RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HATIMAE JACKLINE WOLPER AFUNGUKA BAADA YA KUBADILI DINI KWA MARA YA PILI..



Hatimaye mwanadada Jacqueline Wolper ameamua kuweka wazi kilichotokea mpaka kuamua kubadili Dini yake ya Uislamu na kurudi kwenye ukristo tena. Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii mwanadada huyu wa bongo movies ametoa ujumbe ufuatao kwa mashabiki wake.
“…mambo mashabiki zangu.sikua na njia nyingne yakulikwepa hili nanaamini kua kwa wale mashabk zangu waislam amtomaind maana akuna mtu wakumsikiliza chin ya hanga zaidi yawazazi so imenipasa kurudi kanisani kwakauli yawazazi wangu.naamin kama aujaolewa ata uwe na miaka mingap bado unatakiwa kua chin ya imaya ya wazazi ata ukifa ujue unazikwaje na mimi ni binadam sijui saa wala dakika.muhm nikuwajuza nakuwaelewesha mashabk zangu stak maswal nawapenda wote…”
Hapo awali iliripotiwa kuwa mwanadada huyu ameamua kuwa mkristo tena baada ya penzi lake lililosababisha abadili dini na kuwa muislamu na jamaa aitwaye 'Dallas' kuvunjika hivi karibuni.
Swali ni je, atabadili dini tena akitokea mwingine wa dini aliyo tofauti na sasa?

STAA anayefanya vyema katika tasnia ya filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ameamua kurudi katika imani yake ya awali ya Kikristo ikiwa ni miezi michache tangu alipotangaza kubadili dini na kuwa Muislamu.
Novemba 3, mwaka huu (Jumapili iliyopita) paparazi wetu alimnasa Wolper katika Kanisa la KKKT lililopo Kijitonyama jijini Dar, akisali sambamba na waumini wa kanisa hilo.

Bila ya kificho, Wolper ambaye alipokuwa Muislamu alikuwa akitumia jina la Ilham alisimama na kujitambulisha kama muumini mpya wakati mchungaji wa kanisa hilo alipowataka waumini wapya kufanya hivyo.
Wolper akiwa katika ibada kanisani hapo. Wakati ibada hiyo ikiendelea, Wolper alionekana kuimba pambio kwa hisia kali na ibada ilipoisha, alitoka kanisani huku mkononi mwake akiwa ameshika Biblia.

Wolper (kulia) akiwa na muumini mwenzake nje ya kanisa. Nje ya kanisa hilo, Wolper alionekana akiongea na wazee wa kanisa pamoja na baadhi ya waumini ambapo wote walimkaribisha kwa furaha.


Jacqueline Wolper akiwa katika vazi la Kiislamu wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan mwaka jana. Paparazi wetu alimfuata Wolper na kumuuliza kilichomfanya arudi kwenye dini yake ya awali, naye alisema kwamba amefanya hivyo kutokana na msukumo wa wazazi wake ambao kwa muda mrefu walikuwa wakipinga kitendo chake cha kuwa Muislamu.
“Nimeamua kuurudia Ukristo kwa kuwa wazazi wangu kwa muda mrefu walikataa mimi kuwa Muislamu, kwa hiyo kuanzia sasa siyo Ilham tena, niite Jacqueline kama zamani,” alisema Wolper.

Mwaka jana, Wolper alibadili dini na kuwa Muislamu kutokana na kuwa na uhusiano na Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
Dallas akiwa nje ya nchi akamtaka Wolper kubadili dini ili akirudi wafunge ndoa ya Kiislamu, Wolper alikubali na kufanya hivyo katika Msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni jijini Dar na kuchagua jina la Ilham.

Gari aina ya BMW X6 alilonunuliwa Wolper na Dallas baada ya kuwa muislamu. Dallas alirudi nchini lakini wawili hao hawakufunga ndoa bali penzi lao likaingia doa na kumwagana, Wolper akaendelea na msimamo wa imani yake hiyo mpya na mara kwa mara alikuwa akidai kwamba hataiacha dini hiyo pamoja na kumwagana na Dallas.

Comments