RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KIJANA AKIMBILIA KANISANI BAADA YA BABA YAKE KUMWEKA REHANI ALIWE NYAMA NA WACHAWI


Wiki iliyopita nilienda kutembelea tawi la kanisa la Ufufuo na Uzima - Kilombero, nikiwa huko nilipata wasaa wa kuongea na kijana mmoja ambaye aliniambia jambo moja la ajabu sana, kijana huyo alikuwa ametoroka nyumbani kwao na kukimbilia kanisani. Nilipomuuliza akaniambia kuwa, ni kwasababu alikuwa amekopewa nyama. Nikavutiwa kumuuliza zaidi, ndipo aliponiambia kuwa baba yake ambaye alikuwa mchawi alikula nyama za watu (wachawi wenzake) lakini ilipofika zamu yake kutoa akawa amemweka rehani mwanaye (huyo kijana). Mimi nilipopata taarifa ndipo nikakimbia kuja hapa, kijana huyo alieleza. Jambo hilo lipo kabisa na kuna watu leo ambao wanaishi huku wakiwa wamekopewa nyama na wachawi bila kujua:

Jambo hili linaweza kuonekana ni jipya kwako lakini Biblia inalitaja, kuwa lilikuwa likitendeka na watu waliokuwa wakimwabudu mungu moleki.

Kwanini wachawi wanakula nyama za watu kwa mujibu wa Biblia.

Ukweli juu ya ya watu wanaokula nyama za watu katika Biblia.:
Walawi 18:21; 20:2"2 Tena uwaambie wana wa Israeli, Mtu awaye yote miongoni mwa wana wa Israeli, au miongoni mwa wageni waketio katika Israeli, atakayetoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, sharti atauawa; wenyeji wa nchi watampiga kwa mawe.";
Neno kizazi chake halina maana ya kizazi cha mwanamke bali lina maana ya watoto wake.

Kujua ukweli huu kuwa neno hili lina maana ya watoto; utaipata katika 2Wafalme 23:10 "Naye akainajisi Tofethi, iliyomo katika bonde la wana wa Hinomu, ili mtu asipitishe mwana wake au binti yake motoni kwa Moleki.", huyu moleki ni mungu aliyekuwa anaabudiwa kipindi hicho, ambaye kwa yeye watu walikuwa wanatoa sadaka za watu. Yeremia 32:35 "Tena walijenga mahali palipoinuka kwa Baali, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwapitisha wana wao na binti zao katika moto kwa ajili ya Moleki, jambo nisilowaagiza; wala halikuingia moyoni mwangu kwamba walitende chukizo hilo; wapate kumkosesha Yuda.", kuwapitisha wana wao katika moto (sacrifice) maana yake ni kuwatoa kafara kwa mashetani.

Unaweza sema kuwa haya mambo yalifanyika katika agano la kale tu, bali biblia inatuonyesha pia katika Matendo ya Mitume 7:43 "Nanyi mlichukua hema ya Moleki, Na nyota za mungu wenu Refani, Sanamu mlizozifanya ili kuziabudu; Nami nitawafahamisha mwende mbali kupita Babeli."

Kumbe hata katika agano la jipya moleki yuleyule ambaye alitolewa sadaka ya watoto katika agano la kale ametajwa tena. Kimsingi, moleki ni shetani yuleyule ambaye anapokea nguvu kutoka katika damu na nyama za watu. Hayo mambo yaliyokuwa yakifanyika kipindi hicho bado yanafanyika hata sasa.

Hizi zote ni sadaka zinazotolewa kwa mashetani.
2Wafalme 10:20, "Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani." Wamwabuduo shetani hutoa sadaka za watu kwa mashetani, jambo hilo liko wazi kabisa. Ndivyo walivyofanya kwa moleki kwa kutoa wana na binti zao kwa mashetani.

Kwanini wanatoa sadaka kwa mashetani.
Wachawi hutoa sadaka za watu kwa mashetani kwasababu ya nguvu iliyo ndani ya damu, biblia inasema "damu ni uhai" hivyo damu ya mtu ina nguvu ya uhai ndani yake. Kwasababu hiyo, wachawi wanapokula nyama ya mtu na kunywa damu wanapokea nguvu ya uhai iliyo ndani ya damu.

Kinachotokea
Anayetenda kazi ya kuua huu mwili ni shetani, hivyo mtu alikwisha kukopewa nyama anatumiwa pepo la kumuua, na hapa mtu huyo ataonekana ana matatizo, magonjwa yasiyotibika kumbe ni hatua za kuelekea kufa. Kuna watu ni wagonjwa leo kumbe ni matokeo ya watu waliokwisha kutoa kwa mashetani.

Usikate tamaa Yesu anaweza.
Yawezekana upo kwenye matatizo leo lakini ni muhimu kujua kuwa unapookoka unatakiwa uchukue hatua nyingine ya kupigana vita ya rohoni dhidi ya vifungo vya kutoka kwa wachawi. Hakuna kumiliki bila kupigana hata hivyo katika vita hii tumeahidiwa ushindi.

Wakolosai 1:13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;
14 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;

Unapookoka unahamishiwa katika ukoo wa Yesu, shetani anakuwa hana nguvu tena katika maisha yako.

Comments

kweli walimwengu wana mambo.