RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UPENDO BENSON ASEMA, "NENO LA MUNGU LINAPUMZI NA LINAMUUJIZA WAKO"..MSIKIE SASA

Neno la Mungu ni hai, lina pumzi ya Mungu ndani yake maana neno hili ni Mungu mwenyewe.. (Yohana 1:1) na unaposikia Neno la Mungu likihubiriwa, ujue halikukufikia bure bali limebeba muujiza wako, inaweza kuwa ni uponyaji wa moyo au mwili, kufunguliwa, kuonywa, kuinuliwa, kutahadharishwa jambo, kuongozwa kwenye njia sahihi nk.(Luke 4:18-19). Ila unachohitaji wakati unapolisikia neno ni "NEEMA YA MUNGU YA KULIPOKEA HILO NENO SAWASAWA KABISA NA JINSI ROHO WA MUNGU ALIVYOKUSUDIA".
 Ukizubaa kidogo tu shetani akapata nafasi ya kuingia ktk mawazo yako, anatwist akili yako, neno likija unalipokea in a twisted way, unajikuta unaendelea kubaki kama ulivyo miaka na miaka, wengine wanafunguliwa, wewe unabaki vilevile.. Na ndio maana saa zingine mahubiri yanapogusa kwenye maonyo mwingine anakwazika mpk anaamua hata kuhama kanisa nk. "Bwana akupe Neema ya kulisikia neno la Mungu (kwa usahihi kabisa) sawasawa na Roho Mtakatifu alivyokusudia ili uweze kufunguliwa na kuwekwa huru, naharibu kila vizuizi vya mwovu vinavyosababisha usipokee neno sawasawa na kusudi la Mungu, kwa Jina la Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai,AMEN". Good Morning! — at Mbezi Beach, Dar Es Salaam.

Comments