RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KUNA WATU MUNGU AMEWAPA VIPAJI LAKINI CHA JULIET DOUGRASI NI KIBOKO

Nimesikia nyimbo nyingi za waimbaji lakini niliposikia za huyu dada hakika niliamini ya kwamba Mungu ni wa ajabu. Unaweza kusikia mtu fulani kaimba vizuri sana na ukafikiri hakuna mwingine anaweza kuja kuimba zaidi yake. Tumeona waimbaji waliotamba na wanaotamba kwa nyimbo zao kama vile Solomon Mkubwa, marehemu Chibalonze, marehemu Sedekia, Rose Muhando, Martha Mwaipaja na wengine wengi. Hawa waimbaji wamekuwa wakifanya vizuri sana kwa utukufu wa Mungu.

Juliet Dougras

Lakini kuna watu ambao Mungu anazidi kuwaandaa kwa kazi yake kwa vizazi vijavyo, na leo hii kainua mtumishi wake Juliet Dougras kutoka Bukoba. Mwimbaji huyu kwa umbo ni mdogo sana lakini viti alivyonavyo ni vikubwa sana. Nyimbo zake ukisikiliza utatamani Mungu angeshuka ili akuchukue. Nyimbo zake zina ule mguso wa ajabu sana na ukizidi kusikiliza unahisi ubaridi na vipele kusisimka. Jamani sijui nisemeje lakini muombe Mungu ujipatie albamu yake inayoenda kwa jina la U MTAKATIFU ya JULIET DOUGRASI. Itakuwepo sokoni hivi karibuni.

Na kama hujui, huyu dada ameishi na familia ya waimbaji machachari ambao kwa sasa makazi yao yako Marekani na sio wengine ni J-SISTERS. Juliet Dougras anasema hawa wamekuwa msaada mkubwa sana katika kuchochea karama ya uimbaji.

Akiongea na Rumafrica, Juliet Dougras alisema karama ya uimbaji alikuja kuitambua mwaka 2008 na kujiona kumbe anaweza kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji, na hapo alianza kuichochea kwa bidii na kujiunga na kwaya.

Rumafrica imepanga siku ya kufanya mahojiano na huyu dada ili tujui mengi kutoka kwake,

Unaweza kuwasiliana naye kwa simu +255 659 474 667

Comments