RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MALKIA WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA ROSE MUHANDO KUFANYA TAMASHA LA SHUKRANI MBELE ZA MUNGU na KUWEKA WAKFU DVD YAKE YA “ANACHEKA”-DAR

Tumeona matamasha lakini hili litakuwa funga mwaka. Kama mnavyomjua malkia wa Gospel Tanzania, Muhando huwa ahakosei kabisa katika kufanya kazi ya Mungu.  Utaweza kuona nguvu ya Mungu ikishuka kwa kupitia uimbaji wa dada huyu ambaye amejitoa kufanya kazi ya Mungu.

Mnakaribishwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyote kuona kazi ya Mungu ikifanyika kwa kupitia mtumishi huyu wa Mungu. Nyimbo zake zimejaa mafundisho tosha kwa kila anayesikiliza nyimbo zake. Ukifika utahudumiwa na kiroho chako cha imani kitainuliwa siku hiyo.
 
Tamasha litafanyika katika kanisa la Lutherani Mabibo External, Siku ya Jumapili 24/11/2013 kuanzia saa 8:00 mchana.
 
Waimbaji watakuosindikiza upako wa Rose Muhando ni Mheshimiwa Martha Mlata, Edson Mwasabwite, Addo Novemba, Stara Thomas, Stella Joel, Debora Said, Faraja Ntaboba, John Shabani, Tumaini Njole, Kwaya ya Vijana KKKT Mabibo Externa, Unit Family, DP,

HAKUNA KIINGILIO NA WOTE MNAKARIBISHWA

Comments