RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWACHENI NABII TB JOSHUA AITWE NABII TB JOSHUA..ANAUSHANGAZA ULIMWENGU KWA KAZI ZAKE

Huyu mtumishi kwa kweli ananishangaza kwa kazi zake!!! Mimi kama Rulea Sanga nimetendewa makuu na mtumishi huyu Nabii TB Joshua. Kile kitendo tu cha kunialika kufika kanisani kwake na kusalimiana naye kwangu ni muujiza wa ajabu. Nabii TB Joshua katika watu wote duniani wanaosambaza habari zake katika mitandao aliona blogu ya RUMAFRICA ni ya kipekee na ikamagusa sana katika moyo wake na kutamani kumuona mmiliki wa blogu hii ambaye ni mkinga kutoka Makete aitwaye Rulea Sanga. Nilijiuliza mengi sana na kuiangalia blogu hii ina nini cha ajabu mpaka mtumishi wa Mungu TB Joshua kuipenda na kunialika kanisani kwake. Kwa akili ya kibinadamu unaona si kawaida. Nimekuwa nikifanya kazi za kusambaza habari za watumishi wa Mungu na sijaona mtumishi kama TB Joshua kwa upendo wake na kuthamini kazi za watu wanaofanya kazi ya Mungu. Hii ni changamoto kwa watumishi wengine wa Mungu hapa Tanzania na nchi zingine. Watumishi mnatakiwa kuwajali hawa watu wanaowasambazia huduma yenu na ikajulikana duniani kote. Kazi hii sio ndogo ni kazi kubwa sana. Nabii TB Joshua aliona hilo na ndio maana aliamua kunitia moyo ili nisonge mbele kwa kazi ya Bwana.

Jamani nasema hata leo nikifa na nikabahatika kuonana na Mungu, nikaulizwa juu ya watumishi wa Mungu waliokushangaza duniani, nitasema ni Nabii TB JOSHUA hata kama wengine wapo lakini huyu kaniwezesha kufika sehemu ambayo watu wengi duniani wanatamani kufika lakini wanashindwa kufika. Wengine ni mamilionea watamani kumuona mtumishi wa Mungu inashindiakana kutokana na ubise alionao.
http://thetbjoshuafanclub.files.wordpress.com/2010/07/mpg.jpg

BAADHI YA VITU NILIVYOJIFUNZA NIKIWA SCOAN

Kuna mambo mengi nilijifunza katika kanisa lile

KUJISHUSHA
Nabii TB Joshua ni tofauti sana na unavyomuona katika TV, baada ya kutoka katika TV huwa katika maisha ya kawaida sana, hufanya kazi kama watumishi wengine.

KUCHAPA KAZI
Nabii TB Joshua anafanya kazi kama punda, siku moja nimeshuhudia Nabii TB Joshua akihudumia watu kuanzia asubuhi mpaka saa tisa usiku. Nilijiuliza maswali mengi sana. Na kulipopambazuka akaendelea kufanya kazi ya Mungu kama kawaida na kwa nguvu zote.

WAUMISHI WAKE
Watumishi wenzake wanafanya kazi kama nyuki kwa kushirikiana na wanafanya kazi zao kwa umakini na haraka.

TARATIBU ZA KUMUONA NABII TB JOSHUA
Taratibu za kumuona Nabii TB Joshua zimewekwa kwa mpangilio, watu wanaenda kwa kufuata namba zao na sio kiholela holela.

WAIMBAJI
Jambo liliniacha mdomo wazi ni pale nilipoona waimbaji wanafanya usafi, yaani wanafagia kanisa. Nilijifunza mengi sana kupitia waimbaji hawa. Haijalishi wewe ni wa namna gani, kwa Mungu wote ni sawa na hakuna ubaguzi.

UWEPO WA KIMUNGU NDANI YA KANISA
Ukiingia kanisani kwake kuna hali fulani unapokea au unaona kama kuna mabadiliko fulani katika mwili wako. Kanisa lake ni tulivu sana na unahisi uwepo wa Mungu.

