RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ALINE VYUKA, MWANA DADA MWENYE NDOTO ZA KUFIKA MBALI, AENDELEA KUFANYA VIZURI HUKO USA


Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Burundi na muigizaji wa filamu anayeishi huko Marekani, DUKUDE VYUKUSENGE aka ALINE VYUKA aendelea kujizolea sifa kwa kuvitumia vipaji alivyopewa na mwenyezi Mungu.

Akiongea na mwalimu John Shabani (Katibu mkuu wa chama cha muziki wa injili Tanzania), Aline amesema kuwa, anajua kule Mungu aliko mtoa, hivyo ana maono ya kwenda mbali zaidi ki huduma, kielimu na kijamii.

Aline Vyuka ambae alianza kuimba kwenye kwaya akiwa na umri wa miaka 7, miwili iliyopita aliweka hewani album yake 'Vyukusenge Vol 1' na baada ya hapo aliweka akaja na album yake ya pili 'Dukunde Vol2' Nyimbo ambazo zimempa chati sana. Lakini hata hivyo Aline hajaridhika na kiwango chake cha uimbaji, anatamani kufanya vizuri zaidi, hivyo basi katika kuboresha huduma yake ya uimbaji, mwanadada huyo amekuwa akifanya kila awezalo ili kuwa mwimbaji bora. Moja ya waalimu wa nyimbo za injili walioamua kusimama na Aline ni mwalimu John Shabani . Mungu akipenda mwaka huu mwana dada huyo anatarajia kutembelea nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Tanzania na kurekodi nyimbo zake mpya.

Pia Mwana dada huyo anajiusisha na mpango mzima wakuigiza filamu. Mwaka 2010 filamu yake 'Family issues' iliwekwa hewani na ikamletea sifa kemu kemu kwa upande wawapenzi wa filamu. Mwaka wa 2013 ali iweka wakfu filamu yake ya pili 'ORPHANS'. Ukizingatia kuwa dada huyo ana mpango kabambe wa kuwasaidia watoto yatima na mabinti waliozalishwa majumbani.Pamoja na ugumu kidogo wa kipato lakini kwa maombi yako na ushauri wako na hata pia mchango wako, vitamsaidia kufika mbali. Aline analo kundi linalo igiza filamu zake na yeye ndio kiongozi wahilo kundi,linajulikana kama 'BAHOWOOD' akitambulika ka Director na Muandishi (Story writer) kwenye filamu zote ambazo zilishatoka.
Mwsho Aline ametujulisha kuwa :" Ninaandaa filamu itakayojulikana kama INTERPRET "
Endelea kumwombea!

Akirekodi mkanda wa video

Akiwa na rafiki yake baada ya ibada huko mareakani



Ndani ya studio

Chanzo cha Habari: John Shabani

Comments