RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

JE KUNA POSSIBILITY YA KUFIKA MBINGUNI KWA BABA KWA KAZI HII YA BLOGGING?

Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana hasa kwetu sisi mabloga wa Kibongo, tumekuwa tukifanya kazi hii bila hata ya malipo yoyote, tunatumia fedha zetu na muda wetu kuhakikisha tunakufikishia wewe issues zinzoendelea katika wingu la mwenyezi Mungu. Hii kazi ni tofauti sana na ukifananisha na kazi ya uimbaji wa nyimbo za Injili au mtumishi yoyote kwani tumeona wao wanapokuwa wakifanya kazi zao za uimbaji au kuhubiri mara nyingi hulipwa na wengi wamekuwa wakipelekana mahakama kama hujawalipwa au kudhurumiwa. Tumeona waimbaji wakubwa sana wakitapeli fedha za watumishi wao wanapokuwa wameaalika kuimba na wao kutokomea na kitita cha fedha.


Rulea Sanga yuko busy sana na matukio, Je atafika kwa Baba kwa kazi yake hii?

Bloggers wengi ni choka mbaya sana wao hufanya kazi hii kwa mapenzi ya Mungu, mara nyingi wamekuwa wakijituma kufika katika maeneo ya matukio kwaajili ya kupata habari. Pia wengine wakifika katika eneo hilo hulazimika kutoa kiingilio kama kuna kiingilio. Sasa mimi ninajiuliza hawa jamaa watauona ufalme wa Mungu kwa kazi yao hii isiyothaminiwa na wengi hapa bongo hasa blogu za Kikristo?

Bloggers wenzangu, mimi ninaamini hii ni kazi ya Mungu ya kufichua mabaya na kuonyesha mazuri ambayo wana wa Mungu wanafanya hapa dunia. Tunatakiwa kushikamana na kutoaangalia sana mshiko kwa Mungu wetu anajua kazi yetu hii. Ninajua inaumiza sana lakini ipo siku jina la BWANA litainuliwa kwa njia yetu hii ya blogging.Tusiwekeane kinyogo kwa wote tunafanya kazi ya kusambaza habari za Kristo kwa watu wetu ili wajue mishemishe zinazoendelea katika wigo wa Yesu Kristo.

Wewe kama mtalaam wa kukopi na kupesti fanya kwa juhudi zote kwani unafanya kwa mapenzi ya Mungu. Lengo letu ni kuona mwili wa Kristo unajengwa na wenye nguvu.

Mimi ni kutakie kazi njema na mafanikio siku ya leo..Amina

Weko katika Bwana
Rulea Sanga

Comments