RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SHUHUDA ZENYE KUINUA IMANI YAKO NA KUMTUKUZA MUNGU...MUNGU AZIDI KUMTUMIA MTUMISHI WAKE NABII FLORA PETER

Mwandishi na Picha: RUMAFRICA
..........

MAMA GLORY AMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA MWANAE UPOFU NA KUPOOZA KWA MUDA WA MIAKA KUMI NA NNE
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Diana au mama Glory; namshukuru Mungu wa Nabii Flora kwa makuu aliyonitendea, naomba mama pokea hiki kidogo nilichokipata. Najua ni makubwa sana aliyonifanyia kwa mwanagu, mwanangu alikuwa haoni toka amezaliwa mpaka amefikisha miaka kumi na nne, na alikuwa amepooza upande mmoja. Siku ya tatu nilipohudhuria katika madhababhu hii ya Nabii Flora aliweza kufunguliwa siku hiyohiyo, upofu uliisha na kule kupooza kote kuliondoka. Sasa hivi nikitembea naye simshikilii anaona na anatembea mwenyewe, kwa leo sikuweza kuja naye ameniambia amechoka, namshukuru Mungu sana, sasa hivi naweza kumuacha nyumbani peke yake.

ESTERB SHOO AMSHUKURU MUNGU KWA KUWEZA KUJENGA NYUMBA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Esta Shoo; namshukuru Mungu wa Nabii Flora amenitendea mambo makubwa sana, nimeweza kujenga nyumba ya room tano na inafensi na kila kitu. Namshukuru Mungu wa Nabii Flora kwa kunipigania na maadui zangu, nilikuwa siwezi kushika pesa mkononi, lakini baada ya kuniombea, sasa hivi pesa ninashika na ninaweza kufanya kitu chochote. Namshukuru Mungu wa Nabii Flora sana, naomba Mungu azidi kumuinua.

JOHN MATERU AMSHUKURU MUNGU KWA KUREJESHEWA PESA ZAKE ZILIZOKUWA ZIMEIBIWA Bwana Yesu asifiwe, naitwa John Materu; namshukuru Mungu wa madhabahu hii ya Nabii Flora, kwa kweli amenitendea mambo mengi sana. Juzi nilikuwa naenda kununua vifaa vya kazini, nikawa nimeinama nashuka kwenye pikipiki, nashangaa watoto wanaokota pesa zangu zote zilizokuwa mfukoni, mmoja akaziweka kwenye mfuko, akaniambia wanataka kugawana lakini nikawaambia hapana. Nikamwambia nashukuru sana na nikatoa asante kwake yeye, na hapa namshukuru Mungu wa Nabii Flora, kwa kunitendea mengi ya kuweza kurudisha hizo pesa.

EMMILIANA JOSEPH AMSHUKURU KWA KUMWEZESHA KUPATA MIMBA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Emmiliana Joseph; niliingia hapa toka mwaka jana mwezi wa kumi na mbili, nilikuwa na matatizo ya ufukara. Baada ya kukutana na mtumishi wa Mungu Nabii Flora kitu cha kwanza nilibadilisha maisha, nikapata pesa. Na baada ya hapo nikamwambia mtumishi wa Mungu Nabii Flora, ninamiaka Sita ndani ya ndoa sina mtoto, akaniambia mwanangu utakwenda kupata mtoto, baadaye nikapokea ujauzito bila mimi kujijua. Mume wangu sasa akawa anaumwa ule ujauzito ukawa unamsumbua yeye, baada ya kuingia hapa Nabii akamwambia mwanaume unaumwa mimba, wacha mke abebe mimba wewe fanya kazi. Na mimi nilipofika hapa sikumweleza kitu chochote Nabii akaanza kunitabiria, baada ya kunitabiria akanipa siku, akaniambia baada ya wiki mbili uende kucheki, kwenda kucheki ikawa haionyeshi. Lakini nikafanya kliniki na Nabii, nikaja kwa Nabii akawa ananiwekea mkono anaomba mimi namwambia Mungu asante, hata kama huko wamesema hakuna kitu lakini Mungu wa Nabii, ametenda maajabu, waliokufa wamefufuka itakuwa mimi. Nikasema cha kwangu kipo, wewe Daktari macho yako kipofu, nikaendelea kufanya kliniki mimi na Nabii. Baada ya miezi minne nikaja hapa, nikamwambia mama nahitaji kuanza kliniki, naomba uniombee , na kweli nilivyoenda kliniki mimba ikaonekana, namshukuru Mungu wa Nabii Flora. Napenda kuwaambia waumini mnao hudhuria mahali hapa, hata mimi nilipotokea nilikuwa mkatoliki tena kiongozi wa wamama, nilipokuja hapa niliingia mguu nje mguu ndani, ujauzito wa kwanza ukatoka, lakini baada ya kuacha vyote na kuja moja kwa moja, nimepata ujauzito, namshukuru sana Mungu.

