Marehemu Emmanuel SK Motubatsi enzi za Uhai wake
Aliyewahi kuwa mshindani wa shindano la Cocacola pop star na mwimbaji wa kundi mahiri la Joyous Celebration la nchini Afrika ya kusini mwanakaka Emanuel SK Motubatsi amefariki dunia siku ya alhamisi kwao Pretoria, Afrika ya kusini huku chanzo cha kifo chake bado hakijaelezwa ingawa kwa mujibu wa jumbe mbalimbali zilizotumwa kwenye ukurasa wake wa Facebook inaonyesha mwanamzuki huyo amekatisha uhai wake kwa kujiua, ushahidi unaotokana na ujumbe uliowekwa na mwimbaji mwingine wa zamani wa Joyous mwanadada Tebello Sukwene, pamoja na watuma ujumbe wengine.
Emanuel atakumbukwa kwenye kundi la Joyous ambako ameshiriki katika album ya 10 na 11 akitambulishwa zaidi kwa wimbo wa "You raised me up" na Sefefo sa moya" alizoimba akiwa na kundi hilo, huku kitambulisho chake ilikuwa nywele zake fupi alizokuwa ameweka rangi nyeupe. Moja kati ya sifa zake alikuwa na sauti nzuri sana iliyomfanya akaishia nafasi ya tatu kwenye mashindano ya Cocacola pop star mwaka 2003 kisha akaamua kujiunga na kundi la Joyous Celebration baada ya muda. Lakini pia marehemu alikuwa na uwezo mkubwa wa upigaji kinanda na vyombo vingine bila kusahau uimbaji.
Source: Gospel Kitaa
Comments