RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UNAPANIKI NINI WEWE...??? ACHA HIZO...!!! KIBOKO YETU YUPO....!!!

Na Rulea Sanga

Acha kupaniki mtu wa Mungu. Unapopitia Magumu jikaze kiume na mtazame mwenyezi Mungu. Acha kupaniki na kuona hilo jaribu ndio mwisho wako wa kuishi hapa duniani. Ishi katika IAMNI mtu wa Mungu. Kitu kidogo tu unapaniki na kujiona wewe huwezi. Kila kitu kinawezekana chini ya jua, ishi katika IMANI na pia futa ya jana na kazania ya sasa huku ukiangalia ya mbele. Macho yako yaangalie mbele na acha pa iangalie chini...Songa mbele mwana wa Mungu
Devil anafurahi sana anapoona wewe unaanza kupanikia au kujishtukia unapojaribiwa, anacheka sana na kukuona wewe ni mpumbavu na mjinga sana. Kumbuka devil anamuogopa sana Mungu na anajua wewe ni mwana wa Mungu na inampasa kukuogopa kama anavyomuogopa Mungu, sasa anapoona mtu mwenyewe kiwewe unatetemeka anapokutisha......yeye anafurahi na kujiona ni mshindi.

Kaza buti dada yangu na kaka yangu, hakuna kitu cha kukutisha hapa duniani. Ulizaliwa peke yako na utakufa peke yako. Kuwa na msimamo kwa kila jambo, usiteteleke na kutishwa na wenye nguvu. Waliokuzidi kiuchumi au kielimu au kwa namna yoyote wasikutisha na walivyonanvyo. Unatakiwa kujivunia kwani unaye Mungu awezaye yote.

Acha kusikia mamneno ya watu, kwani hawatamani kukuona hapo ulipo, wanatamani kukushusha. Kaza buti mtu wangu, kwani juhudi zako ndizo zitakazokutoa ulipo. Acha kubabaishwa na washikaji au ndugu wasiopenda maendeleo.

Tafuta marafiki wanaokuwezesha pale unapohitaji kuwezeshwa kwani hao wanamapenzi na wewe. Kuna washikaji wengine wanakuja na maneno ya kuvunja moyo hasa pale unapotaka kupata ushauri juu ya jambo unalofikiri litakuinua kiuchumi. Ukiona mshikaji anakuambia maneno ya kukuvunja moyo mpige chini na umuombee ili kesho anapokuja kwako akupe mawazo ya kukuinua na sio kukatisha tamaa. Ukiona anazidi kukupa story za kukurudisha nyuma, mpe LIVE hapo hapo mwambie mshikaji mbona hunitii moyo bali unaniyeyusha.

Watu wa Mungu huu ni wakati wetu wa kuwa shujaa kimwili na kiroho. Tunatakiwa kutupilia mbali woga wa kujiona hatuwezi. Wewe kama unachoma mkaa piga uwa galagaza....chomoka katika hali hiyo na utamani kuuza majiko ya gesi na sio mkaa tena. Unapoamka asubuhi hakiksha unamuomba Mungu akusaidie siku ianze na baraka na Mungu akupe marafiki wenye kutamani wewe uwe na maendeleo.

Unapoona mwenzako anakuja kwako anahitaji msaada wa mawazo, mpe na usibanie kwani kufanya hivo utamuwezesha afanikiwe katika maisha yake, ana akifanikiwa atakukumbuka siku ya uzee wako. Acha tabia ya kubaniana...huo ni uchoyo na Mungu hapendi. Unaweza ukawa huna pesa ya kumsaidia mwenzako lakini ukawa wazo la kumsaidia apate pesa.

Wewe dada yangu ambaye hujaolewa na wewe kaka yangu ambaye hujaoa kama mimi, usi-panic unapoona namba za miaka zinasona ninachojua mimi ni kwamba kila jambo mbele za Mungu linamakusudi yake. Ila sikushauri hata kidogo kutooa au kuolewa wakati mwenyewe unasukumwa na Roho wa Mungu kuolewa au kuoa, ukifanya hivyo, ninakuambia utachemsha mno. Mungu anapokukuambia sasa olewa au oa, please tii roho wa Mungu. Ila usi-panic unapoona mchumba humpati.

