RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NABII FLORA SIKU YA ALHAMISI 19.12.2013 ALIHUBIRI JUU YA NDOA, KUFANIKIWA, KUTEMWA KUTOKA TUMBO LA NYANGUMI, MAOMBI YA UPONYAJI NA MIUJIZA YALIFANYIKA

SALAMU
Ninawapenda kwa jina la Yesu Kristo na kwa damu ya Yesu Kristo. Ninawakaribisha wote mnayenitazama kwenye youtube, facebook na kunisoma katika blogu yetu ma ninyi mnayenitazama hapa kanisani LIVE ninawakaribisha mahali hapa.


SIKU AMBAYO MUNGU ALIMVIKA KIATU NABII
Nina kila sababu ya kumuinua Mungu katika siku hii ya nne ya uumbaji ambayo Mungu aliweza kumvika kiatu na koto Nabii. Ninajua ni siku ya kuvikwa utukufu.


MOMBI
Kabla sijafanya chochote ningelipena niombe, ninakuomba uinue mikono yako. “Baba Mtakatifu na Mungu wetu utendae mambo makuu nay a ajabu. Nalitukuza jina lako wakati huu. Ninasema asante Baba kwaajili ya watoto wako na kuachilia watumishi wako wake kwa waume ambao Mungu wameingiia hekaluni mwako.

Ninaachilia nguvu yalko Baba, ninawavika mavazi ya utukufu, ninavua vazi la laana, ninav9ua vazi la magonjwa, mateso, ninakwenda kuachilia nguvu ya UPAKO. Baba ninaachilia upako kwa watu hawa, ninaomba nguvu ya Yesu kutembea sasa..Pokeeeeaaaaa neema!!!

Baba gusa mama, kaka, kijana, mtoto Yule katika kazi zake. Baba onekana juu ya mabinti, akina mama, wababa. Kwa masaada wa Mungu ninakufungua mahali ulipofungwa.

Ipo nguvu ya Mungu mahalihapa. Ninaona mkono wa Mungu ukikugusa sasa..Pokeeeaaa kwa jina la Yesu Kristo. Baba tunajua ulinyang’anya sheatani funguo za mamlaka. Nami nampokonya shetani funguo za kuzimu na mauti. Shetani achia katika viwanja hivi, mauti hauna mamlaka, roho za kuzimu na mauti ninakufunga hapa hupati kitu, hakuna atakayekufa hapa.

Ninaachilia nguvu, ninaachilia nguvu, ninaachilia Neema kwako, pokea sasa na Bwana akutendee. Ninasema inuliwa siku ya leo, na Bwana atende kwako, Yesu akuinue asubuhi ya leo. Pokea Baraka kwa jina la Yesu Kristo.

NABII AELEZA ALICHOKIONA WAKATI MTUMISHI WA MUNGU OCTAVIAN AKIFUNDISHA NENO LA MUNGU.
Kipindi mtumishi wa Mungu alipokuwa akifundisha sisi Neno la Mungu, niliona utukufu wa Mungu wa ajabu mahali hapa, niliona ndegi mmoja ishara ya TAI alikuwa amechanua kabisa mabawa yake. Bwana akanambia watu wangu nitawainua katika mbawa za tai.Bwana anakwenda kukuinua katika mawio ya jua, adui yako hatakuona wala hatakupata.

NENO LA MUNGU
WIKI YA UPONYAKJI NA KUBARIKIWA
Tutasoma katika kitabu cha Yeremia 33:1-9. Tena jina la Bwana likamjia Yeremia kwa mara ya pili hapoa alipokuwa alikuwa amefungwa katika uwanda wa walinzi akasema Bwana utendae jambo hili na uumbae jambo hili lipate kuthibitika kwake. Yamkini hata wewe uko hapa maisha yako yamefungwa, uchumi wako umefungwa, mambo yako hayaendi, umefungwa na shetani lakini leo unakwenda kufunguliwa kwa jina la Yesu Kristo. Bwana anasema na wewe leo yeye alifanyae jambo hili na aliumbae lipate kuthibitika kwake. Tumeumba mwaka huu vitu vingi sana na tumekutamkia mambo mengi sana, tumetamka kufanikiwa, tumefanya hivyo ili lipate kuumbika kwako

