RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WAZIRI MKUU TANZANIZ MH. PINDA KUWA MGENI RASMI KATIKA KUSHEREKEA MIAKA 7 YA UREJESHO KANISA LA RGC TABATA CHANG'OMBE



Mheshimiwa Pinda takuwa mgeni rasmi katika siku hii ya kipekee kwa waumini wa kanisa la RGC Tabata Chang'ombe kwa Mtume Peter Nyaga. Siku hiyo kutakuwa na ugawaji wa vyakula kwa wajane, yatima na walemavu. Kanisa hili linasherekea kutimiza miaka saba tangia limeanza hapa nchini Tanzania. Askofu Arthur Kitoga wa Kenya atakuwepo siku hiyo. Kumbuka ya kuwa Askofu Kitonga ni mwanzilishi wa maknisa la Redeemed duniani likiwemo hili la RGC Tabata chini ya Mtume wa Mungu Peter Nyaga


Mtume Peter Nyaga akiongea na Rumafrica alimshukuru sana Mungu kwa kumfanikisha kupata chakula hiki kwaajili ya hawa ndugu zetu wenye uhitaji. Mtume Peter Nyaga amewaomba Watanzania wenye kuguswa na hawa yatima, walemavu na wajane wafike siku hiyo ili waweze kuwasaidia kwa michango yao yoyote ilie watakayokuwa nayo siku hiyo

Sherehe hizi zitapambwa na bendelea kama hiyo hapo chini kwa kusudi la kumuinua Yesu Kristo. Kutakuwa na waimbaji mbalimbali na hakutakuwa na kiingilio chochote. Walete Yatima, Walemavu na Wajane ili Mungu aongee nao siku hiyo ya tarehe 7/12/2013 katika kanisa la RGC Tabata Cjhang'ombe jijini Dar es Salaam


Pia kutakuwa na uzinduzi wa vitabu na DVD mbalimbali vya Mtume Peter Nyaga zilizotenenezwa na RUMAFRICA (+255 715 851523). DVD na Vitabu vitauzwa kwa Tshs 5000 tu.

VITABU VITAKAVYOPATIKANA SIKU HIYO NA SIKU ZIJAZO











 
Design imefanywa na RUMAFRICA +255 715 851523



Comments