MAMA ANATOA SHUKRANI KWA MUNGU WA NABII FLORA KWA MATENDO MAKUU ALIYOTENDEWA BAADA YA KUNUNUA STICKER YA NABII FLORA
Bwana Yesu asifiwe; mimi ninatoa ushuhuda kuhusu hizi sticker zinazotolewa hapa Kanisani, ilikuwa siku ya Ijumaa usiku mimi na mtoto ambaye anaugonjwa wa Sickless cell, na kutokana na ugonjwa wake mfupa wa nyonga ulikuwa umelika, kwa hiyo anapata shida ya kukaa, kusimama na kutembea. Kwa hiyo Ijumaa usiku nikamwambia tuweke hii sticker kwenye huo mfupa tuombe, tukaomba usiku huo, tukalala ilipofika Jumamosi asubuhi yaani jana. Ghafla mtoto akapata maumivu makali sana ya tumbo, akaniambia mama nitafutie dawa, nikatafuta sikuona, nikamwambia ngoja nikuwekee hii sticker. Akaweka sticker akailalia akaomba, baada ya dakika tano akasema Mama tumbo limenyamaza, na huwa sio kawaida tumba kutulia mapema hivyo, alafu akasema miguu inauma, nikaweka tena sticker baada ya muda maumivu yakaisha. Kwa hiyo ndugu zangu wote mimi nawashuhudia kwamba, hizi sticker mzinunue zina nguvu ya ajabu, mimi zimenisaidia na ninyi zitawasaidia. Naimani Nabii atanisaidia mwanangu atapona kabisa, na mwanangu mwingine ambaye amechanganyikiwa kwa nguvu ya hizi sticker atapona.

JOYCE AMSHUKURU MUNGU KWA KUMWEZESHA KUCHUKUA MAFUNZO YAKE JESHI SALAMA, PIA MDOGO WAKE AMEJIFUNGUA SALAMA BAADA YA KUNYWA MAJI YA NABII FLORA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Joicy; namshukuru Mungu wa mahali hapa Mungu wa Nabii Flora kwa kuwa amenipigania mengi katika maisha yangu. Mwaka jana nilipata promotion ya kwenda Moshi kwenye mafunzo ya Jeshi. Nilikuja hapa nikamweleza Nabii, akaniwekea mkono, akanitabiria akaniambia hakuna baya lolote litakalokupata, na kweli ndani ya miezi sita Mungu wa Nabii Flora alinipigania kwakuwa ilikuwa ni mafunzo magumu. Kweli nilimuona Mungu wa Nabii Flora, sikuumia, sikuumwa, na daima nilikuwa nikiomba, nikimuona Nabii katika ulimwengu wa Roho, hivyo namshukuru sana Mungu wa mahali hapa. Nilivyorudi nilikuta mdogo wangu ni mjamzito, na amezaa mtoto wa kwanza, wa pili kwa matatizo, nikaja mahali hapa nikachukuwa maji, siku ya Jumanne wiki hii akawa anasikia dalili ya uchungu, nilipompeleka Hospitali, nikampa maji ya Nabii akanywa, akasema anasikia uchungu kwa mbali. Nesi akaniambia wewe muache wahi kazini, kufika tu kazini nikaambiwa ameshajifungua, kwa kweli Mungu wa mahali hapa anatenda kila siku, hivyo namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora,na sita muacha katika maisha yangu.

BATULI LENARD AMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA NA PIA WATOTO WAKE WAMEPATA KIBALI CHA KWENDA KUSOMA UGANDA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Batuli Lenard; namshukuru Mungu kwa kunishushia mteule Nabii Flora, anayempaka mafuta na kumpa kibali. Zaidi ya yote kuweza kumponya yule mjukuu ambaye pepo alikuja kwa kasi, ili aweze kumwangamiza na sisi tuteketee, lakini Bwana ametutendea. Ninapenda kumshukuru Mungu kwa ujumbe wote ambao upo mbele ya madhabahu hii, kwa kazi yake kubwa ambayo inaendelea katika madhabahu hii yenye majibu. Pia mimi nilikuwa naandamwa na magonjwa mengi, lakini baada ya kukutana na mteule wa Mungu Nabii Flora, Mungu alifanya kitu ndani yangu. Niliugua toka nikiwa darasa la tatu, hata sikusoma lakini Mungu amenipa uwezo na kipaji kikubwa, nilitembea kote hadi kwa babu Loliondo kikanywa kikombe, nikamaliza Mashekhe na Mahostadhi, bado sikupona. Lakini baada ya kuingia kwenye madhabahu hii yenye majibu, ya mteule wa Mungu aliyepewa kibali na mbingu. Nikiwa nyumbani kwangu nilimuona nyoka akishuka akaniambia bye bye, kuanzia hapo wapendwa mimi sijawahi kunywa panadol wala sijawahi kuugua Malaria. Pia Mungu wa Nabii Flora ameweza kuwainua watoto wangu, wamepata kibali cha kwenda kusoma Uganda.