TELEVISHENI ZAKE
TV zake zilizozagaa kila kona ya kanisa lake muda wote zinaonyesha matendo makuu yanayofanyika katika kanisa lake, yaani ibada zake, shuhuda, matendo makuu na mambo mengi yanayohusu SCOAN

UKARIMU
Muda wote niliokuwa huko sijawahi kuona Nabii TB Joshua akiwa amenuna, muda wote ni mtu wa kutabasamu tu. Ukimwangalia unahisi kufarijika hata kama hajasema neno lolote kwako.

UFUGAJI
Nabii TB Joshua ni mtu anayependa sana mifugo, niliweza kuona ngamia, farasi, ndege wa aina mbalimba, kuku, sungura na wanyama wengi wamefugwa na wenye afya nzuri

MICHEZO
Nabii TB Joshua anaonekana kupenda sana michezo, niliweza kuona team yake ya mpira wa miguu. Timu hiyo waliowengi ni yatima na vijana wa mitaani waliochukuliwa na Nabii TB Joshua kwa lengo la kuwalea na kuwasomesha.
USAFIRI
Kuna jambo lilinishangaza sana. Kanisa lake na sehemu ya kulala sio mbali sana ni kama mita 100 au 200, lakini Nabii TB Joshua hutumia magari yake kuwachukua wageni na kuwapeleka kanisani. Nilichojifunza ni kwamba huyu mtu ana upendo kwa wageni na hatamani kuona wageni wake wanasumbuka wanapokuwa katika kanisa kwake.

Jamni ni mengi mengi mengi nilijifunza, nitazidi kufunguka ili na wewe uweze kujua mengi kuhusiana na safari yangu ya SCOAN 2012

TUONE KAZI ZA NABII TB JOSHUA


Nabii TB Joshua akijishusha na kuwa kama mtu wa kawaida kuwasaidia wenye shida
http://osujiinnocent.files.wordpress.com/2013/08/tb-joshua.jpg
Nabii TB Joshua bila ya kuangalia umaarufu wake na heshima anayopewa na mataifa, bado kazi za kijamii ianafanya kama zamani.

Hii ndio kazi ya Bwana. TB Joshua hakika anafanya kazi ya Mungu, anakula na wenye shida

Zuleika with Prophet TB Joshua

http://distanceisnotabarrier.files.wordpress.com/2010/02/tb-joshua-with-evelyn.jpg
TB Joshua na Evelyn
http://distanceisnotabarrier.files.wordpress.com/2010/02/tb-joshua-with-christians.jpg
Evelyn alipopokea zawadi na Nabii TB Joshua
http://distanceisnotabarrier.files.wordpress.com/2010/02/nissan-car-gift.jpg
Nissan aliyopewa Evelyn na TB Joshua
tb-joshua-prophecy 1
Mh. Edward Lowasa wa 9 kutoka kushoto ndani ya SCOAN
http://tbjoshuawatch.files.wordpress.com/2011/04/the-scoan-auditorium.jpg
Maelfu ya watu wanaohudhuria ibada zake ndani ya SCOAN

Nabii TB Joshua anapokuwa katika kumtafuta Bwana kwa kusoma Habari za Njema katika vitabu mbalimbali
Photo: TB Joshua then. 1997.
Nabii TB Joshua mwaka 1997

Enzi hizo Nabii TB Joshua akiwaombea watu wenye shida mbalimbali
Click for Full Image Size
Jamani huyu mtumishi wa Mungu Nabii TB Joshua, Mungu azidi kumuongezea upako kwani katoka mbalimbali sana katika huduma yake hii ambayo ni ICON duniani

Comments

jane said…
Kwakweli rule Hutu Mtumishi sijawahi kuona ana roho ya ajabu sana anasaidia wenyeshida ana upako was ajabu sana huwa ananivutia sana na natamani siku moja nikamwone live IPO siku mungu atanipeleke tu name nazidi kumuombea kwa mungu azidi kumbariki na watumishi engine wage basis mfano was Hutu Mtumishi watoto yatima na wajane ni wengi sana wanahitaji Faraja name wakuwapa Faraja no watumishi was mungu na sisi tuliookoka. Mungu akubariki sana rule.JANE Mbezi luis