RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UJUMBE HUU UNAKUHUSU KABISA..NI IBADA ILIYOFANYIKA KATIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASALA KWA NABII FORA PETER SIKU YA JUMAPILI 22.12.2013

Nakusalimu kwa jina la Bwana, nakukaribisha katika wakati mzuri wa neno la Mungu, nakukaribisha katika ibada hii iliyojaa upako na utukufu. Katika wakati huu wa Bwana kukutendea, katika mwezi huu Adari, ambao Bwana alifanya mapinduzi, akapindua mawazo ya Hamani akajitwalia ushindi Modekai, na akawa na sifa na sifa zake zikavuma sana.

Akawa na ukuu tena ule ukuu sana, nataka upate ukuu juu ya mali zako, nataka sifa zako zivume zidi yao, waambie Bwana amekwisha kunitangulia Galilaya. Bwana amekwisha kuvuka amewatangulia tayari, yaani maadui zako umekwisha kuwatangulia mbele. Nakutakia baraka lazima uongozwe na mtumishi aliyevuka.

NENO LA MUNGU LINATOKA KATIKA KITABU CHA NABII ISAYA 45:1-7
Haya ndiyo Bwana amwambayo Koreshi masihi wake, ambaye nimeushika mkono wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake; tunakwenda kutiisha mwaka 2014, tunakwenda kuyatiisha mataifa yote, yatatiishwa chini ya miguu yetu, maadui zako watainama chini yako, wewe utawekwa juu asema Bwana wa majeshi.
Nami nitalegeza viuno vya wafalme; Bwana anakwenda kulegeza vile viuno vya matajiri, ile baraka itaamriwa ije kwako, zitatoka baraka kule zitakufuata mwana wa Mungu, anasema anakwenda kulegeza vile viuno vya wafalme ili wewe upate baraka za fedha. Tarajia akaunti zako kwenda kujazwa, huu ni mwezi Adari, mwezi wa kwenda kupigwa maadui zetu, wanaozuia riziki zetu.
Ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa, nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali malipoparuza; Bwana anakwenda kulegeza vile viuno vya wafalme atayafungua malango mbele yako, sasa baraka zinakwenda kufunguliwa, unakwenda kuvuka ukiwa na baraka. Yamkini watu wamekwaruza maisha yako, wamekuchafua jina lako, lazima utakasike.
Nitavunja vipande vipande; anasema Bwana asubuhi ya leo, anakwenda kuvunja vipande vipande, yamkini milango ya shaba inakuzuia, umemaliza mwaka hujapata ajira, leo mimi nakwenda kuvunja vipande vipande malango ya chuma. Yamkini mama mwaka unakwisha hujapokea mimba yapo malango ya chuma yamezuia, leo mimi kwa jina la Bwana, ninavunja vipande vipande hayo malango ya chuma, tena nakwenda kulegeza vile viuno vya wafalme wataleta baraka kwako.
Watakupandisha cheo, viuno vyao vitalegezwa, bosi wako utashangaa anakuita vizuri, yamkini wamesema maneno mengi juu yako, ya kukugombanisha na bosi wako ili ufukuzwe kazi, watakuona unatangazwa kuwa Mkurugenzi kwao. Wakakuwa chini yako, wewe ndio utapewa safari za kwenda mikoani, waliochonga juu yako Bwana atafanya mapinduzi, pokea baraka.
Na kukatakata mapingo ya chuma; nami nakwenda kukatakata mapingo ya chuma, yamkini kuna mapingo ya chuma, yanayozuia muujiza wako, yamezuia biashara zako, yamezuia amani ya ndoa yako, yamezuia mahusiano yako na mume wako, hayo mapingo ya chuma leo ninakwenda kuyakata. Nimepewa msimeno, mkasi wa moto ninakwenda kukata hayo mapingo ya chuma, yanayozuia muujiza wako, usipate safari za kwenda Ulaya, usifanikiwe, usipate amani, usipate kazi, biashara zako zisiende. Kabla hatujamaliza mwaka ninayakata hayo mapingo ya chuma, nataka uvuke ukiwa mwepesi kwa jina la Yesu, pokea baraka Bwana akuvushe ukiwa na baraka.

Nami nitakupa hazina za gizani; nataka nikupe hazina za gizani Mtanzania, na zile mali zilizofichwa mahalia pa siri, umaskini sio mpango wa Mungu, kukosa pesa sio mpango wa Mungu, kuwa omba omba sio mpango wa Mungu. Sasa Bwana anakwenda kuziinamisha hizi mbingu, anakwenda kutikisa, nataka Bwana akutendee, mapingo ya chuma yanakwenda kukatwa. Anasema mimi Bwana nitakupa zile hazina za gizani, ili upate kujua mimi ni Bwana niliye kuita kwa jina lako.
Watu wanasema wametendewa, kwa nini wewe haujatendewa? Kama hujatendewa labda ulisema vibaya juu ya mtumishi wa Mungu, unaambiwa hiogope Roho ya agano na huieshimu. Nilisha samehewa dhambi zote na Bwana, leo asubuhi nilikuwa nawaambia watumishi usicheze na mwenye agano, na wala usijilinganishe naye. Hata wewe unasesikia maneno, maneno hufuata sehemu palipo na kidonda, kunakuwa na connection ya mashetani kwako, ndio maana maneno yanapitia kwako, yanakuja Kanisani.
Hebu funga kata hizo nyaya, funga milango na madirisha, zuia maneno mabaya, kwanini wakuletee wewe maneno mabaya, kataa. Ukiona watu wanakuletea umbeya ujue na wewe unahasili ya umbea, kataa tena kata zile kamba, mwambie mimi siitaji niambie ya Yesu. Maneno yanavunja moyo ukiwa huna imani unavunjika, kuna watu hawana misingi ya imani, akisikia neno anavunjika. Kaa tayari masaa yote ukimtazama Yesu aliye juu, ukimuangalia Mungu aliye mwema, tazama matendo makuu, Mungu atembei na wenye dhambi.

MWISHO

Tupo Mbezi Salasala shuka kituo cha Mbezi Mbuyuni na Uliza kanisa la Nabii Flora
www.nabiiflora.blogspot.com
Picha na RUMAFRICA



Comments