 8 mchana na baada ya hapo kutakuwa na chakula, mazishi yatafanyika saa 9:00 mchana Sinza hapa jijini Dar es Salaam.

Ninawashukuru Wote
Rulea Sanga
+255 715 851523

Comments