Biblia inaendelea kusema, Bwana alitendalo jambo hili na aliumbae ili apate kuthibitisha. Bwana ndiye jina lake asema hivi, Niite nami nitakuitikia nikuonyeshe mamabo makubwa. Maana Bwana wa majeshi asema hivi, katika habari za nyumba za mji huu na katika habari za nyumba ya mfalme Yuda zilizobomolewa ili kuyapiga maoboma upanga, watakuja kupigana Wakalidayo,  Nawe mwite Bwana asubuhi ya leo naye anakwenda kukuitikia. Mwite juu ya magumu yako, matatizo yako, shida yako, na Bwana anakwenda kukuitikia mwezi huu adari maana mbiingu zimesogezwa mno.

Bwana anakwenda kukuonyesha mambo makubwa na magumu ambayo wewe huwezi kuyajua. Hebu mwite Bwana katika mwezi huu adari, siku hii ya nne ya uumbaji. Pamoja na hayo matatizo yatakayokupata, nitauficha mji huu uso wangu Una tatizo gani linakusumbua na halija kaa vizuri? Bwana anakwenda kusawazisha maisha yako sasa!!

Mtakutana na watu wasiomjua Mungu nao watapiga kama hautakuwa na Mungu ndani yako. Bwana anasema atakwenda kuficha uso wake juu ya watu wanaoharibu maisha yako, wamekuchawia, wameharibu duka lako, wameharibu ndoa yako, Bwana anasema ataficha uso wake na kuwafumbia macho yake.

Bwana anasema, Tazama nitakuletea afya na kupona. Hii ni wiki uponyaji na Bwana ataleta afya yako kwako, wala wanakusumbua kwa uchawi, madeni, waliokuchukulia kiwanja chako, wamemega shamba lako. Watu hawa watamuomba Mungu na Mungu hatawakubali.

Kuna ndugu zetu waliofungwa na Bwana anakwenda kuwarudisha. Kama kuna ndugu yako amefungwa katika Roho na katika mwili anakwenda kufunguliwa. Maana Bwana anasema nitwarudisha wafungwa wa Yuda. Hata kama uchumi wako umebomolewa Bwana anakwenda kurudisha kama mwanzo.

Mara ya kwanza ulikuwa unachumbiwa na kupendwa kila saa na sasa hupendi tena, Bwana anasema anakwenda kurudisha upendo huo kama mwanzo, na hautapata misukosuko kamwe, Yesu atakwenda kuleta amani kwako. Hajalishi umepimwa na madaktari na ukaambiwa una mauti, ninasema usiogope mauti, wamekuambia CD4 zimeshuka wewe sema za kwangu zimepanda na waambie Yesu alipokuwa msalabani alisema yote yamekwisha. Bwana ahakusema UKIMWI, kansa itabaki kwako bali alisema yote yamekwisha.

Yamkini mama umefungwa katika ndoa yako na sasa hupendwi tena, hata ukivaa vizuri mumeo anakuona kama umevaa matambala, hata kama umevaa nguo zinazoendana na shape yako lakini anakuona kama umevaa nguo za kizee, hata kama unajipodoa sana yeye anaona sura yako ina mabonde. Lakini Bwana anasema anakwenda kukujenaga kama kwanza.

Watu wengi shetani kaiba mafanikio ya watu, shetani kaiba sura za wanandoa mpaka unatamani kuachana na maswala ya  ndoa ili uishi peke yako kwani ndani ya ndoa kumechafuliwa na shetani. Mungu ankwenda kufanya jambo siku ya leo..UBARIKIWE SANA

Somo liliendelea…

Tembelea
www.rumaafrica.blogspot.com
Jinsi ya kufika. Panda magari ya Tegeta kama umetokea Mwenge, shuka Mbezi Mbuyuni, uliza kanisa la nabii Flora la Huduma ya maombezi na Uponyaji utaonyeshwa. Tupo barabarani kabisa.

Wasiliana na Nabii Flora kwa simu +255 657442699
Octavian +255 716310661

Mwandishi
RUMAFRICA
www.rumaafrica.blogspot.com
+255 715851523




Comments