RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PHOTOCOPY YA STICKER YA NABII TB. JOSHUA NA TONE LA ANOINTING WATER VYA BADILISHA MAISHA YA ROSE MWAIHOJO

Rose Mwaihojo amekuwa akimuota sana Nabii Tb Joshua kwa muda mrefu, na alikuwa akitamani sana kuonana naye lakini hakuweza kubahatika kuonana naye. Rose amekuwa akitamani sana kupta Anointing Water na Sticker akiamini kuwa akitumia tu maisha yake na matatizo yake yata kwisha. Rose amekuwa akijibiisha katika kutafuta Anointing Water na sticker kwa nguvu zote.

Rose Mwaihojo alikuwa akitafuta sana Anointing Water ya Nabii TB Joshua bila ya mafanikio kwa muda mrefu sana.  Alikuja kubahatika na kupata tone la Anointing Water kutoka kwa rafiki yake anaishi Dar es Salaam. Rose aliweza kuchanganya na maji ya kawaida na aliweza kuyatumia hayo maji yaliochanganywa na Anointing Water, na alipokunywa alitapika sana.

Rose aliweza kubahatika kukamata sticker ya Nabii TB Joshua kutoka kwa rafiki yake na  alipokamata tu mikono yake ilianza kupata ganzi, tumbo lake lilianza kuvurugika. Baada ya hapo alimuomba rafiki yake akatoe photocopy ya hiyo sticker akiamini itafanya jambo katika maisha yake. Rose alisema alipoitoa photocopy alienda nyumbani kwake nakuweka chini ya mto wa kulalia na alipoweka tu alisikia sauti ikisema "Toa Hivyo Vitu" .

Hali yake kiuchumi na kiafya tangia ametumia sticker hiyo na Anointing Water imeanza kubadilika kwani hapo nyuma alikuwa na matatzo makubwa sana kipindi hajatumia sticker hiyo na Anointing Water. Alisema, Kabla ya ya kutendewa muujiza huo, alikuwa akimuota sana Nabii TB Joshua katika ndoto.

Dada huyu anaomba sana maombi ya Nabii TB Joshua ili aweze kufanikiwa katika mitihani yake aliyofanya.

Unaweza kuwasiliana na Rose kwa simu +255 755440648 kwa ushuhuda zaidi

Mwandishi
Rulea Sanga
www.rumaafrica.blogspot.com
+255 715851523

Comments