Watumshi wa Mungu wanapokutamkia maneno magumu ya kuvunja moyo, wewe kaza buti na songa mbele, waache na maneno yao, kwani siku ya mwisho wataulizwa na Mungu juu ya maneno yao. Unapoona mtumishi wa Mungu kakusema aul kukutukana wewe fuarahi na ikiwezekana kama una roho ile ya kishujaa, nenda shop na umnunulie zawadi nzuri sana na umpe, ninakuambia ukifanya hivyo utaona kama atarudia kufanya hivyo kwako. Watumishi wa Mungu sasa tumezidi sana kuwakatisha tamaa na kuwasema waumini wetu. Tuache hiyo tabia ni mbaya sana.

Utakua mtu kaa peke yake anasononeka kama vile kafiwa au kaambiwa ana masaa machache ya kunyongwa...weweeeee acha hizo yupo mwokozi wetu Yesu Kristo, mwanandamu asikupe taabu wala kukubabaisha. Kuna wakati mwingi unaishi katika nyumba za kupanga kama mimi na inafika kipindi cha kulipa kodi huna mshiko, ukitazama huku na kule huna msaada, na pengine huna wazazi yaani YATIMA kama mimi...Ukicheki washikaji nao wamepigika kama wewe..ukicheki ndugu wanajifanya kama hawakujui vile, ukichomekea kuwapiga mzinga wanachomoa...Ninakumabia ndugu yangu wa kumpiga mzinga ni Yesu tu. Ila kuna taratibu za kumpiga mzinga Yesu, fuata taratibu zake na kanuni zake, kama hutafanya hivyo atakutosa tu. Utajiuliza kanuni gani hizo?  Kuna kitabu kinaitwa BIBLIA na ndani ya hiyo BIBLIA kuna taratibu zake za kufanya, ninakuambia ukifanya hivyo utaona wandazi kutoka kwa GOD....!!!!

Acha tabia ya kuwa ombaomba, utadharaulika na kuonekana huweza lolote mbele za rafiki zako au mke wako, acha kuwa tegemezi..chomoko nenda mitaani, fanya kazi bila kuona aibu, usiwe mtu wa kuchagua kazi, piaga kazi mwanaume...HESHIMA YA MTU NI KUONEKANA UNA KAZI HATA KAMA HAINA KIPATO CHA KUTOSHA...Jibidiishe mwanaume.

Kama mimi ninakuzingua poa ila ninakupa mchomoko. Wewe kama unaongoza kondoo wa Mungu, wasaidie hwa watu wafike mbingu na pia wafundishe jinsi gani ya kupata mshiko ili waweze kukmtolea Mungu hapo kanisani kwako. Acha kuwaambia POKEEEEEAAAAAA...!!! bila kuwapa mbinu za kupokea. Utakuta jitu linamzigo wa madhambi, bila ya jitu hilo kuliungamisha dhambi unabaki kusema POKEEEEA SAFARI ZA ULAYA...Jamani mbona mnatuonea sana nyinyi watumishi wa MUNGU.  Poa tu ngoja tukomae wenyewe kumtafuta huyu YES, ipo siku tutatoka na sisi tutaanza ksema POKEEAAAA. Ila binafsi lazima niwape watu njia sahihi ya kupata muujiza wao na sio TOA NDUGU.... TOA NDUGU ULICHONACHO WEWE, BWANA ANAKUONA MPAKA MOYONI MWAKO....Ahhaaaaa jamani tumechoka..

Rafiki yangu ninaomba sasa uchukue BIBLE na usome kuna jambo utapokea kwa kusoma kwako, Mungu atakupa maarifa...

Poa baadae...

Comments

Mama watatu said…
Amen kaka yangu', asanteee unatia moyo sana . Barikiwaaa