RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HABARI ZINATOKA GOSPEL KITAA JUU YA MKESHA WA KUMALIZA MWAKA KATIKA KANISA LA WORD ALIVE SINZA MORI SIKU YA JANA

Kabla ya yote..Ninakushukuru sana Gospel Kitaa n crew yako kwa picha zako ambazo zitafanya baraka watu. Mungu azidi kulinda huduma yako hii. Picha zako zitadumu milele na Mungu atakwenda kufanya jambo katika maisha yako kwa kupitia kazi ya mikono yako. Amen
-----------------------------------------
Wengi huwa na mkesha wa kumaliza mwaka tarehe 31 Disemba kuamkia mosi Januari mwaka mpya, ila kwa Word Alive Center iko tofauti, kwani wao humaliza mwaka wiki moja kabla, na hapa ni ibada ya mkesha wa kumaliza mwaka kama ilivyofanyika usiku wa kuamkia leo, ambapo Mchungaji kiongozi, Deo Lubala alihubiri alielezea namba 12 kuwa namba ya kiuongozi, na kisha kutoa neno la kinabii wka mwaka 2014 kuwa mwaka wa kibali maradufu.

Tazama picha kama ambavyo mkesha huo ulikuwa, video zake zitakujia kama kawaida kupitia ukurasa wetu wa youtube.

Blogger Rulea ndani ya nyumba

Mchungaji Kiongozi, Deo Lubala akisifu pamoja na umati.





Angel Bernard akiongoza ibada ya kumuabudu Mungu



Aaaaaaaaameeeeeeeeen 



Pastor Billionare jukwaani akisalimu watu.









Jesca wa Boniphace akiwajibika madhabahuni




Sasa ni saa ya kumpokea Yesu kama BWANA na mwokozi wa maisha yetu.

DPC Rivers of Life wakifanya mambo yao.




Praise team ikichangamnsa umma.

Te Amo...

Pilipili haiwashi...

...pilipili inachekesha, mwe.



Living Waters jukwaani





Karibu Word Alive Center, Sinza.


Comments