RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UNANICHOSHA NA VITUKO VYAKO KANISANI

Kuwa hivyo ndugu yangu...kwa kweli sio vizuri kuonekana unahudhuria sana kanisani lakini ukiwa katika nyumba ya ibada unafanya vituko. Mungu hapendi kukuona ukifanya vituko na hapendezwi sana na tabia hiyo. Ni mbaya tena mbaya sana mbele za Mungu.

Utakuta mtu wakati wa kuomba na kumtukuza Mungu anaanza kuchart na watu katika simu na wengine wanaanza kukodolea macho kwa watu wengine wakitazama wanasalije. Wewe umeenda kanisani kufanya nini? Fuata kile ambacho umekiendea na sio kufika kanisani na kuanza kufanya vitu ambavyo haviendani na ibada. Mtu mwingine anafika kanisani na kuanza kusinzia, jamani hii ni tabi nzuri kweli. Unatakiwa kufanyiwa maombi sana wewe unasinzia kanisani. Ogopa sana kusinzia kanisani kwani shetani anapenda sana kukuona wewe unasinzia ile usisikie kile Mungu anaema juu yako kwa kupitia watumishi wake.

Kuna tabia mbaya sana wakati wa sifa utakuta watu badala ya kumuimbia Mungu kwa kumaanisha, wao utakuta sura zao na vitendo vyao haviendani na vile wanaviimba. Utakuta mtu wakati wa sifa yeye anaanza kujitazama na wengine kujiangalia katika vioo kama wamependeza. Wakati wa kupiga makofi utaona walio wengi hata makofi yao hayasikiki, wanapiga kwa mapozi. Jamnai tunapokuwa katika eneo lolote fanya jambo kwa asilimia zote na sio kufanya kwa ku-beep.

Kulia ni Rulea Sanga akiwa SCOAN kwa Nabii TB Jishua siku ya Ijumaa Mkesha 2012

Kumetokea tabi ya kuwasema watumishi wa Mungu wanapokuwa madhabahuni wakihubiri, utakuta mtu anamjadili mtumishi wake alivyovaa au anavyohubiri. Watu hawa wamekuwa watu wa kuzungumzia vitu negative kwa watumishi wa Mungu. Kuna akina dada wamekuwa wakirembua macho yao wakati watumishi wa Mungu wakihubiri, na hii imekuwa ikiwadondosha watumishi wengi na kujikuta wanaingia katika masuala ya ngono. Inaumiza sana kuona mtumishi amedondoka kihuduma eti kwa sababu ya mwanamke kumfanyia vituko ili afanye naye twendo la ndoa. Ipo siku wewe unayewadondosha watumishi wa Mungu utalia na kusaga meno tena hapa hapa duniani.

Mimi niishie hapa kwa leo.

UBARIKIWE SANA
Rulea Sanga



Comments