DADA AMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA UJAUZITO BAADA YA KUKAA KWENYE NDOA YAKE KWA MUDA MREFU BILA KUPATA MTOTO
Bwana Yesu asifiwe, natokea hapa Salasala; Mungu amenitendea mambo makuu sana, nilikuwa katika ndoa yangu kwa muda wa miaka 3 sipati mimba, lakini baada ya kuingia katika madhabahu hii, nimeweza kupata mimba mwaka huu, namshukuru sana Mungu. Pia ninamshukuru Mungu nilikuwa sina kazi lakini sikua ya Jumatano, niliitwa kwenye interview, na nimepewa wiki mbili tu niitwe kuanza kazi, namshukuru Mungu, namshukur pia Nabii Flora.

DANIEL MBUYA AMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA MAGONJWA YAKE PIA KUFANIKIW AKUONGEA NA MTOTO WAKE WALIOPOTEZANA KWA MUDA MREFU

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Daniel Mbuya; kunarafiki yangu alinieleza mambo ambayo Nabii alimfanyia, alimponya ugonjwa wa Kisukari, akapata na kazi. Na mimi nilikuja kulikuwa na matatizo yananisumbua, kati mambo yaliyokuwa yananisumbua nimepata majibu, sasa nimepata tiba, ugonjwa uliokuwa unanisumbua kwa muda wa miaka 25. Kutokana na ugonjwa uliokuwa unanisumbua toka mwaka 1994 sikuweza kuganya kazi, kwa hiyo huo ugonjwa sasa umetoka na ninajisikia hamu ya kufanya kazi. Na pili toka mwaka 2003 kuna mtoto aliondoka nyumbani, huyo mtoto akawa awasiliani na mtu yoyote nyumbani. Nilimueleza Nabii akaniambia usiwe na wasiwasi huyo mtoto atapatikana, jana amenipigia simu saa nne usiku, akaniambia yupo salama. Lakini mwaka jana alipata ajali, ni mguu tu unamatatizo kidogo, na amepata mchumba anaishi naye na sasa wana mtoto mmoja. Namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora na ni Mungu wangu pia.

MWINJILISTI NEEMA AMSHUKURU MUNGU KWA MATENDO MAKUU ALIYOMTENDEA KUJENGA NA UCHUMI WAKE KUONGEZEKA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Mwinjilisti Neema; namshukuru Mungu wa Nabii Flora, kwa jina lingine namuita Mama yangu mshauri, yaani sina cha kumrudishia Nabii Flora Mama yangu, amenitengeneza kiroho. Kwanza nilivyokuja sivyo kama nilivyokuja sasa hivi, namshukuru Mungu wa Nabii Flora, pale nilipokosea ameweza kunirekebisha. Na ameweza Mungu wa Nabii Flora kunitengeneza, nimekuwa tofauti na nilivyokuja, na ninajitahidi kumuomba Mungu wa Nabii Flora aendelee kunibadilisha. Na ninaona baraka zinakuja, nipo tofauti na nilivyokuwa, milango ilifungwa lakini ninaona baraka zinafunguka kila iitwapo leo. Tarehe 20 nilitaka kutolewa vyombo vyangu nje, siku mbili zilizopita kabla ya tarehe 20, nilikuja hapa kumwambia Mama, sina kodi ya nyumba na sijui ni kwa nini nakosa. Nikashangaa kushinda tu siku moja kabla tarehe ile haijafika nikapata kodi ya nyumba, nilitumiwa pesa na Mama bila kutegemea, alinipigia simu akaniambia Neema nataka nikutumie nauli uje huku. Nikamwamba Mama sina kodi ya nyumba naomba unitumie alafu nitajipanga upya nije kukusalimia, namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora. Pia amemponya mtoto wangu alikuwa ana alage mwili mzima vidonda visivyopona kwa muda wa miaka 5, pia alidondoka akatenguka mkono, nilipomleta hapa Nabii akamshika tu ule mkono ukapona. Pia mimi aliniponya nilikuwa na uvimbe sehemu za siri, Nabii aliniombea tu kwenye simu lakini ule uvimbe ulipasuka.

JINSI YA KUFIKA
Panda Magari ya Tegeta kama umetokea Mwenge, shuka Mbezi Mbuyuni, uliza kanisa la Nabii Flora.|
Tembelea
Blogu: www.nabiiflora.blogspot.com
Facebook: Nabii Flora Peter
Picha zimepigwa na RUMAFRICA

Comments