RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MCHUNGAJI WA KANISA AMLAWITI MTOTO HUKO MAJOHE JIJINI DAR ES SALAAM.


Mchungaji wa kanisa mojala kilokole lililopo Kichangani majohe ,Dar es salaam aliyetjwa kwa jina moja la Benard anadaiwa kutiwa mbaroni kwa tuhuma za ulawiti wa mtoto wa kiume (jina tunalo)mwenye umri wa miaka 15. Kwa mujibu wa mdogo wa mchungaji huyo aliyejitambulisha kwa jina la Hamis, kaka yake huyo alikamatwa wiki iliyopita baada ya watu waliojitambulisha kuwa ni askari kufika nyumbani na kumuweka chini ya ulinzi.

Alisema kuwa katika kuishi na kaka yake huyo, aliwahi kumuona huyo mtoto anayedaiwa kulawitiwa mara moja tu kwani yeye bado ni mgeni.


Kwa mujibu wa dogo aliyedaiwa kuingiliwa, alikutana na mchungaji huyo mwaka jana maeneo ya Stendi ya Banana-Ukonga, Dar ambapo alimuomba na kumwambia kuwa alikuwa anatafuta mtoto wa kumfanyia biashara ya mayai huko Majohe nyumbani kwake.


Alisema kuwa alikataa na kumwambia hawezi kwenda naye bali aende akazungumze na wazazi wake nyumbani.

 
Alisimulia kuwa baada ya hapo, aliongozana na baba mchungaji hadi kwa wazazi wake ambapo walikubaliana kuwa kila mwezi atamlipa mshahara wa shilingi 30,000.


Baada ya makubaliano hayo ‘dogo’ alisema kuwa aliondoka na mchungaji na baada ya kukaa kwa muda mfupi huku akiendelea na biashara ya mayai, mchunga kondoo huyo wa Mungu alianza tabia ya kumfanyia unyama huo huku akimdanganya kuwa atampa simu.


“Kuna wakati kweli ananipa simu kwa muda na kuninyang’anya.
“Kwa siku moja alikuwa ananiingilia mara mbili, asubuhi na jioni,” alisema mtoto huyo kwa uchungu.


Alisema kuwa baba mchungaji aliendelea kumfanyia ‘usodoma’ kwa muda mrefu.


Alisema baada ya kufika nyumbani kwa wazazi wake, mama yake alimgundua na kumtaka kueleza ukweli.


“Nilimweleza baba na mama jinsi mchungaji anavyonifanyia ukatili, walimwita nyumbani wakiwa tayari wameshaandaa polisi jamii, alipofika aliwekwa chini ya ulinzi lakini aliwaomba msamaha polisi jamii hao pamoja na wazazi huku akiahidi kutorudia tena.


“Kila mtu alikubaliana na msamaha na kumpa masharti kwamba afilisiwe vitu vyake vyote kama faini ya kosa.


“Alikubali, akafilisiwa vitu vyote  vikakabidhiwa kwa wazazi wangu ambapo baba yangu alikuwa mgonjwa hivyo kutokana na kukosa uwezo aliviuza vitu hivyo kwa ajili ya matibabu na mwishowe akafariki dunia,” alisema.


Mtoto huyo aliendelea kusimulia kuwa baada ya kuachana na mchungaji huyo kwa muda mrefu, kuna msichana mmoja mtaani kwao anayejulikana kwa jina la Asha ambaye alimfuata na kumbembeleza kuwa waende tena kwa mchungaji huyo, naye akakubali na baada ya kufika huko huku wakiwa wameambatana na mtoto mwingine wa kiume (17), mchungaji huyo alimfanyia tena mchezo huo na kumpa fedha huyo msichana hivyo akawa kama yeye ndiye aliyeenda kuwauza.


“Juzi hapa mtaani kwetu aliuawa mwizi mmoja, baada ya kuona kile kifo nilimuita mama yangu na kumwambia natubu maovu yangu ndipo nikaanza kumwelezea jinsi nilivyorudi tena kwa mchungaji kwa kushawishiwa na huyo Asha,” alisema mtoto huyo.


Huku mchungaji huyo akiwa na tuhuma hiyo ya kufanya mchezo huo na mmoja chumbani na mwingine sebuleni, mwanaume ambaye ni rafiki wa mchungaji huyo aliyetajwa kwa jina moja la Rahim naye akaingia kwenye mkumbo na kuendeleza dhambi ya kuwasulubu vijana hao. 


Mchungaji huyo, rafiki yake na Asha, wote waliswekwa nyuma ya nondo za mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Stakishari, Dar na kufunguliwa shitaka namba STK/RB/13160/2013-ULAWITI wakisubiri kesi yao kuanza kuunguruma.


Wanahabari wetu walifanikiwa kuzungumza na askofu wa mchungaji huyo, Grace Joseph ambaye alikuwa na haya ya kusema: 


“Kwa jinsi ninavyomjua mchungaji wangu siamini kama amefanya kitendo hicho hivyo tuhuma hizo sikubaliani nazo kabisa ila polisi wanaendelea na uchunguzi.”
Source: Vituko vya Mtaa

Comments