RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SIONI SHIDA KWA WACHUNGAJI MASHOGA, ASEMA PAPA FRANCIS


Papa Francis akijibu maswali ya wanahabari wakati akirejea kutoka Brazil. ©AP
Ni siku moja mara baada ya kurejea kutoka kwenye siku ya vijana duniani, tamasha la asili ya kanisa katoliki ambalo limefanyika mwaka huu nchini Brazil. mara baada ya kurudi Ulaya, Papa Francis amezungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza katika mkutano, na kunukuliwa akizungumzia kuhusu watumishi mashoga.

Katika mkutano na waandihsi wa habari ambao umechukua takriban dakika 82 wakiwa angani, Papa Francis amesema kuwa hana shida na mtu ambaye ni shoga na anamtumikia Mungu kikamilifu.

Nitanukuu kwa Kiingereza na kisha kutafsiri kwa kiswahili rahisi.

"If someone is gay and he searches for the Lord and has good will, who am I to judge?" Francis asked. "We shouldn't marginalize people for this. They must be integrated into society."

Yaani anasema, "Kama mtu ni shoga na anamtafuta Bwana na ana nia njema, mimi ni nani hata nihukumu?" Papa Francis anasema na kuongeza, "Hatupaswi kutanga watu kutokana na hili suala. Inabidi wakubalike na kuchukuliwa ndani ya jamii."

kauli ya Papa Francis inaonekana kukinzana na ile ya mtangulizi wake, Papa Benedick XVI, ambaye mnamo mwaka 2005
, alisaini waraka wa kueleza kuwa wanaume wanaojihusisha na masuala ya ushoga, hawatakiwi kuwa makuhani. Kwa mujibu wa Papa Francis, mtazamo wake ni kwamba watumishi mashoga wasamehewe na dhambi zao zisahauliwe.
Hata hivyo licha ya mtazamo huo wa Papa. Bado sera ya kanisa katoliki hairuhusu masuala kama hayo, ila kutokana na kauli ya kiongozi huyo mkuu wa kanisa katoliki, huenda kukawa na mabadhiliko kwenye mtazamo wa kanisa kuhusu jambo hilo.
Chama kikubwa cha kupigania haki za mashoga nchini Marekani, Human Rights Campaign - wameonekana kufurahishwa na kauli ya Papa, na kusema kuwa, "kwa miaka kadhaa sasa tumeona mashoga na wasagaji wanaotokea Vatican wakikandamizwa, kauli ya Papa inaleta matumaini angalau." Anaeleza Rais wa chama hicho, Chad Griffin.
Katika hatua nyingine Papa Francis alizungumzia kuhusu wanawake kuwa na jukumu zaidi katika kanisa, lakini kusema kuwa bado hawawezi kuwa wachungaji/makuhani.

Papa Francis akishuka kutoka kwenye ndege mara baada ya ndege kutua kwenye uwanja wa ndege wa kivita wa Ciampinos, pembezoni mwa Rome wakati akirejea kutoka Brazil tarehe 29 Julai 2013. ©AP

Comments